Tabia za wanawake

Tabia za wanawake

Coaster2015

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2018
Posts
2,609
Reaction score
2,738
Habari Wadau,
Ni Imani yangu kwamba mnaendelea vema na pilika za siku kwa siku, Imedhihirika kwamba wanaume ndio huwa tunahangaika kubeba mizigo ya wenza wetu ikiwemo stress ambazo hupelekea kujipata na maradhi kama Kisukari na Presha,
Mimi ni mtanzania kiasili na ninaishi mikoa ya kanda ya ziwa, nina mke ambaye tumeishi pamoja kwa miaka ipatayo 23, tunao watoto wanne, tulivyoanza maisha huyu mwanamke alikuwa ni mwenye kutoa taarifa na kuomba ruhusa kwa mambo mengi aliyotaka kufanya ambayo yalihitaji Attention yangu, But kwa miaka ya hivi karibuni nimeanza kuona akibadili taratibu na tabia na kuanza kujifanyia mambo yake kwa namna anavyoona inafaa kwake, (Inawezekana ndio Uhuru wanaoudai wanawake), Nami ni mmoja ya watanzania waliokuwa effected na mfumo wa uendeshaji sera wa nchi hii kwa maana ya kuathirika kiuchumi, Kutokana na situation hiyo huyu mke wangu amefikia hatua anapopewa Kadi za kuchangia Harusi anachangia kama single huku akijua yeye ni mke wa mtu, ameshafanya hivyo zaidi ya mara tatu hivi, siku za nyuma wakati uchumi wangu uko vizuri mimi sikuwahi hata siku moja kuchangia kadi ya harusi single, kadi zote ambazo nimewahi kuletewa nimekuwa nichangia double kumaanisha Mr & Mrs.wa bahati mbaya sana kila anapopewa kadi huwa hasemi, anakaa kimya akpata pesa kwenye shughuli yake anaamua kuchangia kiasi kidogo ambacho huwa ni single, kifupi ni kwamba sio kwamba anakuwa hana pesa ya kuchangia double ila anaona kama anapoteza pesa yake kuchangia double, Kwangu mimi naona kama hili ni tatizo la maadili, Naomba kujua kutoka kwenu wadau, Je huyu anakuwa na sifa za kuendelea kuitwa mke wa mtu ?, na kama SIO, nini cha kufanya.
 
Hawa jamaa zetu wana mambo mengi sana...dah! Ongea nae tu huenda ukapata kujua mengi zaidi ya hilo
 
Affected and effected are two words that
are commonly confused in writing, while
their meanings are related they are very
different. We want to make sure we're
always communicating effectively so
keeping these two words straightforward
is important.
Effected means to actually do something,
to execute, produce or bring about
something. It's an action word of actually
doing something, i.e. "He effected a
reorganization of the finance
department."
Affected is used to describe something
being impacted. This is a word you
would commonly use when something
has been impacted,
 
Weka misingi ya familia yako na umshirikishe. Msingi mmojawapo ni utaratibu wa muda wa kufika nyumbani. Mpangie asifike nyumbani zaidi ya saa moja na nusu usiku; vinginevyo ni lazima uwe naye ndo muingie muda umeenda.
Kwa kufanya hivyo utakuwa umedhibiti tatizo hilo. Kwa ufupi huko kwenye hizo sherehe za kipekee tena usiku kwa vyovyote vile kuna mtu anakusaidia shughuli.
 
Kama mlianza maisha miaka 23 iliyopita, bila shaka amekuconsult vya kutosha kiasi na yeye sasa anaweza kufanya maamuzi bila kushauriwa.

Katika umri huu sitegemei mwanaume kunishauri kila jambo kama nilivyokuwa kwenye 20s, 30s na early 40s.
Kama nitakuwa sijajifunza miaka yote hiyo hata huyp mume inabidi anishangae. Unless nahitaji ushauri mpya, yes nitataka ushauri.
 
itakua kuna kibe10 kinamsaidia haha
 
Hayo ya kiben10 ni dhana ya mtu asiejiamini au asieaminika au control freak!

Miaka 23 ya ndoa bado unataka mtu akuombe ushauri au ruhusa? Sana sana ni kutoa taarifa kukujuza yafuatayo au yatokanayo.
mazoea ndo apo yana tabu kama walizoeshana hivyo alafu ghafla yatokee mabadiliko ndo hapo itamchukua muda kuyakabiri
 
Miaka 23 ya ndoa ya ndoa na bado wajiuliza kama bado anafaa kua Mke? Na kama utapewa jibu hafai utamuacha kisa kufanya vitu vyake mwenyewe...hauko serious mkuu

Vitu vidogovidogo visikufanye upoteze imani kwa mkeo..unaona anachofanya hakikufurahishi ongea nae..huenda kuna kipindi ulianza hako katabia na yeye sasa anaamua kulipiza
 
Sio lengo langu kusema eti nimuache hapana, nimeweka hapa ili kujua yawezekana kuna mtu mwingine amewahi kufanyiwa haya anaweza kuniambia alirekebishaje, Itoshe tu kusema unaweza ukaona kwamba ni vitu vidogo vidogo lakini kwangu nahisi ni tatizo la kimaadili, binafsi sipendi mtu anaefanya mambo bila utaratibu, hili linaweza kuwa tatizo langu peke yangu
 
Kama mlianza maisha miaka 23 iliyopita, bila shaka amekuconsult vya kutosha kiasi na yeye sasa anaweza kufanya maamuzi bila kushauriwa.

Katika umri huu sitegemei mwanaume kunishauri kila jambo kama nilivyokuwa kwenye 20s, 30s na early 40s.
Kama nitakuwa sijajifunza miaka yote hiyo hata huyp mume inabidi anishangae. Unless nahitaji ushauri mpya, yes nitataka ushauri.
Kujifunza hakuishi, kushauriana hakuishi na kama nyie ni mwili mmoja lazima mshauriane kwa kila jambo, ila suala la maamuzi baada ushauri ni jambo lingine na tena ndilo zito na muhimu kuzingatia, maamuzi yenye faida lazima yawe "RATIONAL" (minimum risk) ,vinginevyo itakuwa ni jeuri tu (hii ni kwa wote, mwanaume/mwanamke).
 
Sio lengo langu kusema eti nimuache hapana, nimeweka hapa ili kujua yawezekana kuna mtu mwingine amewahi kufanyiwa haya anaweza kuniambia alirekebishaje, Itoshe tu kusema unaweza ukaona kwamba ni vitu vidogo vidogo lakini kwangu nahisi ni tatizo la kimaadili, binafsi sipendi mtu anaefanya mambo bila utaratibu, hili linaweza kuwa tatizo langu peke yangu
Ongea na mwenzio
 
Kujifunza hakuishi, kushauriana hakuishi na kama nyie ni mwili mmoja lazima mshauriane kwa kila jambo, ila suala la maamuzi baada ushauri ni jambo lingine na tena ndilo zito na muhimu kuzingatia, maamuzi yenye faida lazima yawe "RATIONAL" (minimum risk) ,vinginevyo itakuwa ni jeuri tu (hii ni kwa wote, mwanaume/mwanamke).
Johng, maelezo yako mazuri lakini yamevaa Koti, jaribu kudadavua ulicholenga kuongea ili tuelewane vizuri
 
Back
Top Bottom