Tabia za Facebook jamvini zinanikera

naona kuna wageni wameingia jamvini hawajielewi. Kwanza wanaandika vifupi mpaka basi kama ni kiingereza andika YOU sio U na kama ni kiswahili andika kiswahili fasaha hatutaki kifupi wala mkorogo Mfano SASA anaandika XAXA mbadilike bhana.
shekhe hata wewe umeshakua mkongwe! na umeshangia kwenye harakati za JF-anti wageni!
umetisha baba!
 
Tatizo watu hamtaki kuendana na mazingira kama umekuta watu wanaandika kiingereza na kiswahili fasaha iga usijeukajulikana weWe ni mzamiaji
 
Hapa Mahali ni pazuriiiii ndugu wanapo kaaa, wakipatana vyema na wakipendana:

Senior Member
Join Date : 5th December 2011
Kumbe Hata ukikaa mwezi mmoja hapa unakuwa "Senior Member" na unaweza kuwalalamikia wageni...
 
Tatizo watu hamtaki kuendana na mazingira kama umekuta watu wanaandika kiingereza na kiswahili fasaha iga usijeukajulikana weWe ni mzamiaji

Kabla ya kusema yote haya hakikisha mikono yako ni misafi pia.
Whoever comes to equity must come with clean hands.
Sio kiingereza, ni Kiingereza
Sio kiswahili, ni Kiswahili
Sio weWe, ni wewe
sio usijeukajulikana, ni usije ukajulikana.
Pia uwe unaweka nukta na alama za mkato kwenye sentensi zako.
Kama kweli unachukizwa na hao wasioandika lugha fasaha, basi anza kujichukia mwenyewe.
 
naona kuna wageni wameingia jamvini hawajielewi. Kwanza wanaandika vifupi mpaka basi kama ni kiingereza andika YOU sio U na kama ni kiswahili andika kiswahili fasaha hatutaki kifupi wala mkorogo Mfano SASA anaandika XAXA mbadilike bhana.

Dah! Hebu rudia lugha uliyotumia. Ni Kiswahili fasaha kweli?
Unaanza sentensi kwa herufi ndogo
Badala ya kuandika Kiingereza, umeandika kiingereza
Badala ya kuandika Kiswahili, umeandika kiswahili.
Huweki nukta mwisho wa sentensi.
"mbadilike bhana" ndio lugha fasaha? "bhana" maana ya nini?
 
Huku nako ulikuwa unatumia lugha fasaha?

andika kiingereza fasaha hatutaki tabia za facebook hapa sawa

wewe unaangaika account tatu za nin wakufungie kabisa

yule nliyekua nataka kununua id yake kafika. Jaman weye bibie mzima niambie bas niku Pm

kama hautak nikujue si bas kwan ni lazima nikujue sikubembelez una jina zur lakin halishabihiani na unayofanya.

amna amesema yeye ndo anapatikana kwenye hzo ofis

mmh! Sina maana hiyo shukran kwa ilo vip mawasiliano?

kwel wew unatumia matope unareply kwa quote kwa kukopi sired yote!
 
uchunguzi na uzoefu wangu, hizo lugha mara nyingi hutumiwa na wanafunzi either wa sekondari ama waliongia vyuoni karibuni.

so mimi kusema ukweli nikiona mtu kaandika hivyo namuweka kwenye group ya under 24, tena hapo kwa kumpendelea, akiendelea namuweka kwenye group ya under 21 au U19. maana huko ndiko kwenye tabia hizo..... wao wanajiona wajuaji...kumbe tulitumia tabia hizo enzi zile za sms kwenye simu inagharimu usd 0.12 (enzi za kutumia dola) yaani tshs 201 ya leo. tulifanya hivyo kuogopa makato makubwa ya fedha. lakini sasa hawa wadogo zangu sijui wanaogopa akiandika neno full bundle litaisha???

kama unamfahamu mwambie abadilike!!
 
Hapa Mahali ni pazuriiiii ndugu wanapo kaaa, wakipatana vyema na wakipendana:

Senior Member
Join Date : 5th December 2011
Kumbe Hata ukikaa mwezi mmoja hapa unakuwa "Senior Member" na unaweza kuwalalamikia wageni...

ndiyo ujue mambo ya multiple IDs
 
nashukuru naendelea vizuri tangu nipone ugonjwa wa facebook. nilisema sirudi tena kule na wandugu wa kule wakafikiri natania!
 
Back
Top Bottom