Tabiri yatakayotokea Mei Mosi 2024 Arusha

Sanyambila

JF-Expert Member
Jan 24, 2018
352
469
Wanajamii habari za majukumu:

Kesho jumatano ya tarehe 01-05-2024 pale Arusha katika viwanja vya sheikh Abeid Amani Karume kutafanyika Sherehe za wafanyakazi Wote wa Umma na binafsi. Sector zote.

Kama ilivyo Ada Mgeni rasmi ni Mwajili mkuu wa SERIKALI Mh. Dr. Samia Suluhu Hasani, Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Vitu vinavyogonga vichwa kwa Sasa kwa wafanyakazi ni Kama ifuatavyo

1. KIKOKOTOO hiki ni habari ya mjini kikokotoo kimeonekana ni ukoloni Mambo Leo kwa wastaafu 33% ya pension ndiyo hupewa mstaafu Sasa kiasi kidogo pia hakitoki kwa wakati , mstaafu anafuatilia mafao Hadi kupata mpaka miaka 3 bado anafuatilia mafao.

Kitakacho jiri kesho ni kuunda kamati ili ku evaluate kikokotoo mwakani ni uchaguzi hii Ni Technical strategy inaweza kufutwa ili watumishi wakipe kura chama Tawala.

2. UPANDISHAJI WA MADARAJA
Hili ni shangwe tu Ila litasemwa kesho ili kuongeza kurasa katika hotuba za Mgeni rasmi

3. AJIRA MPYA
wale watumishi tarajali wategemee kuanzia kesho waanze kuandaa documents zao kesho ajira zinatangazwa na linki zote zinafunguliwa watu waanze kuomba imecheleweshwa ili kuongeza shughuli zilizopangwa Mei mosi Kwa Mgeni rasmi asikose la kusema.

4. NYONGEZA YA MSHAHARA KIMA CHA CHINI
watumishi msitegemee Ila Hadi itahaidiwa kwamba tuna shughulikia Ila mwakani lazima kibunda kiongezeke makofi kwa Mgeni rasmi

5. ANNUAL INCREMENTS
HAPA NYONGEZA IPO ILA ITAKUWA YA CHINI CHINI SIYO MBAYA WALAU YA KUTOSHA KILO MOJA YA NYAMA YA NG'OMBE

Makonda kesho lazima atatoa Boko moja litakuwa habari ya mjini

Natabiri tu ( Kama Nyerere)

Ongeza unabii wako siku ya kesho.

===

Pia soma:

Dkt. Mpango: Serikali imepokea hoja ya kuboresha kikokotoo kwakuwa wafanyakazi hawaridhishwi na kanuni zake
 
Hivi rais wetu tofauti na kushiriki hizi sherehe za serikali, kuzindua vitu na kwenda nje, hua Hana ziara za mkoani?
Mikoani kulivyo kubaya hivyo tutatembelea mwakani Kwa ajili ya kuwashawishi Wanyonge waendelee kutuamini ili tuendelee kutumia vyema Kodi za jasho lao,,Ila kwa sasa acha tuendelee kwenda Falme za kiarabu huko kina Biriani ya ngamia na kizimkazi Kwa ajili ya mafukizo ya marashi yanukiayo vyedii mnoo###MikoaniKubaya###
 
Wanajamii habari za majukumu:

Kesho jumatano ya tarehe 01-05-2024 pale Arusha katika viwanja vya sheikh Abeid Amani Karume kutafanyika Sherehe za wafanyakazi Wote wa Umma na binafsi. Sector zote.

Kama ilivyo Ada Mgeni rasmi ni Mwajili mkuu wa SERIKALI Mh. Dr. Samia Suluhu Hasani, Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Vitu vinavyogonga vichwa kwa Sasa kwa wafanyakazi ni Kama ifuatavyo

1. KIKOKOTOO hiki ni habari ya mjini kikokotoo kimeonekana ni ukoloni Mambo Leo kwa wastaafu 33% ya pension ndiyo hupewa mstaafu Sasa kiasi kidogo pia hakitoki kwa wakati , mstaafu anafuatilia mafao Hadi kupata mpaka miaka 3 bado anafuatilia mafao.

Kitakacho jiri kesho ni kuunda kamati ili ku evaluate kikokotoo mwakani ni uchaguzi hii Ni Technical strategy inaweza kufutwa ili watumishi wakipe kura chama Tawala.

2. UPANDISHAJI WA MADARAJA
Hili ni shangwe tu Ila litasemwa kesho ili kuongeza kurasa katika hotuba za Mgeni rasmi

3. AJIRA MPYA
wale watumishi tarajali wategemee kuanzia kesho waanze kuandaa documents zao kesho ajira zinatangazwa na linki zote zinafunguliwa watu waanze kuomba imecheleweshwa ili kuongeza shughuli zilizopangwa Mei mosi Kwa Mgeni rasmi asikose la kusema.

4. NYONGEZA YA MSHAHARA KIMA CHA CHINI
watumishi msitegemee Ila Hadi itahaidiwa kwamba tuna shughulikia Ila mwakani lazima kibunda kiongezeke makofi kwa Mgeni rasmi

5. ANNUAL INCREMENTS
HAPA NYONGEZA IPO ILA ITAKUWA YA CHINI CHINI SIYO MBAYA WALAU YA KUTOSHA KILO MOJA YA NYAMA YA NG'OMBE

Makonda kesho lazima atatoa Boko moja litakuwa habari ya mjini

Natabiri tu ( Kama Nyerere)

Ongeza unabii wako siku ya kesho
6. MAKONDA
Anaweza kutanguliwa mbele ya halaiki na kubaki analia lia na manabii.
 
Ila Mama anawadekeza sana watumishi, wakilia tu..wanabembelezwa.
Mbona awamu ya tano walikuwa hawadeki kama awamu hii ya sita???!!!
 
6.NATABIRI WATUMISHI WALIOHAMISHWA WASITEGEMEE CHOCHOTE HASA LA KULIPWA STAHIKI ZAO KAMA VILE DISTURBANCE ALLOWANCE, TRANSPORT ALLOWANCE ETC.
 
Makonda amekinukisha mkesha wa Mei mosi ni kunywa nalulewa walinzi I wadudu hakuna kuondoka na chupa NYAMA Kama zote machali kipande hiki ni nomaaa( wadudu voice)
 
Back
Top Bottom