Tabora waliichagua CCM lakini CCM imewalipa mateso

Tabora waliichagua CCM lakini CCM imewalipa mateso

Halmashauri ya Manispaa ya Tabora mjini (inayoongozwa na CCM) imepandisha kodi ya majengo kutoka Sh.10,000/= hadi 25,000/= kwa jengo moja.

Ongezeko hili lina kasoro zifuatazo;

#MOSI
Ongezeko hili limepangwa kienyeji kinyume cha sheria ya Serikali za mitaa No.7 ya mwaka 1982 (The Local Government Act (Urban Authorities,1982. No. 7). Sheria hii inataka upandishwaji wa kodi ya majengo (property tax) ufanywe kwa maazimio ya kikao cha "Full Council" yani watendaji wa Halmashauri, Madiwani wote plus wenyeviti wote wa mitaa na vitongoji.

Lakini kwa Tabora haijafanyika hivyo. Mkurugenzi na watu wake wamejifungia ndani wakajipangia bei walivyotaka. Haya ni matumizi mabaya sana ya madaraka. Wamejiamulia tu kupanga kwa sababu wanajua wananchi hawawezi kukataa. Huu ni ubabe, ni wizi na unyang'anyi.

Cha ajabu eneo hili lina Mbunge na hajatoa kauli yoyote kuhusiana na suala hili. Kukaa kimya kwa Mbunge huyu inamaanisha kuwa anakubaliana na "wizi" huu wa Halmashauri. Kama hakubaliani nao mbona asitoe kauli ya kupinga? Kwanini asiwakosoe halmashauri kwa kufanya maamuzi kienyeji bila kuitisha "full council meeting" kama sheria inavyotaka?

Ukimya wake unamaanisha nini? Kwamba yuko "neutral"?. Albert Einsten aliwahi kusema ukiwa "neutral" mahali ambako mnyonge anaonewa inamaanisha unamuunga mkono yule anayemuonea mwenzie. Mwalimu Nyerere nae akasema ukimuona tembo ameweka mguu wake kwenye mgongo wa chura, halafu ukajifanya upo "neutral" hakika chura hataelewa "neutrality" yako. Je hivi ndivyo Mbunge huyu wa CCM Tabora (Emmanuel Mwakasaka) alivyoamua kuwa neutral wakati wananchi wakionewa?

#PILI
Ongezeko hili ni kubwa sana. Halilipiki. Kupandisha kodi kutoka 10,000/= hadi 25,000/= ni ongezeko la asilimia 150%. Hiki ni kiwango kisichovumilika na ni kumtesa mwananchi maskini aliyehangaika kujenga nyumba yake miaka na miaka.

Yani kiwanja anunue mwenyewe, nyumba ajenge mwenyewe kwa kuhangaika na kukopa halafu halmashauri mje mpandishe kodi kienyeji vile mnavyojisikia? Hivi CCM mkoje? Hamuwezi kuendesha serikali bila kuwadhulumu watanzania? Sisemi watu wasilipe kodi. Nataka walipe, lakini sio kwa kiwango hiki cha kukomoana. Asilimia 150% ongezeko? Hapana, hata ingekuwa mimi silipi.

Kwanini haikupanda kwa asilimia 20% au 50% walau ifike 12,000/= au 15,000/=?? Nani aliyefanya upembuzi yakinifu na kupendekeza ipande kwa 150%?

Hivi serikali haijui kuwa kodi ikiwa kubwa sana inachangia watu wengi kukwepa maana inaumiza? Ni wajibu wa kila mwananchi kulipa kodi lakini inabidi iwe "reasonable". Haiwezekani kodi ipande kwa 150% halafu utegemee watajitokeza wengi kulipa. Wengi watakwepa.

Wakati halmashauri ya jiji la Arusha inayoongozwa na CHADEMA imepandisha "property tax" kwa asilimia 5% wenzao Tabora wamepandishwa kwa asilimia 150%. Yani wananchi wa Tabora wananyonywa mara 30 kuliko wa Arusha (150% ÷ 5%).

Kwa kufanya hivi Halmashauri ya Manispaa Tabora imeweka rekodi ya kuwa Halmashauri ya kwanza nchini kupandisha kodi ya majengo kwa kiwango kikubwa zaidi. Cha ajabu wananchi hawa wananyonywa hivi lakini waliichagua CCM kuanzia madiwani, wabunge hadi Rais. Ndio maana huwa nasemaga ili uwe mfuasi wa CCM unahitaji degree nyingi sana za ujinga. Haiwezekani unyonywe hivi halafu uko busy kusema "CCM hoyee". Lazima utakuwa na shida ya akili.

#TATU,
Kodi hii haiakisi uhalisia. Kiasi cha shilingi 25,000/= kilichopangwa na Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ni kwa majengo yote. Yani mwenye ghorofa atalipa 25,000/=, mwenye vyumba viwili atalipa 25,000/=, na mwenye chumba kimoja atalipa 25,000/=. Hii si haki hata kidogo.

Tozo hii ilipaswa iendane na tathimini ya nyumba husika. Haiwezekani mmiliki wa kiwanda alipe 25,000/= na mkulima maskini wa tumbaku mwenye chumba kimoja nae alipe 25,000/= eti kisa yote ni majengo. Huu ni wizi wa mchana kweupe.

Haiwezekani nyumba ya bati, nyumba ya makuti, nyumba ya nyasi, nyumba ya tofali na nyumba ya matope zote zilipe kiwango sawa cha 25,000/=. Huu ni unyonyaji uliopitiliza.

Lakini je hivi Halmashauri ya manispaa ya Tabora imekosa vyanzo vingine vya mapato hadi kuamua kunyonya wananchi kikatili namna hii?

Naomba kamanda Hawaa Bananga (Mbunge viti maalumu CHADEMA mkoa wa Tabora) uwasaidie hawa ndugu zako kupata haki yao maana mbunge wao waliyemchagua ameshindwa kuwasaidia.

Kodi hii ipunguzwe (iwe reasonable) na pia ifanyike tathmini ambayo itasaidia kila nyumba kulipa kulingana na aina yake ya Ujenzi. Haiwezekani nyumba ya tope na nyumba ya ghorofa zikalipa sawa.

Malisa GJ.!
kwa kuwa mlichagua ccm hapo kwao ni rahisi kuandika muhstasari feki wa kikao na kusema kikao kilifanyika na hakuna hatua yoyote watakayochukuliwa, mfano ni hati feki waliyoipeka kwenye uchaguzi wa meya dar,hakuna hatua yoyote aliyochukuliwa yule aliyepeleka barua feki kwa kuwa ni ccm
 
Arusha mjini,moshi,mbeya,ilemela,nyamagana n.k.haya ni baadhi tu ya maeneo ambayo upinzani umeyaongoza na kufanikiwa kuyatoa katika lindi la umaskini.sasahivi dsm ipo chini ya UKAWA sasa subiri uone maendeleo ya kweli.

Hayo maeneo uliyotaja nikienda tawakosa omba omba ?
Hakuna watu wanye umasikini?
Wajinga sana nyie na babu yenu
 
Hayo maeneo uliyotaja nikienda tawakosa omba omba ?
Hakuna watu wanye umasikini?
Wajinga sana nyie na babu yenu
Maeneo niliyokutajia ni tofauti na maeneo ambayo ccm imechukua majimbo yote ya mkoa kama dodoma.hakuna mkoa maskini na wenye omba omba kama dodoma ambapo ccm ndo inaongoza majimbo yote.
 
angalia mikoa yote ambayo wameichagua ccm ndio inaongoza kwa umaskini.
na ndio hao hao kutwa wanaimba hapa kazi tu baada ya muda wanalia njaa
Hao ambao wanaongoza kwa utajiri mbona wanafanya kazi ya kuimport wanaume kutoka Kenya?. Mbona wameshindwa kupambana na viroba na bangi?. Mbona maendeleo yao yanashindwa kuwazua wasiendelee kulalamika hovyo kila kukicha?. Achana na mawazo ya kitumwa.
 
Kilimanjaro tuliichagua watu wanaojua wananchi wao vizuri jinsi walivyo sio kwamba tuna shida ya vitu kama hivyo bali tunataka watu wanaowajali wananchi na wasio na maringo na vyeo tulivyowapa sisi ndio maana tunachagua upinzani watu ambao hawachoki kuwasikiliza wale waliowachagua
Hata hivyo poleni sana naona bado mnadanganywa na kofia kanga tisheti elfu kumi kumi ishirini na mwisho mnaenda kuwachagua kuleni theni msiwachague upinzani uko kwa ajili yenu mnaambiwa then mnaziba masikio
Kwa sababu ya hicho kiburi chenu ndio maana mkataka kujitenga muwe na jimbo la kaskazini?. Akili matope hizo.
 
Ni nani aliyeisahau Tabora na kuinyima Maendeleo toka Uhuru?Kumbe unakiri kwa kinywa chako kuwa CCM na serikali zake zimeinyima Tabora maendeleo,lakini kwa njaa yako na umasikini wa kipato ulionao,ukaona bora upokee kofia,T-shirt,kanga na sh.5000/pamoja na sahani ya wali maharage ili uichague ccm iendelee kukutawala.

Kweli ccm inanufaika na ujinga wa Watanzania,jitu linakiri kuwa ccm haijafanya kitu toka Uhuru,lakini haliachi kuichagua tena na tena.Endeleeni tu na ujinga wenu na mtaendelea kubaki nyuma kimaendeleo hadi pale mtakapozinduka na kuanza kudai haki zenu.

Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya umasikini wa Watanzania na ccm,maeneo yote yaliyokithiri kwa ufukara wa kipato ndiyo yanayoongoza kuichagua ccm,hii ni aibu sana.
Na nani aliyeikumbuka Tabora, unakiri kwa kinywa chako kuwa sasa serikali ya CCM imeikumbuka Tabora au siyo?
Na kama wewe unaulea umasikini kwenu usiilaumu CCM, laumu kichwa chako.
 
Tanzania ya Magu niya viwanda naona mzee sasa hivi anajipgia cm kwenye vipindi vya TV tu kwani hii serikali ya kazi tu inaendeshwa vp? Ogopa sana kua nakiongozi anapenda kila siku atokee kwenye media
 
Hiv tabora ndio manispaa ya kwanza Tanzania duh kweli maisha yanaenda kasi sana katika mikoa inayopenda ccm sijaona kama tabora halafu vijana wa huko wanajifanya wahuni kweli kumbe bado wanadanganyika na T-shirt za njano na kijani
 
Maeneo niliyokutajia ni tofauti na maeneo ambayo ccm imechukua majimbo yote ya mkoa kama dodoma.hakuna mkoa maskini na wenye omba omba kama dodoma ambapo ccm ndo inaongoza majimbo yote.

Wewe umeamua kutukana tuu watu wa Dodoma.
Huko Kilimanjaro kwenu watu wanafanya kazi saa ngapi ilhali wanashinda wanakunywa UKAWA/mbege hadi wake zao wanakimbilia Kenya? Au umekunywa UKAWA?
 
Lipeni tu hakuna namna maana tumechoka, CCM mliipenda wenyewe acha muisome namba.
 
Sasa hivi kuna ujenzi wa barabara kama ifuatavyo;
-Tabora mpaka Nzega
-Tabora mpaka Manyoni
-Tabora mpaka Sikonge

Reli itakarabatiwa na bado inapitia Tanora kwenda Mwanza na Kigoma.
Sasa mtoa mada wahasishe wana Tabora waikatae miradi hiyo ili ipelekwe kwa wahitaji.
 
Lipeni tu hakuna namna maana tumechoka, CCM mliipenda wenyewe acha muisome namba.


kulipa sio tatizo...

hoja: hiyo sheria mpya ilifuata taratibu za vikao na maamuzi ya kisheria?.

hoja: upandaji wa gharama kwa 150% ulizingatia vigezo gani?

hoja: kodi kulipwa kwa uwiano sawa(fixed rate) pasipo kujali ukubwa na matumizi ya ardhi husika, je ulifanyiwa upembuzi yakinifu?
 
Laima watu wanaochagua ccm wapandishiwe garama ili wakati wana hakiki gharama watulie WASOME NAMBA vizuri waka walizoea 500, inafika 5,000 hapo lazima atoe macho asome imuingie.
 
Back
Top Bottom