Tour De France
JF-Expert Member
- Jun 12, 2014
- 345
- 336
maana yake ni kwamba humjui kwa tabia na mienendo yake. Yawezekana yeye kwa asili yake si mtu anayejali mda (wapo watu wa hvyo), lakin pia kwa kuwa hakuwah kukuona pia na hana mazoea na wewe hajawa na ile concentration kwako kama shemej yake. Kikubwa tunza hizo sms kama ushahidi siku ya kesi. Lakini pia jiandae kwa maelezo mazuri kuhusu kujibizana huko maana yeye kuchelewa kufika yawezekana siku ya kesi akatoa sababu nzuri kabisa ya kwa nin alichelewa ambayo wewe hukuweza kuvumilia na kumsubiri ili akwambie kwa nin alichelewa ila mkaishia kujibizana hovyo.
Mwisho wa siku jiandae kuomba msamaha, huyo ni shemeji yako na yawezekana kakukosea na ulikuwa na sababu ya kureact lakin kama huyo jamaa yako ni mtu ambae unataraji kuoana nae ni vema ukaomba msamaha kwa shemeji yako usianze kutengeneza maadui mapema ktk familia ambako unataraji kwenda huwezijua huyo shem ana ushawish gani kwa wanafamilia wengne.
Namaanisha hata ukionekana we ndo unadeserve kushnda hiyo kesi, usijejigamba na kutembea kifua mbele kwa kumwonyesha shem wako kuwa ni looser! Endelea kuwa nae tu positively kama shemej yako
Akiwa na akili atafuata huu ushauri lkn akiwa ndo walewale basi ataendelea kuntangaza shemej yake kuwa dk mbili mbele sijui haziivi na kaka yake sjjui nini!... hujaolewa tayari ushaanza kuchagua marafiki wa ndugu wa mume? Unajua kwa nn mchumbaako anaishi na mdogo wake mpaka sasa? Unajua ni kiasi gani anampenda mdogo wake? Na akiendelea hivi itafika muda jamaa itabidi achague mchumba au mdogo wake na si wote wanaoegemea upande wa mchumba wengine huwaambii kitu kwa ndugu zao! Atachagua upande wa ndugu yake na hapo atapokuja tena kuntangaza!.. ndoa wanazitaka lkn kuvumilia na kujipa muda wa kuwasoma ndugu hamuwezi!