Tujikomboe Finance
JF-Expert Member
- May 8, 2013
- 212
- 81
Wanajamii,
Siku hizi kumeibuka tabia miongoni mwa watanzania kushangilia/kufurahia mtu anapopata matatizo. Zamani ilikuwa mtu akipata tatizo hata kama ni mtu mbaya jamii ilikuwa ikisikitika na kumsikitia huyo aliyeathiriwa.
Siku hizi ni tofauti kabisa, kuna hali fulani ya chuki imeanza kujitokeza katika ya watu wenye nafuu fulani ya maisha/fursa/kipato. Nitatoa mifano michache ambayo mimi mwenyewe nimeshuhudia.
1. Siku moja nilikuwa mtaa wa shule ya uhuru, nikiwa kwenye foleni kibaka akanyoa kioo (side mirror) huku watembea kwa miguu wakiona na kuangalia. Jamaa mmoja akasema '' aah bora wawaibie na nyie muone uchungu kama tunaotembea'' kauli hiyo iliungwa mkono na watu kibao na wakafurahi kweli kweli.
2. Mara nyingi ukiwa unaendesha gari ukapishana/kukwaruzana na mtu wa daladala, abiria wa daladala mara nyingi watamsaidia dreva na kukushutumu wewe hata kama kosa ni la daladala. Na wengi hutoa kashfa kama ''gari la mkopo'' gari la kuazima, au gari la dada yako ili mradi tu waonyeshe chuki zao
3. Hivi sasa watu wamekuwa wakishangilia sana wanaposikia habari za kutumbuliwa majipu. Ukiwasikia wakifurahia utasikia kauli kama ''walikuwa wanajidai sana, ''sasa tuwe wote sawa, wametunyasasa sana, tuisome namba wote, heshima irudi etc.
4. Hivi karibuni kulikuwa na zoezi la kubomoa nyumba na vibanda vya biashara maeneo ya Mbezi mwisho. Nilishangaa sana kila kibanda/nyumba kikivunjwa wamiiliki walikuwa na majonzi lakini vijana wengi walikuwa wanashangalia na kusema ''yes sasa tuwe sawa wote, hakuna cha mwenye hela, wote tufulie tu............
Mimi najiuliza hii ''akili'' ya kuona umaskini wa mtu unasababishwa na uwepo wa mtu mwenye kipato zaidi yako inatoka wapi? Hii chuki dhidi ya walio nacho/wenye fursa/ wenye kazi dhidi ya watu wengine sio mwenendo mzuri hapo mbeleni itakuja kuwa tatizo kubwa