Habari Wadau,
Ni Imani yangu kwamba mnaendelea vema na pilika za siku kwa siku, Imedhihirika kwamba wanaume ndio huwa tunahangaika kubeba mizigo ya wenza wetu ikiwemo stress ambazo hupelekea kujipata na maradhi kama Kisukari na Presha,
Mimi ni mtanzania kiasili na ninaishi mikoa ya kanda ya ziwa, nina mke ambaye tumeishi pamoja kwa miaka ipatayo 23, tunao watoto wanne, tulivyoanza maisha huyu mwanamke alikuwa ni mwenye kutoa taarifa na kuomba ruhusa kwa mambo mengi aliyotaka kufanya ambayo yalihitaji Attention yangu, But kwa miaka ya hivi karibuni nimeanza kuona akibadili taratibu na tabia na kuanza kujifanyia mambo yake kwa namna anavyoona inafaa kwake, (Inawezekana ndio Uhuru wanaoudai wanawake), Nami ni mmoja ya watanzania waliokuwa effected na mfumo wa uendeshaji sera wa nchi hii kwa maana ya kuathirika kiuchumi, Kutokana na situation hiyo huyu mke wangu amefikia hatua anapopewa Kadi za kuchangia Harusi anachangia kama single huku akijua yeye ni mke wa mtu, ameshafanya hivyo zaidi ya mara tatu hivi, siku za nyuma wakati uchumi wangu uko vizuri mimi sikuwahi hata siku moja kuchangia kadi ya harusi single, kadi zote ambazo nimewahi kuletewa nimekuwa nichangia double kumaanisha Mr & Mrs.wa bahati mbaya sana kila anapopewa kadi huwa hasemi, anakaa kimya akpata pesa kwenye shughuli yake anaamua kuchangia kiasi kidogo ambacho huwa ni single, kifupi ni kwamba sio kwamba anakuwa hana pesa ya kuchangia double ila anaona kama anapoteza pesa yake kuchangia double, Kwangu mimi naona kama hili ni tatizo la maadili, Naomba kujua kutoka kwenu wadau, Je huyu anakuwa na sifa za kuendelea kuitwa mke wa mtu ?, na kama SIO, nini cha kufanya.