rosemarie
JF-Expert Member
- Mar 22, 2011
- 6,887
- 3,441
Mimi siyo mpenzi sana wa jukwaa hili, lakini nimeona ni vema kuja hapa na kutoa ushauri wangu wa bure,
Tabia ya mafumanizi au kufumania imeota mizizi na inatakiwa kukemewa kwa nguvu zote, nasema hivyo siyo kwa sababu napenda kuona watu wakitoka nje ya ndoa la hasha bali napenda kulinda heshima ya kizazi tulicho nacho kwani kufanya vitendo hivyo vya mafumanizi ni kushusha hadhi ya taifa letu na kuonekana hatufikirii vizuri.
Picha za kufumania zinaonekana kwenye mitandao kila siku tukiona picha za watu wa heshima na tunaowajua,watu waliominika kwenye idara mbalimbali ambao ni binadamu tu wa kawaida wasio wakamilifu.
Kwa kweli ni kitendo kibaya sana na kinaonyesha ni jinsi gani tulivyo na uwezo mdogo wa kupambanua mambo, Mke wako akiamua kwa hiari yake bila kulazimishwa au kubakwa tafadhali sana mpe nafasi kwani kuna sababu nyuma ya pazia,wanawake ni watu wenye akili sana japo hazionekani waziwazi, naomba uelewe mke wako siyo mali yako hata kidogo wala siyo mtumwa wako bali ni msaidizi wako na hakuna lingine,kwa taarifa yako tuu ni kwamba mke wako akiamua kutoka nje ya ndoa amekudharau sana.
Anapoamua kutoka nje ya ndoa siyo kwamba hajui bali anajua anachokifanya na ameamua hata kama utamfumania mara mia na kama anataka atatoka tena na tena.Hivi umewahi kufikiria madhara ya kufumania halafu mtu anawekwa front page ya magazeti?
Huyo mtu hana familiya hana watoto ndugu wazazi jamaa na marafiki? Hivi tunafikiria mbali kabla ya kuchukua hatua? Hivi hao wanaofumania ni watakatifu? Ndiyo maana .''Yesu akawaambia wale watu waliomleta mwanamke aliyefumaniwa asiye na dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe'', mwenye uwezo wa kumzuia mwanamke asitoke nje ya ndoa ni mwanamke mwenyewe na baba yake au mama yake na siyo wewe mume wake, kumbuka pale juu nimesema mke wako siyo mali yako hata kidogo.
Ushauri wangu ukimfumania mke wako tafadhali sana kaa chini tulia mwite kwa heshima na muulize ni kwa nini anafanya vile,jibu utakalopata fikiria na chukua hatua, kama kuna matatizo ndani ya nyumba na kama bado unamwitaji mke wako jaribu kurekebisha ili uendelee na ndoa yako, kama ukiona hakuna jinsi nyingine tafadhali mwandikie talaka nitashangaa sana mwanaume kumfumania mke wake na kumrudisha nyumbani na maisha kuendelea na umeshatoa siri kwenye mitandao na magazeti, je watoto wako na ndugu na marafiki watakuonaje tumieni akili kidogo mbona kila mtu amepewa akili ni kuamua kutumia.