Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,286
- 10,831
Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imekanusha taarifa iliyochapishwa na gazeti la Mwananchi iliyosema wafadhili wajitoa dawa za UKIMWI.
TACAIDS imesema taarifa hiyo si ya kweli hakuna wafadhili waliojitoa, kwa kuwa hadi sasa mahusiano ya Tanzania na wafadhili yako vizuri.
Wamesema taarifa sahihi ni kuwa kwa muda wa miaka 8 fedha za wafadhili zilipungua kwa baadhi ya mambo ya mapambano ya UKIMWI na hiyo sio kwa Tanzania pekee bali nchi zote zinazotegemea wafadhili.
Kutokana na hilo, serikali iliunda Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI(ATF) ambao umewezesha serikali kununua septrin kwa miaka mitatu mfululizo.

au mnasemaje??
kwa combination ya dawa moja tu tukumbuke kuna regimen zaidi ya 10 za ARV ambazo zinakua prescribed kwa wagonjwa tofauti tofauti kulingana indication zao na mahitaji. Hapo bado matibabu ya magonjwa nyemelezi, kukinga na kuzuia maambukizi mapya, Uzazi salama, vijana, N.K