Tabia ya Mume inanitesa

Tabia ya Mume inanitesa

devj

Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
8
Reaction score
1
habari zenu wapendwa!
jamani mie nimeletewa hili jambo na mdogo angu wa damu kabisa akiniomba ushauri na kwa kweli nimeona nije kwenu mnisaidie tumshauri cha kufanya kutokana na yeye kukata tamaa na kufikiria kuondoka kwenye ndoa yake.

Ameolewa miaka 3 iliyopita na ana mtoto mmoja.
Kwa muda mrefu tabia za mume wake zimekuwa zinamkosesha raha sana na kumfanya ajute kuolewa ingawa Ndoa ni baraka kutoka kwa Mungu.kwanza anasema kuna mengi sana anayofanyiwa na mume lakini hili kalinyooshea mikono,Mwanaume anaweza kununa hata wiki nzima bila kuongea ndani,akitoka kazini mwanamke atapika,atamuandalia maji ya kuoga,atakula na ataangalia TV huku kanuna ,akienda kitandani basi ndio kulala pembeni kabisa ya kitanda,ikitokea ukamgusa hata kwa bahati mbaya ntakavyosukumwa daah..

Alishajaribu sana kumuuliza mwenzie kama kuna tatizo na husema hakuna,akamwambia basi kama hakuna tatizo kwa nini awe hivyo mpaka mwanamke anakosa raha na amani moyoni?alimweleza kuwa tabia hiyo huwa inamkwaza na kujiona labda mwenzie hampendi tena na anamuona kero pale nyumbani,hapo Mwanaume anabadilika kwa muda na kuwa wa kawaida na baada ya muda mfupi hali ni ileile inajirudi.

Ukienda hata upande wa kufanya tendo la ndoa ni mpaka mwanaume aamue yeye,ameshamchunguza sana kama ana mwanamke mwingine lakini kwa asilimia 100 hana mtu.

kwanza anasema hakumbuki mara ya mwisho mwanaume amemkiss ni lini,amekuwa anamiss vitu vingi sana kutoka kwa mumewe lakini asilimia kubwa ya mume ni mkali na busy,anatamani hata wale sahani moja huku wanaongea lakini hataki.

Ikitokea mtoto akalia hata kidogo mume anamfokea mwanamke hata mbele za wageni..na pia hajali ni wakwe wala shemeji.

Na anachoshangaa nyumba anahudumia vizuri kwa chakula ingawa kikiisha mama huwa ana kazi ya ziada kujieleza katumiajetumiaje mafuta yakaisha na hii kumpelekea hata vikiisha kutoomba tena kwa hofu.

Ameshamsihi sana kuhusu hiyo tabia lakini mabadiliko yameshindikana ,kamwambia kama kamkosea ni bora akamwambia kwani yeye si malaika,lakini anasema hapana,amejaribu kutafuta detail za kazini kwake kama kuna tatizo lakini hakuna lolote na mara nyingi kununa huku hukufanyia nyumbani tuu.Nyumbani kwao na mume haoni wa kumuomba ushauri kwani wako familia ya Mama yake,dada yake na yeye wa mwisho kuzaliwa,Wote hao mara nyingi wana matendo ya kuwasiliana na mumewe kwa chinichini wakieleza shida zao na hawataki yeye ajue iwapo anawatumia fedha,huku hilo nalo linamsononesha kwa kuona mama mkwe labda anamuhisi yeye kuwa anaweza kumkataza mtoto ake asimsaidie,anatamani mama mkwe angekuwa huru kwake basi angeomba ushauri.

Kwakweli mie mwenyewe aliponisimulia mwili umesisimka na kuogopa nimtie moyo kwa neno lipi,Samahani kwa maneno mengi na kama ntakuwa nimechanganya maelezo mnisamehe...Karibuni tusaidiane kuokoa taasisi yetu ya ndoa.

Mbarikiwe sana kwa Michango mtakayotoa.
 
Labda mdogo wako ajaribu kumuweka chini shemeji yake (Rafiki wa karibu sanaaa wa mumewe). Amueleze na kumuomba ushauri. Pia anaweza jaribu kumuuliza kama kuna kitu mumewe kamuambia huyo rafiki kuhusu ndoa yake then atapata dokezo kuhusu pa kuanzia....Only the friend who knows the husband deeply can give you the quickest soln.

Maybe mumewe kajua kitu alichofanya mkewe in the past na heshima ya mkewe kwake imeshuka...Labda mumewe alikuwa anampenda sana huyo mkewe na kagundua kitu ambacho ni deep sanaaaa kiasi kwamba anajua ile quality ya mahusiano imecompromisiwa, na yule mke aliyemwona malaika si 'malaika tena'. Kiukweli ni issue ambayo inaweza kuhitaji a significant psychotherapy....
 
Huyo Mwanaume hana mwelekeo wa kubadilika, ajaribu kumpeleka kwa viongozi wa dini, ikishindikana, hata kuachika nalo ni jibu.
 
Mmmmh..pole sana,najua ni wewe mwenyewe....kwanza hiyo tabia ya huyo mwanamume siyo nzuri kabisa,wanaume hatununi.....mwiko kabisa,tunakasirika,yakiisha yamekwisha!!!ila kuna suala moja,kuna uwezekano huyo mwanaume ni mkimya sana,hivyo mwanamke anavyofanya vikosa vidogo vidogo,yule mwenzake anakereka,ila kwa kuwa ni mkimya,hawezi kuyaongea!!!viki'accumulate sana,kuna mfanya asongeke moyoni,na anaamua kususa.Jambo la kwanza,ajaribu KUPUNGUZA kufanya vikosa vidogo vidogo mpaka bwana arudi sawa,then apenyeze huko kukwazika kwake.....NDOA BANA.....WACHA MCHEZO NAYO!!!ILIMSHINDAGA MZEE MADIBA........CHEZEA NDOA WEYE!!:mvutaji:
 
Mwanamume hanuni kwa mkewe aisee, au hawa ndo wale vijana wakiume wanaojisifia uzuri wa sura? Ila kwa ushauri, ashirikishe wazee wa kiroho, inawezekana huyo kijana ana pepo au jini mahaba
 
story kama hii ilishakuja humu jamvini; ningekuwa kama EMT ningeweza kuifukunyua na kuweka link.
 
Last edited by a moderator:
Tabia ya mwanume kununa from know where naichukia sana ,akinuna na mimi nanuna mpaka atakapoamua kuacha na lazima aseme kilichomnunisha ,hapo kuna tatizo kuna kitu ila nduguyo hajakuambia vizuri
 
story kama hii ilishakuja humu jamvini; ningekuwa kama EMT ningeweza kuifukunyua na kuweka link.

mi kwakweli natamani sana kujua kuweka link!
kuna vitu huwa natamani sana kufanya ulinkisho lakini nashindwa !
na si wanijua nilivo na makumbukumbu!
we acha tu!
itabidi EMT atupe twisheni!
lakini hata mwaJ anajua ujue!tumwambie atufundishage!
 
Last edited by a moderator:
Huyo mwanaume ni made from iringa? mana watu wa huko ndo wana tabia ya kuacumulate vitu moyoni mwisho wananuna nuna mwanzo mwisho
 
hapo ndo umuhimu wa mwanamke kuwa na kipato unapoonekana...angeziba gap bila kumuomba....

pia si kaamua kujinunia mwenyewe?
Saa nyingine dawa ya moto ni moto.....

Akinuna wewe jipare vizuri fanya yako.....
Weekend jitokee zako nenda hata coco upunge hewa kuepukana na ghubu la mume......
Kitandani usimguse na siku akitaka unyumba wewe ndo uwe umechoka.......

Baadhi ya mijanaume ikijua wake zao wanawapenda hugeuka vigego...

Anyway je kabla hawajaoana mwanaume hakuwa na tabia hizo? Ina maana ndugu yako hakuziona?

Kuhusu kuwapa hela kwao sometimes wanawake msimind mambo madogo madogo si anasaidia kwao mradi hajaneglet majukumu yake tatizo liko wapi? Hata akimnunulia baba yake chupi mke unataka kujua?
 
Tabia ya mwanume kununa from know where naichukia sana ,akinuna na mimi nanuna mpaka atakapoamua kuacha na lazima aseme kilichomnunisha ,hapo kuna tatizo kuna kitu ila nduguyo hajakuambia vizuri

Kama ni mabigwa wa kununa pasipo kusema sababu dada yangu ni wanawake, ndio maana hata ukisoma coments za wengi utasikia wanasema mwanaume hanuni kwa mkewe na lina ukweli mwingi.

Kweli huyo atakuwa na tatazo zaidi, ama wana migogoro ya muda mrefu baina yao hadi jamaa amekata tamaa na ndoa yake.

Na kwa kuzingatia kuwa haya ni maelezo ya upande mmoja, kila mwamba ngozi huvutia kwake so judgement kwa hapa sio rahisi sana maana mleata thread yeye kulingana na andiko lake anaonekana she is innocent 100% kitu ambacho sio rahisi sana kama anavyotaka kuliaminisha jukwaa.

Anyway wenye experience watamsadia hasa wamama walio kwenye ndoa kama walishakutana na mambo kama hayo and what was the solution/s.

Lakini mimi experience yangu huwa naona wamama wananuna with no reason behind na inaweza kuwa hata siku tatu mfululizo, ila kama the opposite napo huwa inatokea nadhani through hii thread tutapata shuhuda and if possible na solution pia.
 
Pole sana kwa yaliyomsibu mdogo wako, me simshauri kabisaa aache ndoa yake bila kujua sababu inayomfanya mumewe awe vile.
Chamsingi awaite viongozi wa dini awaeleze iloswala mbele ya mumewe ninauhakika kama mke ndiye anayemkwaza ni lazima atasema na mambo yatakaa sawa.

Ndoa si lelemama mjue, ukiwa kwenye ndoa kuwa tayari kukabiliana na lolote otherwise usiingie kabisa!
 
Mie naona kama ni gubu la mume hilo. Yaani acheke njia nzima akifika mlango wa nyumbani ananuna!

Labda tuulize kama hiyo tabia ni mpya au alikuwa nayo siku zote?
 
Pole sana dada yangu.
Ninaungana na mchangaaji mmoja hapo juu,kunauwezekano mkubwa sana kua huyo jamaa kunakitu amekijua ambacho kilifanywa na huyo mke wake siku za nyuma na alikua hakijui na baada ya kukijua kimeondoa thamani yote chamsingi tafuta mtu wa karibu yake then ujaribu kufanya uchunguzi ikiwezekana tumia indirect ways.kama nikweri anza kuonyesha kua kwasasa hauko hivyo tena.
 
hapo ndo umuhimu wa mwanamke kuwa na kipato unapoonekana...angeziba gap bila kumuomba....

pia si kaamua kujinunia mwenyewe?
Saa nyingine dawa ya moto ni moto.....

Akinuna wewe jipare vizuri fanya yako.....
Weekend jitokee zako nenda hata coco upunge hewa kuepukana na ghubu la mume......
Kitandani usimguse na siku akitaka unyumba wewe ndo uwe umechoka.......

Baadhi ya mijanaume ikijua wake zao wanawapenda hugeuka vigego...

Anyway je kabla hawajaoana mwanaume hakuwa na tabia hizo? Ina maana ndugu yako hakuziona?

Kuhusu kuwapa hela kwao sometimes wanawake msimind mambo madogo madogo si anasaidia kwao mradi hajaneglet majukumu yake tatizo liko wapi? Hata akimnunulia baba yake chupi mke unataka kujua?

Madamu hiyo inaitwa ndoa, na ameomba ushauri ili ndoa yao isimame hapo kwenye red maneno yake hayajengi, japo najua tuko huru kuongea yalio miyoni mwetu.

Ila hayo yaliyo kwenye Green kulingana na shida ya mhusika sio mbaya, ni maneno yanayojenga na kuimalisha.
 
Kama anajua kimombo mwambie asome kitabu kinaitwa 'Think Like a Man and act Like a LADY'K imeandikwa na Steve, kitamsaidia saaanaaaaaaaaaaaaa
 
habari zenu wapendwa!
jamani mie nimeletewa hili jambo na mdogo angu wa damu kabisa akiniomba ushauri na kwa kweli nimeona nije kwenu mnisaidie tumshauri cha kufanya kutokana na yeye kukata tamaa na kufikiria kuondoka kwenye ndoa yake.

Ameolewa miaka 3 iliyopita na ana mtoto mmoja.
Kwa muda mrefu tabia za mume wake zimekuwa zinamkosesha raha sana na kumfanya ajute kuolewa ingawa Ndoa ni baraka kutoka kwa Mungu.kwanza anasema kuna mengi sana anayofanyiwa na mume lakini hili kalinyooshea mikono,Mwanaume anaweza kununa hata wiki nzima bila kuongea ndani,akitoka kazini mwanamke atapika,atamuandalia maji ya kuoga,atakula na ataangalia TV huku kanuna ,akienda kitandani basi ndio kulala pembeni kabisa ya kitanda,ikitokea ukamgusa hata kwa bahati mbaya ntakavyosukumwa daah..

Alishajaribu sana kumuuliza mwenzie kama kuna tatizo na husema hakuna,akamwambia basi kama hakuna tatizo kwa nini awe hivyo mpaka mwanamke anakosa raha na amani moyoni?alimweleza kuwa tabia hiyo huwa inamkwaza na kujiona labda mwenzie hampendi tena na anamuona kero pale nyumbani,hapo Mwanaume anabadilika kwa muda na kuwa wa kawaida na baada ya muda mfupi hali ni ileile inajirudi.

Ukienda hata upande wa kufanya tendo la ndoa ni mpaka mwanaume aamue yeye,ameshamchunguza sana kama ana mwanamke mwingine lakini kwa asilimia 100 hana mtu.

kwanza anasema hakumbuki mara ya mwisho mwanaume amemkiss ni lini,amekuwa anamiss vitu vingi sana kutoka kwa mumewe lakini asilimia kubwa ya mume ni mkali na busy,anatamani hata wale sahani moja huku wanaongea lakini hataki.

Ikitokea mtoto akalia hata kidogo mume anamfokea mwanamke hata mbele za wageni..na pia hajali ni wakwe wala shemeji.

Na anachoshangaa nyumba anahudumia vizuri kwa chakula ingawa kikiisha mama huwa ana kazi ya ziada kujieleza katumiajetumiaje mafuta yakaisha na hii kumpelekea hata vikiisha kutoomba tena kwa hofu.

Ameshamsihi sana kuhusu hiyo tabia lakini mabadiliko yameshindikana ,kamwambia kama kamkosea ni bora akamwambia kwani yeye si malaika,lakini anasema hapana,amejaribu kutafuta detail za kazini kwake kama kuna tatizo lakini hakuna lolote na mara nyingi kununa huku hukufanyia nyumbani tuu.Nyumbani kwao na mume haoni wa kumuomba ushauri kwani wako familia ya Mama yake,dada yake na yeye wa mwisho kuzaliwa,Wote hao mara nyingi wana matendo ya kuwasiliana na mumewe kwa chinichini wakieleza shida zao na hawataki yeye ajue iwapo anawatumia fedha,huku hilo nalo linamsononesha kwa kuona mama mkwe labda anamuhisi yeye kuwa anaweza kumkataza mtoto ake asimsaidie,anatamani mama mkwe angekuwa huru kwake basi angeomba ushauri.

Kwakweli mie mwenyewe aliponisimulia mwili umesisimka na kuogopa nimtie moyo kwa neno lipi,Samahani kwa maneno mengi na kama ntakuwa nimechanganya maelezo mnisamehe...Karibuni tusaidiane kuokoa taasisi yetu ya ndoa.

Mbarikiwe sana kwa Michango mtakayotoa.

Mpe pole sana.
Haya matatizo yapo sana katika jamii zetu. inaweza tokea hata kwa mwanamke pia mfano mm imewahi ni tokea kwa girl friend wangu. Ilikuwa akiniona ananichukia sana basi mm nikajua amepata njemba nyingine kumbe haikuwa hivyo. huyo binti alikuwa ana stress za familia yao huko pluss kitu kinaitwa jini mahaba. mwishowake tuliishia kuachana.

Vitu vinavyosababisha hali hii ni kama vifuatavyo:
1. Msongo wa mawazo...........tiba yake ni kuepukana na msongo wa mawazo sasa utaepukaje mm sijui
2. Mapepo/Jini mahaba.........kuna mapepo yanayowakumba ya jinsia ya kike yanayowakumba wanaume, hili pepo litakuwa linangoneka na huyu bwana na linamfanya huyu bwana amchukie mkewe sana & viseversa....... Hapa tiba yake ni maombi tu
3. Kumchoka mwenzi wako......kuna sababu nyingi zinazosababisha umchoke mwenzi wako, akisha kuchoka basi uwepo wako kweke unakuwa ni kero kwake.

Cha msingi zidi kumfariji wakati anapotafuta chanzo cha huyo mwanaume kuwa hivyo!
 
mi kwakweli natamani sana kujua kuweka link!
kuna vitu huwa natamani sana kufanya ulinkisho lakini nashindwa !
na si wanijua nilivo na makumbukumbu!
we acha tu!
itabidi EMT atupe twisheni!
lakini hata mwaJ anajua ujue!tumwambie atufundishage!

sio tu kulinkisha lkn hata kusearch buy similarity ya content kama humkumbuki aliyepost. Those guys are wizard kwenye haya makitu. LOL
kweli kwa kumbukumbu nakukubali; l am sure ni mlaji mzuri wa vitunguu weye!
 
Back
Top Bottom