Tafadhali CUF msidanganyike kurubuniwa kumrudisha Prof Lipumba uongozini.

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Mimi niseme tu ukweli kua CUF katika kitu ambacho hamtasahau katika maisha yenu ni wakati Prof Lipimba alipoamua kujiuzulu uenyekiti wa chama taifa huku chama kikiachwa kama yatima,katikati ya kampeni za uchaguzi mkuu, huku akiwa ameshiriki katika maandalizi yote ya kampeni, ameshiriki vikao vyote.Maalim Seif mzee wa watu ahamgaikie ya visiwani na bara kwa wakati moja! Iliumiza sana! Kama alikipenda chama ni kwanini aondoke katikati ya kampeni? nia yake ya kujiuzulu katikati ya kampeni ilikua nini kama si kukiangusha chama?

Binafsi namchukilia kama mtu aliyekosa huruma na subira, ni mtu ambaye hakuangalia maslahi ya chama,ni mtu aliyefanya kitendo ambacho ni kama makusudi flani ili chama kiangukie pua kwenye uchaguzi.

Huyu huyu Lipumba aliyejiuzulu uongozi akakimbilia uwanja wa ndege under escort ya ulinzi mkali wa wanausalama kupumzika Rwanda au mwingine?

Hawa wanaomfuata Lipumba nyumbani kwake ati kumshawishi arudie nafasi yake ya uenyekiti wa chama waogopeni kama ukoma, wanatumiwa hawa.Sidhani ndani ya CUF kama kuna kiongozi makini na mwenye subira na shupavu kama Maalim Seif, huyu ndiye roho ya chama .Angalieni wakati Lipimba alipokua mwenyekiti awamu zote chama kulikua na wabunge wangapi bungeni? Wamulikeni vizuri wababaishaji hawa wanaotumiwa kutaka kuanza kukivuruga chama.

Prof Lipumba ni mwanauchumi wamwache afanye kazi zake akiwa amepumzika, Kwa muda alikokifikisha chama inatosha! Msidhani kwamba eti Lipumba angekuwepo amgeweza kufanya masmuzi yeyote kule visiwani, isingewezekana kabisa kwani hatua ambazo chama kinaenda nazo hivi sasa hayana shida ni ya kizalendo zaidi na sahihi.
 
Mimi natofautiana mleta mada kwa sababu Prof. Lipumba japo kitaaluma ni mchumi, ila kiukweli he is a politician by professional, ameifanya siasa ndio ajira yake ya kudumu na hana shughuli nyingine yoyote ya kufanya, au jambo jingine lolote la kufanya ili kuendesha maisha kama yule dr mihogo!.

Mtu amegombea mara 4 na zote amekataliwa hakuwahi kupata hata asilimia 5% lakini kila baada ya miaka 5 lazima awe mgombea wa CUF hadi kufikia yeye na sharubu kujihesabu wao ndio wagombea pekee wa kudumu wa CUF kwenye urais, ndio maana kuliko kukosa kugombea, bora apokee kile kidogodogo cha CCM, na kujitoa ili CUF ivunjike!, kajitoa, CUF haikuvunjika!, fungu alilopewa ni kiduchu tuu!, afadhali mwenzake kapewa mkataba mrefu, yeye fungu limeishamuishia na hana namna nyingine yoyote ya kuendesha maisha yake!.

Sasa CUF wasipomrudisha atafanya nini kingine?!, kwa sababu ubunge au udiwani hawezi kupata kwa sababu hachaguliki!, unategemea nini kwa mtu kama huyu?!, nawaomba CUF please mrudisheni tuu Prof. Lipumba kwenye nafasi yake.

Pasco
 
Huo ushauri wenu pelekeni kwenye maskani za cuf kama pale lozana kwa wanachama kindakindaki wa chama muone kama mtatoka salama
 
Sijui kwa nini hamtaki kusema hadharani kuwa Lowasa ndio chanzo cha mivurugano kwenye vyama vya Upinzani.

Kuanzia Chadema,CUF na NCCR mageuzi.....kifupi jamaa kavuruga sana mstakabali wa Upinzani Tanzania.

Nashangaa watu kuwalaumu Dr.Slaa Na Lipumba kuwa ni wasaliti wakati walituaminisha kuwa hata bila wao saa nne asubuhi wapo Ikulu.

Naamini Mzimu wa Lowasa utautafuna Upinzani miaka mingi ijayo.!
 
Cuf haina watu
wangekuwepo wangeziba pengo so fast usinge notice
Lipumba bado relevant sababu nne kubwa

1.kwanza ni smart kila anachoongea watu wengi wanakubali hata kimyakimya

2.pili hana njaa...hataki kulipwa chochote na CUF....ni kama anajitolea....

3. Bado anajulikana zaidi kuliko mwanachama yeyote wa bara wa CUF..umaarufu nao ni mtaji.kwenye siasa za TZ...

4. wafuasi wa CUF wa bara wanajua alichokuwa anakipigania kupunguza influence ya wana CUF wa Visiwani
huwezi kushindana na kina Seif hasa kama una njaa njaa muulize Hamad Rashid
 
Lipumba na Slaa ni wasaliti wa vyama vyao wasiostahili msamaha kamwe.
Askari yeyote anayejiunga na adui wakati wa vita kali adhabu yake ni.........
Hata hivyo, kama Lipumba na Slaa wana nguvu za kisiasa, waanzishe vyama vyao au wajiunge kwingine na siyo warudi walikotoka.
 
Kulinganisha wabunge aliovuna Lipumba na seif kipindi Lipumba hayupo ni ujuha wa kiwango cha lami,

Cuf imeongeza idadi ya wawakilishi chini ya mwamvuli wa ukawa ambapo hapo mwanzo.haukuwepo..

Katika hoja ya eti kukosa huruma na subira kwa Lipumba ni mufisi, cuf wao walikosa subira ya kutokubaliana na kumpokea fisadi lowasa katika umoja wa ukawa ni kitendo.cha kukosa uungwana na subira..

Lipumba Ana mchango mkubwa katika kuimarisha uhai wa chama cha wananchi Cuf.
 
Mimi natofautiana mleta mada kwa sababu Prof. Lipumba japo kitaaluma ni mchumi, ila kiukweli he is a politician by professional, k ameifanya ndio ajira yake na hana lolote jingine la kufanya kama yule dzoter mihogo!. Mtu amegombea mara 4 na zote amekataliwa hakuwahi kupata hata asilimia 5% lakini kila baada ya miaka 5 lazima awe mgombea wa CUF hadi kufikia yeye na sharubu kujihesabu wao ni wagombea wa kudumu!, CUF wasipomrudisha atafanya nini kingine?!, kwa sababu ubunge hawezi hata udiwani hachaguliki!, anategemea nini kwa mtu kama huyu?!, CUF mrudisheni Prof. Lipumba!.

Pasco
"Kitaaluma ni mchumi lakini he is a politician by professional??"
Boss unataka kutuaminisha wanabodi kuwa "taaluma" na "profession" ni maneno mawili tofauti?
 
Lipumba ni adui wa Cuf kuliko hata ccm ya kisiwandui , kwanza alidumaza cuf kwa miaka mingi sana , huyu hafai hata kuwa mwanachama tu wa cuf achilia mbali uenyekiti , huyu ameonekana kwenye mitandao akipiga bia kigali baada ya kusaliti , mnataka nini ili mjue huyu mtu ni nyoka ?
 
Cuf wameliona kosa lipumba anarudi,kazi ipo kwa kambale waliouza chama kwa lowassa
 
Kulinganisha wabunge aliovuna Lipumba na seif kipindi Lipumba hayupo ni ujuha wa kiwango cha lami,

Cuf imeongeza idadi ya wawakilishi chini ya mwamvuli wa ukawa ambapo hapo mwanzo.haukuwepo..

Katika hoja ya eti kukosa huruma na subira kwa Lipumba ni mufisi, cuf wao walikosa subira ya kutokubaliana na kumpokea fisadi lowasa katika umoja wa ukawa ni kitendo.cha kukosa uungwana na subira..

Lipumba Ana mchango mkubwa katika kuimarisha uhai wa chama cha wananchi Cuf.
Mchango upi ? Kama chama hakikushinda chaguzi huo mchango wake uko kwenye nini ? Uongo utakusaidia nini ?
 
Lipumba ni adui wa Cuf kuliko hata ccm ya kisiwandui , kwanza alidumaza cuf kwa miaka mingi sana , huyu hafai hata kuwa mwanachama tu wa cuf achilia mbali uenyekiti , huyu ameonekana kwenye mitandao akipiga bia kigali baada ya kusaliti , mnataka nini ili mjue huyu mtu ni nyoka ?

Inashangaza sana enyi chadema kuongelea cuf...
 
hakuna adui wa kudumu katika siasa, Lipumba arudishwe, ata mzee wa kubadili gia angani, angebadilisha gia uko uko angani akamrudisha Dr Slaaa, kwa ustawi wa chama, na sio kwa ustawi wa chuki
 
Kuna watu hawajawahi kufanya lolote katika siasa za mageuzi kufikia sacrifice ya Lipumba lakini wanathubutu kuinua midomo kumtusi. Huku ni kukosa staha tu. Busara ni kukaa kimya na kumuheshimu angalao kidogo kwa kile alichowahi kufanya. Tumtendee haki na tusitumie jazba
 
Mimi niseme tu ukweli kua CUF katika kitu ambacho hamtasahau katika maisha yenu ni wakati Prof Lipimba alipoamua kujiuzulu uenyekiti wa chama taifa huku chama kikiachwa kama yatima,katikati ya kampeni za uchaguzi mkuu, huku akiwa ameshiriki katika maandalizi yote ya kampeni, ameshiriki vikao vyote.Maalim Seif mzee wa watu ahamgaikie ya visiwani na bara kwa wakati moja! Iliumiza sana! Kama alikipenda chama ni kwanini aondoke katikati ya kampeni? nia yake ya kujiuzulu katikati ya kampeni ilikua nini kama si kukiangusha chama?

Binafsi namchukilia kama mtu aliyekosa huruma na subira, ni mtu ambaye hakuangalia maslahi ya chama,ni mtu aliyefanya kitendo ambacho ni kama makusudi flani ili chama kiangukie pua kwenye uchaguzi.

Huyu huyu Lipumba aliyejiuzulu uongozi akakimbilia uwanja wa ndege under escort ya ulinzi mkali wa wanausalama kupumzika Rwanda au mwingine?

Hawa wanaomfuata Lipumba nyumbani kwake ati kumshawishi arudie nafasi yake ya uenyekiti wa chama waogopeni kama ukoma, wanatumiwa hawa.Sidhani ndani ya CUF kama kuna kiongozi makini na mwenye subira na shupavu kama Maalim Seif, huyu ndiye roho ya chama .Angalieni wakati Lipimba alipokua mwenyekiti awamu zote chama kulikua na wabunge wangapi bungeni? Wamulikeni vizuri wababaishaji hawa wanaotumiwa kutaka kuanza kukivuruga chama.

Prof Lipumba ni mwanauchumi wamwache afanye kazi zake akiwa amepumzika, Kwa muda alikokifikisha chama inatosha! Msidhani kwamba eti Lipumba angekuwepo amgeweza kufanya masmuzi yeyote kule visiwani, isingewezekana kabisa kwani hatua ambazo chama kinaenda nazo hivi sasa hayana shida ni ya kizalendo zaidi na sahihi.[/QUOTE
Kwa maelezo yako yaelekea wewe si mwanachama wa cuf, je utakuwa una shauri ukisimamia wapi ili ujulikane na wenyewe kisha ushauri wako upewe uzito maana hujaji tambulisha, sioni iwezekane vipi chui ampe ushauri mbuzi juu ya njia ya kupita itakuwa ni muhali tu.
 
Back
Top Bottom