Tabia ya mke kumkimbia mume inasababishwa na nini?

Tabia ya mke kumkimbia mume inasababishwa na nini?

Inategemea na aina ya maisha waliyokuwa wanaishi, kama alikuwa ni wa viwanja na hakuna tena viwanja unadhani atafanya nini na alishazowea starehe.

Hivyo style ya maisha ndio inayosababisha. Ikiwa umeishi na mke kwa kumjenga awe mvumilivu hata iwe vipi hawezi kukuacha cha zaidi atakufariji na kukuombea dua kila kukicha.
hao wako wachache kwenye hii dunia....
 
lakini vitabu vinasema samehe sABA mara sabini akirudi ana nafasi ya kusamehewa na kuendelea kulea.ila atakuwa keshakutesa na upweke
Ipi bora... awe anakukumbia wkt hali ni mbaya.. lakin uchumi ukipanda anakurudia...? Ndio kuna kusamehe brother... lakin ukiwa unasamehe sana.. atakuzoea.. na atakuona poyoyo... kama mwanaume lazima uweke mipaka....
 
Wanawake wengi wa dar wanaishi au kuolewa na wanaume wasio wapenda, yaani mwanamke anaishi tu na mwanaume kutokana na shida zake za maisha hivyo ikitokea mwanaume akawa hana pesa tu basi mwanamke anaona hakuna sababu za kuishi na mwanaume huyo, pia wakati huo huo yupo na mwanaume wake lakini kwakua hampenzi basi lazima anakuwa na kijamaa chakumkuna ambacho anakipenda yeye,

Na maisha yakibadilika kwa mumewe basi yupo radhi kuhamia kwa mchepuko wake bila kujali anapesa au hana,

Mi hua nasema sana kwa marafiki zangu, upendo wa kweli haufichiki hata mara moja na huwezi ku act au ku fake kumpenda mtu daima ipo siku tu utajisahau , sasa ndio hao wanao fakisha upendo hadi wanaingia kwenye ndoa au kuishi na wanaume wasio wapenda na mwishowe matokeo yake ndio hivyo…
 
mjini inakuwa kinyume , mke anakimbia badala ya kuanza kuishi maisha ya kujibana anakimbia maana jiji la watu wengi tofauti anatafuta wenye nazo aendelee kujipodoa

Tpmazembe eti "mke anakimbia badala ya kuanza kuishi maisha ya kujibana" sasa unataka Mke aishi kama SHETANI? ama sijakuelewa
 
Back
Top Bottom