Tabia ya kung'ang'ania

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
15,267
29,906
Huwa najiuliza inakuwaje mtu analalamika kuhusu kazi yake, lakini bado anaendelea kuifanya. Unaweza kukuta mtu mwenye ujuzi na ambaye angepata kazi mahali pengine, lakini haondoki ila kulalamika ni kila siku akilaani kazi yake.

Unaweza kukuta mtu akiwa kwenye ndoa yenye kumuumiza, inayomzuia kufanya yale anayoyataka kwenye maisha yake, lakini badala ya kutoka kwenye ndoa hiyo yenye kumuumiza, anang’ang’ania huku akilalamikia ugumu na ubaya wa ndoa yake kila wakati. Nabaki najiuliza hivi ni kwa nini haondoki?

Unakuta mtu ana tabia fulani mbaya ambayo inamgharimu na anajua.
Ni tabia ambayo akiiacha anaweza lakini haiachi, na kila tabia hiyo ikimuumiza analalamika sana, lakini hayuko tayari kujitoa kwenye tabia hiyo. Hata akipewa msaada wa namna ya kujitoa, haufuati, hataki kuiacha ingawa inamuumiza.

Kwa mujibu wa wanasaikolojia, wanabainisha kwamba kwenye ubongo wa binadamu kuna sehemu iitwayo eneo la liwazo. Kupitia eneo hilo binadamu anajisikia ana usalama akiwa mahali au kwenye hali fulani aliyoizoea, na nje ya mahali au hali hiyo, binadamu anajihisi hayuko salama na wala hana amani.

Kwa binadamu walio wengi hata kama hawana amani moyoni wanonelea ni vyema kubaki mahali au katika hali fulani kwa sababu ya mazoea tu na kwa kuwa kwa kufanya hivyo wanajiona wako salama.Ndio maana utakuta mtu ananyanyasika kazini au katika ndoa wakati umuhimu wa mambo hayo kwake haupo tena. Anachokiogopa hakijulikani!

Ukweli ni kwamba usalama wetu hautokani na msaada kutoka nje; usalama wetu unatakiwa utokane na sisi wenyewe.Lakini kama nilivyosema mazoea yanamfanya mtu kuamini kwamba ni afadhali mateso ya mahali na hali aliyoizoea kuliko kuondoka wakati hajui ataangukia wapi.

Kwa bahati mabaya kama utang’ang’ania kubaki katika eneo lako la liwazo tu, kamwe hutaweza kuujua uwezo wako halisi uliojaaliwa nao au kukijua kipaji chako na kile uwezacho kukifanikisha kwa ufanisi mkubwa.

Ukiamua kwa makusudi kusogea mbele nje ya jamaa unaofahamiana nao; nje ya mazingira uliyoyazoea; na nje ya uzoefu wako, utakuwa umejiondoa katika eneo la liwazo kuelekea njia ya kukua.

Hii ni njia ya kupanua upeo wako. Mtu yeyote anayeanza kujifunza somo jipya shuleni; ajifunzaye lugha mpya; ajifunzaye mchezo mpya; au anayeanza kazi mpya anakuwa amejisogeza nje ya eneo la liwazo.

Hebu kaa utafakari kwa makini na ujiulize kama kuna haja kweli ya kuendelea na kazi hii, tabia hii au uhusiano huu.Kama ukiona kuna haja ya kubadilika basi fanya uamuzi ulio sahihi,maana hatima ya maisha yako iko mikononi mwako.
 
Unakuta watu wengine wanaanzisha uzi za ajabu ajabu hawafati sheria za JF alafu anaandika..
"N:B, Mod mbona mnafuta baadhi ya Uzi zangu but fine"
#Hapa kazi tu
 
Huwa najiuliza inakuwaje mtu analalamika kuhusu kazi yake, lakini bado anaendelea kuifanya. Unaweza kukuta mtu mwenye ujuzi na ambaye angepata kazi mahali pengine, lakini haondoki ila kulalamika ni kila siku akilaani kazi yake.

Unaweza kukuta mtu akiwa kwenye ndoa yenye kumuumiza, inayomzuia kufanya yale anayoyataka kwenye maisha yake, lakini badala ya kutoka kwenye ndoa hiyo yenye kumuumiza, anang’ang’ania huku akilalamikia ugumu na ubaya wa ndoa yake kila wakati. Nabaki najiuliza hivi ni kwa nini haondoki?

Unakuta mtu ana tabia fulani mbaya ambayo inamgharimu na anajua.
Ni tabia ambayo akiiacha anaweza lakini haiachi, na kila tabia hiyo ikimuumiza analalamika sana, lakini hayuko tayari kujitoa kwenye tabia hiyo. Hata akipewa msaada wa namna ya kujitoa, haufuati, hataki kuiacha ingawa inamuumiza.

Kwa mujibu wa wanasaikolojia, wanabainisha kwamba kwenye ubongo wa binadamu kuna sehemu iitwayo eneo la liwazo. Kupitia eneo hilo binadamu anajisikia ana usalama akiwa mahali au kwenye hali fulani aliyoizoea, na nje ya mahali au hali hiyo, binadamu anajihisi hayuko salama na wala hana amani.

Kwa binadamu walio wengi hata kama hawana amani moyoni wanonelea ni vyema kubaki mahali au katika hali fulani kwa sababu ya mazoea tu na kwa kuwa kwa kufanya hivyo wanajiona wako salama.
Ndio maana utakuta mtu ananyanyasika kazini au katika ndoa wakati umuhimu wa mambo hayo kwake haupo tena. Anachokiogopa hakijulikani!

Ukweli ni kwamba usalama wetu hautokani na msaada kutoka nje; usalama wetu unatakiwa utokane na sisi wenyewe.
Lakini kama nilivyosema mazoea yanamfanya mtu kuamini kwamba ni afadhali mateso ya mahali na hali aliyoizoea kuliko kuondoka wakati hajui ataangukia wapi.
Kwa bahati mabaya kama utang’ang’ania kubaki katika eneo lako la liwazo tu, kamwe hutaweza kuujua uwezo wako halisi uliojaaliwa nao au kukijua kipaji chako na kile uwezacho kukifanikisha kwa ufanisi mkubwa.

Ukiamua kwa makusudi kusogea mbele nje ya jamaa unaofahamiana nao; nje ya mazingira uliyoyazoea; na nje ya uzoefu wako, utakuwa umejiondoa katika eneo la liwazo kuelekea njia ya kukua.
Hii ni njia ya kupanua upeo wako. Mtu yeyote anayeanza kujifunza somo jipya shuleni; ajifunzaye lugha mpya; ajifunzaye mchezo mpya; au anayeanza kazi mpya anakuwa amejisogeza nje ya eneo la liwazo.

Hebu kaa utafakari kwa makini na ujiulize kama kuna haja kweli ya kuendelea na kazi hii, tabia hii au uhusiano huu.
Kama ukiona kuna haja ya kubadilika basi fanya uamuzi ulio sahihi,
maana hatima ya maisha yako iko mikononi mwako..........

N:B. Mod Mbona mnafuta Baadhi ya yuzi Zangu bt Fine
Ndoa za kikristo hazivunjiki hadi kifo
 
Ipo nafasi ya uvumilivu pia katika maisha yetu ya kila siku....Na hatupaswi kuwa wepesi ku-give up, dawa ya tatizo lolote ni kupambana nalo na si kulikimbia hata kwenye ndoa inawezekana ni mpango wa Mungu kukupa mke/mme huyo ili upambane na madhaifu yake kwani kupitia wewe atabadilika..
 
Ukiona hivyo chance za kupiga deal kubwa ni nyingi...kuna watu hawagusi salary zao ati
 
Ipo nafasi ya uvumilivu pia katika maisha yetu ya kila siku....Na hatupaswi kuwa wepesi ku-give up, dawa ya tatizo lolote ni kupambana nalo na si kulikimbia hata kwenye ndoa inawezekana ni mpango wa Mungu kukupa mke/mme huyo ili upambane na madhaifu yake kwani kupitia wewe atabadilika..
Yani manuu ha ha ha nkikuonaga najisikia kucheka sana, siku mmoja ntakutafuta tuongee kwa kina
 
Ambiere kiviere mkujinga umesema kweli.. Hiki kitatizo kime kua kama kinasaba(DNA) nadhani ukiamua kufanya utafiti kutokana na hili utakuta idadi kubwa ya watu ni ya wapi etc

Tuna haja ya kujenga watu majasiri
 
Na waaminifu
 
We kipi hapo kati ya hivyo umeweza kukikwepa?tupe na mrrjesho
 
Kuna malalamiko mengine ni njia tu ya mtu kujitamba mbele za watu
sio ukiona mtu analalamika kuhusu mkewe au mumewe ujue ndo hivyo hivyo
wengine wanapenda tu kwenda na jamii ilivyo
akiona watu wengi wanatoa lawama kwa wapenzi wao anajiunga tu
huku moyoni yuko tuli...karidhika na mtu wake
 
The Boss huwa nakukubali sana coz huwa umwaga cheche sana

N:B Congratulation The Boss
 
Back
Top Bottom