Tabia ya Mtoto Kunyonya Kidole! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tabia ya Mtoto Kunyonya Kidole!

Discussion in 'JF Doctor' started by GAMBLER, Mar 25, 2010.

 1. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2010
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari wanajamvi,

  Nina kijana wangu ana miaka 8 mpaka sasa ananyonya kidole sana mpaka akilala, nimejaribu kumkataza sana, hana dalili ya kuwacha, nikawa namchapa ninapomuona ananyonya! lakini bado tu hana dalili ya kuwacha. Ninawaombeni jamani mwenye kujuwa njia au dawa ya kukabiliana na hili tatizo atuelimishe, natumai wengi hapa atakuwa ametusaidia
   
 2. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 819
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Ni utoto tuu akikua ataacha mwenywe au kama vipi hebu mubrainwash mwmabie vidole vina wadudu ukinyonya unapata ugonjwa mbaya itamtisha ataac`ha, ila sishauri!
   
 3. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2010
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante kwa ushauri, wenye kujua namna nyingine watupe advice
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,101
  Trophy Points: 280
  Kama uko bongo anza kumpaka pilipili kali katika kidole anachonyonya, inasaidia sana na nimeona wengi wameacha baada ya kupakwa pilipili. Nimesema kama uko bongo maana majuu ukigundulika kama unafanya hivyo basi hiyo ni Child abuse na unaweza kupoteza mtoto/watoto kwa kufanya hivyo. Kila la heri.
   
 5. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2010
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante sana mkuu, niko Bongo nitajaribu kufanya, wengine mnaojua njia nyingine mnaweza kutupa
   
 6. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2010
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sasa mwanangu wa kiume mwenye umri miaka minne na yeye akinyonya maziwa wenye chupa lazima ajishike kwenye nyeti yake.Nikimwona anafanya hivyo namwambia acha kushika dudu..anaacha lakini anajisahau na kurudia.

  Nadhani kuna sababu za watoto kufanya hivyo lakini dawa ya kuwafanya waache hakuna,ila kusubiri na kuona wakikua huenda wakaacha.
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  kipake kidole kloroquine
   
 8. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2010
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante kwa ushauri, nitajaribu, wengine mnaweza mkaongeza ushauri
   
 9. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hata binti yangu wa 2 years ananyonya sana kidole gumba, nimejaribu kumdiscourage nimeshindwa. lakini akiwa occupied na michezo hanyonyi ila akiwa analia ataendup kunyonya na pia akitaka kulala. naogopa kumpaka pilipili maana akiweka kidole machoni atateseka sana. nimeamua kumwacha tu, lakini inasemekana hiyo process inaharibu dental arragement mdomoni.
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,460
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Ni hali ya kawaida tu...usi mstress mtoto na mapilipili na vitisho....akijigundua kuwa watoto wenziye hawanyonyi kidole atajiona mjinga na kuacha...mimi nimenyonya gumba mpaka 12 years
   
 11. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hata kama ni bongo sikubali umpake mtoto pilipili nitakushitaki nikukuta. kwani mtoto kunyonya kidole si chake we inakukera nn? Ok tuache hayo

  Mara nyingi mtoto kuendelea kunyonya kidole hata baada ya kupita umri wa miaka mitano inaweza kuwa njia mojawapo kwake kukabiliana na stress hasa pale anapokua amechoka au yuko bored, na wengine ni kutokana kutokujiamini au au wanakuwa na low selfconfidence.

  unaweza kumsaidia kuacha kunyonya kidole kwa upole mkataze pale unapoona ananyonya lakini si kwa kumkaripia ua kumchapa hataacha bali atakua anatafuta muda wakunyonya pale ambapo humwoni.

  jaribu kumcopare na wale rafiki zake anaowapenda sana mfano ona fulani anavyopendeza hanyonyi kidole nawewe acha uwe kama yeye

  jaribu kumkip busy na shughuli za mikono, ongea nae pale unapoona anaanza kuweka kidole mdomoni kwasababu hataweza kuweka wakati anaongea

  jaribu pia kuongea nae taratibu kuwa watoto wa umri wake hawanyinyi tena kidole

  lakini ataacha taratibu usitegemee leo wala kesho, may be weeks or months or even years, USIMPAKE PILIPILI PSE, I LOVE KIDS THEY ARE LIKE ANGLES TO ME!
   
 12. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  asante jibu lako nimelipenda, kila kitu kina wakati wake
   
 13. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,460
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Asante mama...ila kula kucha nimeshindwa kuacha...watoto wangu nao wameiga
   
 14. Loner

  Loner JF-Expert Member

  #14
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 12, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muwache Tu! hiyo inakuja kama tabia wakati akiwa hana kitu cha kufanya ndiyo ananyonya.. Miyaka inavyo zidi kwenda na siku hizi walimu wanavyotoa Home work nyingi atakua hana muda wa kuka Idol na atsahau.. Ama unaweza kutumia ushahuri wa kuweka pili pili...
   
 15. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #15
  Mar 25, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  POLE SANA, kwani imekuaffect kwa njia yoyote? mi sioni shida as long as haina madhara kiakili, kiafya na socially pia.
  mbona my 4yrs girl yani ukiona kucha zake utatamani kulia!!! lakini yeye hula akiwa busy mfano anafanya home work zake lazima kucha ziliwe sana cjui ndo kufikiria jibu!!!!!!
   
 16. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #16
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu mwanao sio wa majaribio huyo...utamtesa mtoto!! dah mara pilipili mara kloroqwine...angalia usije ambiwa kikate kidole ukasema utajaribu!!
   
 17. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #17
  Mar 25, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Mi nimenyonya mpaka form one ila usiku tu
  na akili ilikuwepo tu lakini baada ya hapo niliacha
  si ugonjwa na sidhani kama ni tatizo
   
 18. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #18
  Mar 25, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  unahangaika nini ndugu yangu......... muache tu akikua ataacha............

  unachanganya mambo mawili hapo.............. kukua kimwili na kukua kiakili............... huo umri wa miaka minane ni umri wa mwili na kutokana na maelezo yako inaonekana umri wa akili yake uko nyuma kidogo ya miaka minane............... hapo ndipo wazazi wengi hukosa hekima........... sio lazima akili na mwili vikue pamoja........ kuna watoto amabo akili iko mbele ya umri a wengine umri uko mbele ya akili. huyu wako naona mwili ndio uko mbele ya akili kwa makuzi............... jaribu kutathmini na matendo mengine ayafanyayo kama michezo, uhusiano na watoto wengine, nyimbo aazoimba, tabia ake wakati wa chakula nk...... utagundua kuwa ana tabia ambaz watoto wengine wa miaka 8 walisha ziacha.......... ushauri wangu:

  1. endelea kumsoma. inaonekana hata wewe hujamjua vizuri na kama utaendelea kumhukumu kabla hujamjua sawasawa utamuathiri kisaikolojia
  2. wakati unapoendelea kumsoma usimchukulie hatua ambazo ni harsh kama hizo ulizoshauriwa za kutumia pilipili, au viboko kama ulivyosema umewahi kumchapa............ ulifanya makosa, acha. unaweza hata kumfanya akuogope, kukuchukia, au hata akajiona hapendeki... ni hatari kwa saikolojia yake
  3. jitahidi kusisitiza shule na uhakikishe anapata elimu bora
  4. jitahidi kuzumgumza naye mara kwa mara na hasa mambo mbalimbali ya maisha kwa mfano hadithi za kidini kuhusu watu maarufu katika dini yako kutoka katika biblia kama hutojali
  5. nk.

  kwa kifupi, mwanao ni mzima hana tatizp lolote ila ukiendelea kumshughulikia bila busara wewe ndiye utakayemletea matatizo hasa ya kisaikolojia........................
   
 19. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #19
  Mar 25, 2010
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante mkuu, hapo umetupa darasa zuri sana, ubarikiwe
   
 20. kisasangwe

  kisasangwe JF-Expert Member

  #20
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 294
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  try this, kila unapomwona ananyonya kidole usimkaripie ila mweleze madhara yake.. mfano mwonyeshe picha minyoo mwambie kwamba ikiwa atanyonya kidole atapata minyoo kwa sababu mikono ni michafu na hubeba vijidudu, ikiwa ananyonya usiku, akiwa anakwenda kulala kifunge plasta. ongea na marafiki zake wakiwa shuleni wawe wanamdiscourage. akiona anazidiwa ataacha, i was staying wth 1 gal 10years alikua ananyonya vidole, nilipoanza kumwambia ambia kua atapata minyoo na ni hatari kwa afya yake taratibu alianza kupunguza hadi akasahau kabisa.

  kama ana mdogo wake na hanyonyi kidole mtolee mdogo wake mfano, au hata rafiki zake kama hana mdogo wake

  kumpaka pilipili ni harsh mno.
   
Loading...