Unamwambia nini mpenzi wako kuhusu marafiki zako wa damu, wale marafiki zako damu damu, wapuuzi wenzio ambao mnaitana kila aina ya majina, makamanda, masela, washikaji, namaanisha wale watu wako wa karibu, nasema kuhusu wale mashemeji wake wa karibu, wale shoga zako mashost zako etc, unawaelezeaje mbele ya mpenzi wako,mmeo/mkeo mtarajiwa?
Unawazungumiaje mbele yake?
Kuwa makini sana, " Utakachokizungumza kuhusu wao kitaeleweka ni chenu wote" kama utawazungumizia kwa wema, tabia nzuri na ukarimu wao basi utaeleweka na wewe ndivyo ulivyo ! Kama utamwambia mkeo, Tazama Shaban ni mzinzi sana, yule Saulo ni mkali sana, hiki ndicho kitaeleweka mbele ya mwenza wako kuhusu upande wako. ' Ardhi Ujitazame'
Unamchamba shosti yako mbele ya mmeo, wakati wewe ndiyo ulisema huyu ni shoga yangu toka tunakua, unanena mabaya na tabia chafu zoote za rafiki yako Mwajuma mbele ya mmeo, ukumbuke tu anaelewa hizi ndizo tabia zenu nyote ' watch it '
NB: Tabia zote mbaya utakazozieleza ni zenu wote ,wewe na rafiki zako ila zile nzuri zitamuhusu rafiki yako tu[emoji28]
Nikutakieni Wiki njema.