Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Halmashauri ya Manispaa ya Tabora mjini (inayoongozwa na CCM) imepandisha kodi ya majengo kutoka Sh.10,000/= hadi 25,000/= kwa jengo moja.
Ongezeko hili lina kasoro zifuatazo;
#MOSI
Ongezeko hili limepangwa kienyeji kinyume cha sheria ya Serikali za mitaa No.7 ya mwaka 1982 (The Local Government Act (Urban Authorities,1982. No. 7). Sheria hii inataka upandishwaji wa kodi ya majengo (property tax) ufanywe kwa maazimio ya kikao cha "Full Council" yani watendaji wa Halmashauri, Madiwani wote plus wenyeviti wote wa mitaa na vitongoji.
Lakini kwa Tabora haijafanyika hivyo. Mkurugenzi na watu wake wamejifungia ndani wakajipangia bei walivyotaka. Haya ni matumizi mabaya sana ya madaraka. Wamejiamulia tu kupanga kwa sababu wanajua wananchi hawawezi kukataa. Huu ni ubabe, ni wizi na unyang'anyi.
Cha ajabu eneo hili lina Mbunge na hajatoa kauli yoyote kuhusiana na suala hili. Kukaa kimya kwa Mbunge huyu inamaanisha kuwa anakubaliana na "wizi" huu wa Halmashauri. Kama hakubaliani nao mbona asitoe kauli ya kupinga? Kwanini asiwakosoe halmashauri kwa kufanya maamuzi kienyeji bila kuitisha "full council meeting" kama sheria inavyotaka?
Ukimya wake unamaanisha nini? Kwamba yuko "neutral"?. Albert Einsten aliwahi kusema ukiwa "neutral" mahali ambako mnyonge anaonewa inamaanisha unamuunga mkono yule anayemuonea mwenzie. Mwalimu Nyerere nae akasema ukimuona tembo ameweka mguu wake kwenye mgongo wa chura, halafu ukajifanya upo "neutral" hakika chura hataelewa "neutrality" yako. Je hivi ndivyo Mbunge huyu wa CCM Tabora (Emmanuel Mwakasaka) alivyoamua kuwa neutral wakati wananchi wakionewa?
#PILI
Ongezeko hili ni kubwa sana. Halilipiki. Kupandisha kodi kutoka 10,000/= hadi 25,000/= ni ongezeko la asilimia 150%. Hiki ni kiwango kisichovumilika na ni kumtesa mwananchi maskini aliyehangaika kujenga nyumba yake miaka na miaka.
Yani kiwanja anunue mwenyewe, nyumba ajenge mwenyewe kwa kuhangaika na kukopa halafu halmashauri mje mpandishe kodi kienyeji vile mnavyojisikia? Hivi CCM mkoje? Hamuwezi kuendesha serikali bila kuwadhulumu watanzania? Sisemi watu wasilipe kodi. Nataka walipe, lakini sio kwa kiwango hiki cha kukomoana. Asilimia 150% ongezeko? Hapana, hata ingekuwa mimi silipi.
Kwanini haikupanda kwa asilimia 20% au 50% walau ifike 12,000/= au 15,000/=?? Nani aliyefanya upembuzi yakinifu na kupendekeza ipande kwa 150%?
Hivi serikali haijui kuwa kodi ikiwa kubwa sana inachangia watu wengi kukwepa maana inaumiza? Ni wajibu wa kila mwananchi kulipa kodi lakini inabidi iwe "reasonable". Haiwezekani kodi ipande kwa 150% halafu utegemee watajitokeza wengi kulipa. Wengi watakwepa.
Wakati halmashauri ya jiji la Arusha inayoongozwa na CHADEMA imepandisha "property tax" kwa asilimia 5% wenzao Tabora wamepandishwa kwa asilimia 150%. Yani wananchi wa Tabora wananyonywa mara 30 kuliko wa Arusha (150% ÷ 5%).
Kwa kufanya hivi Halmashauri ya Manispaa Tabora imeweka rekodi ya kuwa Halmashauri ya kwanza nchini kupandisha kodi ya majengo kwa kiwango kikubwa zaidi. Cha ajabu wananchi hawa wananyonywa hivi lakini waliichagua CCM kuanzia madiwani, wabunge hadi Rais. Ndio maana huwa nasemaga ili uwe mfuasi wa CCM unahitaji degree nyingi sana za ujinga. Haiwezekani unyonywe hivi halafu uko busy kusema "CCM hoyee". Lazima utakuwa na shida ya akili.
#TATU,
Kodi hii haiakisi uhalisia. Kiasi cha shilingi 25,000/= kilichopangwa na Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ni kwa majengo yote. Yani mwenye ghorofa atalipa 25,000/=, mwenye vyumba viwili atalipa 25,000/=, na mwenye chumba kimoja atalipa 25,000/=. Hii si haki hata kidogo.
Tozo hii ilipaswa iendane na tathimini ya nyumba husika. Haiwezekani mmiliki wa kiwanda alipe 25,000/= na mkulima maskini wa tumbaku mwenye chumba kimoja nae alipe 25,000/= eti kisa yote ni majengo. Huu ni wizi wa mchana kweupe.
Haiwezekani nyumba ya bati, nyumba ya makuti, nyumba ya nyasi, nyumba ya tofali na nyumba ya matope zote zilipe kiwango sawa cha 25,000/=. Huu ni unyonyaji uliopitiliza.
Lakini je hivi Halmashauri ya manispaa ya Tabora imekosa vyanzo vingine vya mapato hadi kuamua kunyonya wananchi kikatili namna hii?
Naomba kamanda Hawaa Bananga (Mbunge viti maalumu CHADEMA mkoa wa Tabora) uwasaidie hawa ndugu zako kupata haki yao maana mbunge wao waliyemchagua ameshindwa kuwasaidia.
Kodi hii ipunguzwe (iwe reasonable) na pia ifanyike tathmini ambayo itasaidia kila nyumba kulipa kulingana na aina yake ya Ujenzi. Haiwezekani nyumba ya tope na nyumba ya ghorofa zikalipa sawa.
Malisa GJ.!