Hili tatizo mkuu lina mizizi halijaibuka tu ghafla. Wakati wa mwalimu Jk Nyerere huduma zajamii zilikuwa juu kiasi kwamba hakukuwa na tofauti kati ya maskini na tajiri (katika huduma za jamii)
Mtoto wamkulima namtoto wa waziri walisoma shule Moja, walikalia dawati moja nk. Vilevile Mzee mwenye nacho na asiyenacho walitibiwa hospitali moja nakuhudumiwa na nesi na Dr huyohuyo.
Hiyo ndo ilikuwa Tanzania ambayo ilikuwa moja, kilammoja alikuwa ndugu wa mwingine bilakujali ni nani, anatokea wapi na ana nini ama hana nini.
Tulipofika mahala tulatupana kilammoja akaanza kuangalia tumbo lake lishibe kwanza, nahata akishashiba haishii hapo tu bali alishe mpk mbwa wake kwanza. Hapo ndotulipotengeneza hii chuki tunayoona ndani ya jamii.
Msidhani matukio yaubadhirifu wamali za umma kama TWIGA kupandishwa ndege, Eppa, Escrow nk kwamba wasionacho hawafuatilii na haiwaumi. Inawama sana sema hawajui wamlaumu nani na wamsamehe nani. Kwahiyo ukiunganisha yote hayo+ ugumu wamaisha, hiyo chuki itaendelea kuwepo nakwa viwango vya kutisha huko mbele ya safari. Ni suala la wakati tu.
Solution nikuhakikisha umaskini unapungua haraka iwezekavyo hasahasa kwa kuanzia nakuboresha huduma muhimu za jamii kama Elimu sawa, matibabu nk.