TADB kwa masharti haya bakini tu na hela zenu,

Vitalis Msungwite

JF-Expert Member
May 11, 2014
3,269
7,779
Tar 12/10/2018 mmoja kati ya viongozi wa benki ya maendeleo ya kilimo (Tanzania Agricultural Development Bank) alikuja kuongea na wanachama cha ushirika Madibira. Ushirika unawanachama 3147 ambao kila mmoja anamiliki eneo la hekta moja (2.5 ekari). Katika maelezo yake ya kuipamba benki hiyo alisema kuwa benki hiyo imeanzishwa ili kuwasaidia wakulima nchini kote. Aliongeza kuwa benki hiyo hutoza riba ya 8% - 12% ya pesa. Lakini masharti yao ni yafuatayo.

1: Mkopeshwaji toka benki ni chama.

Hapa alieleza kuwa wao watakopesha chama na chama kitamkopesha mkulima. Kwamaana kuwa wao hawahusiki na mwanachama gani kakopa kiasi gani!. Hapa chama cha ushirika kinabeba dhamana ya kuwa mkopeshaji wa pili na mkopaji wa kwanza toka benki. Chama kinachukua majukumu ya udhamini na ukopeshaji.

2. Masharti kwa chama cha ushirika

Chama cha ushirika kinatakiwa, kuandika barua ya maombi na kuituma makao makuu ya benki, kuitisha mkutano maalum na kuwaambia wanachama lengo la kujiunga na kuwatumia muhtasari, kupeleka nakala ya kitabu cha wanachama, katiba ya chama, TIN ya chama, bank statement za chama, taarifa za madeni ya chama, taarifa za kibiashara za chama, taarifa ya mkaguzi wa vyama vya ushirika, leseni ya usajili wa chama na ratiba ya zao (kukatua, kuwatika mbegu, kuvuruga,kupanda,uwekaji mbolea,magugu mpaka uvunaji) na Mali za chama kutumika kuchukulia mkopo.

Kwakifupi kuhusu Mali za chama ni ardhi, majengo, miundo mbinu ya maji na barabara, magari, trekta, kombain, rice milling machine, ofisi mbalimbali .

3: chama kitakopesha pembejeo za kilimo kulingana na kalenda ya zao.
Hapa alifafanua kuwa watatoa mbole, dawa za magugu na pesa zinazohitajika kwa wakati husika tu.

Hayo ni baadhi ya masharti ya benki hiyo. Kutokana na hayo naomba niwaambie kuwa bakini tu na hela zenu. Benki nyingine washindani kama CRDB, NMB na MUCOBA wanatoa pesa kwa wakulima moja kwa moja, chama huthibitisha tu kuwa muombaji ni mwanachama au la!. Pia taarifa mnazozitaka ni very confidential na ni sawa na kukikabidhi chama na huenda mwisho wa siku yakatukuta ya kapunga kuuzwa kwa wawekezaji.

Tulishawahi kupata mikopo ya matrekta na Powertila toka taasisi mbalimbali ikiwemo na suma JKT lakini chama hakijawahi kuweka poni Mali zake, mikopo huwa ni kati ya mwanachama na mkopeshaji. Lakini kwa masharti yenu haya,
Bakini tu na hela zenu ni bora tukakope kwenye benki za 20% - 30% ambazo hazirisk Mali za chama chetu kuliko kimkopo chenu chenye masharti kibao utafikiri tunataka kuchumbia.
 
Back
Top Bottom