Tabia hizi sio nzuri, wahusika tubadirike.

Tabia hizi sio nzuri, wahusika tubadirike.

Kasomeko

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2018
Posts
627
Reaction score
1,215
Wakuu habari zenu!
Kuna hizi tabia mbili ambazo binafsi hua zinanikera sana hivyo nimeona niziweke hapa huenda kuna zinao wakera pia. Vile vile huenda wenye tabia hizi wakawa hawajui kama zinaudhi, kupitia maada hii naamini watajifunza na kuachana na tabia hizi.

Kwanza, tabia ya kuingilia maongezi ya watu. Hapa nitaongelea pande zote mbili yani kwa anae ingilia maongezi na upande wa wlio ingiliwa maongezi yao. Unakuta watu wamekaa pembeni wametulia wanajadili kitu usichokijua/ kisichokuhusu, wewe unafika hapo unawasalimia kisha unakaa hapo hapo na kuanzisha mazungumzo mapya/ maada mpya!!!

Mala nyingi nikiwa nimejitenga pembeni na rafiki mmoja au wawili hua inatokea akaongezeka mtu mwingine akaingilia maongezi yetu. Hii mala nyingi husababisha watu kusitisha walichokua wanaongelea ili alieingilia maongezi asijue maada ilihusu nini!

Wewe unae ingilia maongezi ya watu unatakiwa ujue kua unawapotezea muda maana itabidi wakusubili hadi uondoke ndipo waendelee na maongezi yao. Ukikaa hapo kwa muda mrefu huenda ukasababisha watu waahirishe maongezi yao. Kwahiyo ni vizuri kuuliza kama unaweza kuungana nao kwenye maongezi yao, sio unafika nakuvuta kiti unakaa kana vile ulikua na miadi nao!

Mnaoingiliwa maongezi, hua inatokea umekaa na mtu mnaongea mala anatokea mtu unaefahamiana nae wewe tu, yaani hafahamiani na unae ongea nae. Unasitisha maongezi na uliekua unaongea nae kisha unaanza kuongea na huyu aliewavamia yani hani hadi unasahau kama kuna mtu mwingine pale!! Hii sio sawa! Unatakiwa kumwambia mvamizi wenu kua samahani ndg yangu nina maongezi na huyu bwana/ bibi hivyo nitakutafta baadae.

Pili, tabia ya kuongea sana na simu uwapo kwenye kikao/ naongezi na mtu/ watu. Rafiki yako kakuita sehemu akupe fursa ama taarifa ambazo zitakusaidia. Mpo katikati ya maongezi mala simu yako inaita, unapokea unaongea dakika 5! Mnaendelea na maongezi kidogo tu sms imeingia unaijibu huku unaendelea kumsikiliza rafiki anaekupa dili!! Jitahidi kama simu na sms unazopata sio vya mhimu sana achana navyo umsikilize rafiki yako.

Tabia hizi zitakunyima fursa, ikitokea rafiki yako kaingilia maongezi yetu namimi ndiye niliekua nakupa fursa, nitaondoka zangu nikuache uongee na rafiki yako. Na ukiwa unaongea sana simu na kunifanya nikusubiri hadi umalize kuongea/ kujibu sms napo nitaondoka ili uchati vizuri.

Utachukiwa na watu!! Ukimkuta rafiki yako anaongea na mtu mhimu, ukaharibu maongezi yao hadi huyo mtu mhimu akaondoka ujue kabisa rafiki yako atakuchukia.

Jf ni kama jamii haswaa kuna watu wa kila aina kuna werevu, wenye busara, watani, wahuni, vichaa n.k n.k hivyo nategemea michango ya kila aina.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwann ukumwambia huyo aliyeingilia maongezi yenu mda huohuo

Love and peace
 
Kwann ukumwambia huyo aliyeingilia maongezi yenu mda huohuo

Love and peace
Hua nawaambia sana mimi ila naona wanaongezeka nimeona niwaambie na waliopo humu wajue sio poa halafu sio kila mtu ana uwezo wa kumwambia mvamizi asubili, na sio kila mvamizi unaweza kumsubilisha/ kumfukuza. Hivyo n jukumu la wavamizi wote kujua kua uvamizi haupendezi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
halafu bashite ndio ana hiyo tabia sana kibaya zaizi akianza kuongea anakulowesha mate uso mzima
 
Tabia zinazokera zipo nyingi mno nadhani kwa baadhi Yetu uangalizi wa wazazi ulikua hafifu.

Unakuta anakuja mtu kukaa kwenye meza uliyokaa wewe wakati kuna nafasi nyingine nyingi tu zilizopo wazi. Huwa inakera mno.
 
Back
Top Bottom