Tabia zinazonikera za baadhi ya madereva wa Dar es Salaam

Kuna tabia zinanikera sana hasa kwa madereva wa DSM...na hapa sizungumzii daladala nazungumzia madereva wa gari zote ndogo kuanzia BABY WALKERS mpaka VX V8......

1.kuwasha HAZARD [double indicator] wanapoenda moja kwa moja[straight] kwenye crossroads
Kwingine kote nimekuelewa ispokuwa hiyo namba 1 tu, mj nimefundishwa driving school, na naona hiyo ipo sahihi, sasa sijui imekuwaje kero kwako.

Sent from my iPhone using JamiiForums app

Ama hukuelewa ulipokuwa unafundishwa au hao walimu hawakukufundisha kwa usahihi. Kuwasha hazard hakumaanishi kwamba "unanyoosha" kwenye njia panda.
 
mkuu, hiyo no 11 naichukia sana--kuna siku 1 kidogo nigongwe wakati navuka barabara.

halafu sipendi kabisa wale makonda wanaowauliza abiria: UNA 100 NIKUPE 200?
 
Ama hukuelewa ulipokuwa unafundishwa au hao walimu hawakukufundisha kwa usahihi. Kuwasha hazard hakumaanishi kwamba "unanyoosha" kwenye njia panda.

Sidhani kama akili yangu inaweza kukosa kuelewa simple theory kama hiyo, pia sijashawishika kama madereva wote wanaofanya hivyo wamefundishwa na mwalimu mmoja. Hebu nipe elimu ya bure, kwenye hiyo case tunaonesha ishara gani kama tunapita moja kwa moja, badala ya kuwasha hiyo hazard.

Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Kuna tabia zinanikera sana hasa kwa madereva wa DSM...na hapa sizungumzii daladala nazungumzia madereva wa gari zote ndogo kuanzia BABY WALKERS mpaka VX V8......

1.kuwasha HAZARD [double indicator] wanapoenda moja kwa moja[straight] kwenye crossroads
Kwingine kote nimekuelewa ispokuwa hiyo namba 1 tu, mj nimefundishwa driving school, na naona hiyo ipo sahihi, sasa sijui imekuwaje kero kwako.

Sent from my iPhone using JamiiForums app

driving school gani??? ukienda moja kwa moja huwashi indicator yoyote.

pata elimu kidogo

http://www.drivingtesttips.biz/when-to-use-hazard-lights.html
 
2. Hata mimi siipendi. Ni ukimbelembele tu.

9. Wenyewe tunaita swaga
 
Umelenga sawasawa ni kweli kabisa!hiyo namba 4 inanikera sana utaona jitu linaziba halafu linakaa hapo hata nusu saa!halafu umesahau hawa wadada wanangangania stealing kama wanakwea mti!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Na shingo zao huchomoza kama wanajitayarisha kuchinjwa.
 
sasa ukute wale vijana wenye viduku, suruali zinabana na ALTEZZA yao, nakushauri uwe mpole maanake wa nguvu sana za ziada!!!

Hao ndio sitaki hata kuzungumza nao nishatibuana na mmoja wakati wa kutoa maelezo kanataja umri yaani 1 year older than the last born from my mom's womb!!!!!

Nikamwambia askari basi mkuu nasamehe bure!!!!!
Maana baada ya pale obvious angepiga simu aje mama, baba, kaka au yeyote mkubwa then nikajua ni kumuwahi girlfriend ndio kumemponza!!!!!
 
Hahhah hiyo hata mimi ninafanya sana..pole kwa kukukwaza

duh mkuu,ni furaha yangu kama nimeweza hata kumrekebisha mtu mmoja..... OLESAIDIMU MANI mnamsikia huyu....ndio wale anaendesha taratibu ukitaka kumpita anaongeza mwendo!!
 
Last edited by a moderator:
Hao ndio sitaki hata kuzungumza nao nishatibuana na mmoja wakati wa kutoa maelezo kanataja umri yaani 1 year older than the last born from my mom's womb!!!!!

Nikamwambia askari basi mkuu nasamehe bure!!!!!
Maana baada ya pale obvious angepiga simu aje mama, baba, kaka au yeyote mkubwa then nikajua ni kumuwahi girlfriend ndio kumemponza!!!!!

mimi nawaogopa sana hao, nawapisha tu.
 
duh mkuu,ni furaha yangu kama nimeweza hata kumrekebisha mtu mmoja..... OLESAIDIMU MANI mnamsikia huyu....ndio wale anaendesha taratibu ukitaka kumpita anaongeza mwendo!!

Unadhani ni huyu tu???!!! Sema huyu kawa mkweli wengi wamekula dozi kimyakimya!!!
 
Last edited by a moderator:
duh mkuu,ni furaha yangu kama nimeweza hata kumrekebisha mtu mmoja..... OLESAIDIMU MANI mnamsikia huyu....ndio wale anaendesha taratibu ukitaka kumpita anaongeza mwendo!!

Mkuu kuna tabia nyengine siipendi inafanywa sana na madereva wa tax. Unakuta dereva anaendesha kwa kutumia mkono mmoja wa kushoto na ule wa kulia ameuning'iniza kwa nje unakaribia kugusa chini. Sijui wanapata raha gani halafu jitu lenyewe unalikuta ni kubwa jibongeee
 
Sasa umkute anapiga stori na abiria we kichwa kitakuuma kila ukijaribu kutafsiri ishara za mkono hupati maana kumbe anamuelekeza huyo abiria sehemu; ile utakuta ghorofa hivi, kono kalinyanyua baada ya ghorofa unakata kushoto basi kono analipeleka mbele juu ya side mirror na kuukunja kushoto basi hapo umefika anarudisha chini kama anakuambia slow down vile wee tena brekiii..jamaa wa nyuma naye honi sababu haoni sababu ya wewe ku slow down basi hiyo waweza kuta kakuumiza kichwa Vingunguti mpaka Tazara ndio unagundua kumbe wanatia stori zao!!!!
 
aisee mnanivunja mbavu hapa...madereva tuna vituko!!! mara katupa chupa tupu ya maji ya 'UHAI'...gunzi la hindi la kuchemsha na linakosakosa kioo cha gari yako!!!
 
Wiki iliyopita jamaa alikuwa mbele yangu anafanya hivyo vituko huku anavuta sigara mkono kautoa kwa nje. Wakati niko nyuma yake akakirusha kipisi cha sigara kikaruka na kudondokea kwenye kioo changu huku kinafuka moshi. Nikakipiga na wepa kikaanguka.
 
Back
Top Bottom