Mr. Mangi
JF-Expert Member
- Sep 21, 2014
- 1,512
- 771
Hii tabia ya watu kupewa haya majina imekuwa ikibeba historia zao ila mi yamekuwa yakinishangaza na kunifurahisha pia mfano hapa kwetu kuna jamaa anaitwa "machapati" huyu jamaa asubuhi tu anauwezo wa kula chapati kama kumi+ na maharage ya kutosha. Kuna mwingine anaitwa "uji" huyu alikuwa na tabia ya kunyang'anya uji watoto waliokuwa wakitumwa kupeleka hospitali. Kuna kiongoz wa dini kapewa jina ya "majogoo" huyu ana tabia ya kupenda kupewa zawad ya jogoo pind anapotembelea familia flan. Mwingine anaitwa "Ali maukoko" huyu ktk sherehe anahakikisha kala wali wa kutosha na kusubiria sufuria kuoshwa ale ukoko. Vp wewe umesikia yap na historia zake