Tabia ya binadamu

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
3,243
4,379
Binadamu ni kiumbe chenye roho ya kipee.

Anapenda sana furaha ila hajali uhitaji wake wa furaha ana atamuumiza kiasi gani rafiki/ndugu yake binadamu ni kiumbe kinachohitaji mafanikio ya haraka pia hapendi mipango yake ifelishwe na mtu yeyote lakini binadamu huyu huyu yupo radhi kumshambulia mwenza wake ashindwe kwa kila jambo.

Anaweza kukushambulia kwa vyovyote ili wewe ushindwe iwe kwa maneno au vitendo pasi kupata faida yeyote lakini hajali ni kiasi gani anamkwaza mwenza wake binadamu huyu huyu hupoke fadhila kwa mikono miwili ila hurudisha kwa mkono mmoja hakika kuwa binadamu ni kiumbe kilichokosa hekima na busara ila kuna baadhi yao wapo ila asilimia kubwa tumekosa sifa hizo.

Ila lengo ni moja kuipa furaha moyo wako so kivyovyote vile tusikate tamaa kisa kusema au kufanyiwa kitendo ovu na binadamu yeyote muhimu ni kumuomba Mungu akuepushe na husda na mabaya ya mbeleni mwako.

Malengo ndiyo furaha yako, juhudi ndiyo silaha yako.
 
Back
Top Bottom