Tabia ya mke kuiba na kupeleka vitu kwao inakera!

flintsky

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
654
744
Habari za jioni wadau!

Hii kweli kali nimeona niwashirikishe wadau wenye wachumba au wake!

Inashangaza kama si kustaajabisha na kuchefua na kukera kama mwanamke kila siku ukinunua kitu au vitu lazima aibe apeleke na nyumbani kwao! Kama sio kujidhalilisha ni nini?!

Hivi huyu mwanamke utasema unajenga nae fyucha au anataka akufilisi?! Ukinunua mchele au mafuta ujue nusu nusu inaenda kwao! Kila kitu kizuri ukinunua akiona tu hakina matumizi anapeleka kwao!

Sijakataa ni kusaidia kwenu ila kama kuna tatizo niambie sio mimi nanunua bajeti ya mwezi ikifika katikati ya mwezi imeisha ndio nini sasa?! Unawafichia siri kwenu ionekane maisha burudani kumbe choka mbayanmatokeo yake kufanyana chuma ulete tu!

Inakera sana hii!
 
Haujawahi kumuuliza? Wakwe hawajawahi kukushukuru au huwa wanamshukuru mkeo tu?
 
Hiyo c tabia nzur mkeo anapaswa kua waz kwao ili ujue ni jins gan utamsaidia huko kwao, daaah huyo anakosea kwa kweli
 
Ndo hivyo anaona haya kukwambia pengine wewe mkali sana..ama una dharau. Jiulize kwanza kwanini hakutaarifu issue sensitive kama hiyo.

Zungumza nae.
 
Hahahahaha mmhh em ngoja nicheke kwanza.... Huhuhuhuhuuuu.
Wanawake wana mambo jamaniiii asipokukwaza kwa hiki atakukwaza kwa kile ila kaa nae chini uongee nae alaf pia inawezekana na wewe pia unatuma matumizi kwenu kimya kimya ndo maana na yeye ana amua kupeleka kwao anachoweza.......
 
Hili suala si la kumsimanga mkeo....bali ni la kukaa na kuongea naye.....mimi naamini kwenye maongezi hapaaribiki jambo......ingekuwa habari nyingine kama angekuwa anauza......

Vile vile unaonekana wewe ni mtu mkorofi na unayeendesha familia yako kimabavu.....ndio maana hata mambo hayo ambayo ni ya kawaida anayafanya kwa siri.......

Vile vile ni vyema ungemtafutia mkeo kazi ya kufanya ili awe huru kiuchumi......
 
Habari za jioni wadau!

Hii kweli kali nimeona niwashirikishe wadau wenye wachumba au wake!

Inashangaza kama si kustaajabisha na kuchefua na kukera kama mwanamke kila siku ukinunua kitu au vitu lazima aibe apeleke na nyumbani kwao! Kama sio kujidhalilisha ni nini?!

Hivi huyu mwanamke utasema unajenga nae fyucha au anataka akufilisi?! Ukinunua mchele au mafuta ujue nusu nusu inaenda kwao! Kila kitu kizuri ukinunua akiona tu hakina matumizi anapeleka kwao!

Sijakataa ni kusaidia kwenu ila kama kuna tatizo niambie sio mimi nanunua bajeti ya mwezi ikifika katikati ya mwezi imeisha ndio nini sasa?! Unawafichia siri kwenu ionekane maisha burudani kumbe choka mbayanmatokeo yake kufanyana chuma ulete tu!

Inakera sana hii!
Naona mnaishi karibu na wakwe.
Hameni hapo haraka sana. Kama upo Dar hamia Dodoma upesi sana.
 
Tatizo ukishaligundua haliwi tatizo tena.....Hakuna mtu asiyependa kuficha siri za nyumbani kwao hadi pale inapobidi ndiyo utaelezwa, kama umegundua mkeo yuko na tabia hiyo usisubiri hadi akuambie ama mje kugombana kwa ajili ya tabia hiyo ambayo kimsingi si mbaya tatizo ni hajakuweka wazi tu...kama una uwezo tenga budget kila mwezi kama 50k hivi unamwambia wife kila weekend ya mwisho wa mwezi tutaenda kwa Mama kumsalimia ambaye ni Mama ake...So wakati mnaenda unafanya shopping ya hayo mahitaji muhimu kama mchele, sukar nk...Then unakamata wife mnaenda kwao...Naamini mkeo utakuwa umemsaidia kitu kikubwa mno na hata ukweni utapata heshima sana zilizoambatana na baraka...
 
Usiwe na wasi wasi na vitu vya kupeleka chooni. kaa naye chini mpange matumizi yenu ya wiki/mwezi mpe yeye ashike hiyo fedha ya hayo matumizi. Dawa ya mwizi ni kumkabidhi kulinda vitu.
 
Mkeo kiboka hatakagi ujinga kabisa.
Kaa ongea naye atakuelewa tu.
Halafu yawezekana humpatii au humsiadii kuihudumia familia yake ndio mana anaiba.
Ukifanya shopping ya home tenga budget ya kwao pia na si lazima iwe kubwa hata kidogo halafu nunua vitu mpe apeleke.Ukifanya hivo natumai ataacha hiyo tabia na ikiendelea tafuta njia nyingine ya kumkanya
 
Back
Top Bottom