Tabia Hii

njiwa

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,936
2,000
Matatizo ya ndugu au wazazi kuingilia ndoa ni suala lingine linalotajwa sana katika kuvunjika kwa ndoa nyingi. Bila shaka wengi wetu tunajua kwamba mila na desturi zetu (ni potofu, katika hili) ndoa inakuwa ni ya ndugu na wazazi pia, siyo wanandoa peke yao. Lakini kwa bahati mbaya sana katika ndoa nyingi ndugu wa mwanaume ndiyo ambao huingilia ndoa kwa kuwasakama wake katika ndoa hizo wanaume wengi hujikuta wakiwaunga mkono wazazi au ndugu zao dhidi ya wake zao!

Tuache hii tabia esp ndugu wa upande wa mume ....
 
gfsonwin

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
18,244
2,000
njiwa namshukuru sana Mungu sijawah kuwa muhanga a hali hii ila naweza kuisemea kidogo.

siku zote ukiona ndgu wa mume wanausumbufu basi jua kuna mwanya wameupata mahali ama mke ni msemaji sana? ama mume yuko karibu sana na ndugu zake ingawa kaoa? ama wanaish na ndugu nyumba moja. wengi wa watu nilio waangalia niligu dua kwamba hizi ni sababu za wao kuanza kugombana.

busara ya kutumia ili kukwepa hali hii ni hii
mke asiwe mtu a maneno mengi, yaani stori za kupiga mara kwa mara ukweni asiwe nazo.
mume akioa aambatane na mkewe na wao wawili wasimame kama wao hata kwenye shida hasa za kifedha wasiombe kwa ndugu bora kwa marafiki ili nidhamu iwepo na baba aweze kusimama kama baba.
istoshe mume na mke wasioane wakaish karibu na ndugu wa upande wowote ule ama nyumba moja. oa tafuta nyumba yako nje na hapo kwenu msiseme nyumba ya bure mkae humo lazima ndoa ivinjike hii.
 
Last edited by a moderator:

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
47,824
2,000
Pengine hii pia usababishwa na mwanaume kutokuwa na misimamo na kupenda kushirikisha kila tatizo la ndoa watu wengine hasa ndoa! Mnaweza kuwa mbali na ndugu lakini tatizo kidogo limetokea unapiga simu na ndugu wengi hasa wa mwanaume linapotokea titizo ukimbilia kutoa lawama kwa mwanamke ndio hapo huwa chanzo cha matatizo!

ndio maana nikasema muame akiwa na ukaribu na watu wa nyumbani kwao ni tatizo sana. hizi sie husema " mwanaume bado hajatoka nyumbani"
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,760
2,000
Ni sawa kabisa gfsonwin. Kama kukiwa hakuna mwanya wa watu wa nje kuingilia mambo yenu hakuna anaeweza kuvuruga ndoa. Ila mkiachia mwanya, sio ndugu wa mume tu, hata mahausigelo wao na walinzi wa nyumba zao watawavuruga haswaa! Na kutokuwa na amani ni dalili ya mwanaume kushindwa kuwa kichwa cha nyumba.
 
Last edited by a moderator:

gfsonwin

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
18,244
2,000
Ni sawa kabisa gfsonwin. Kama kukiwa hakuna mwanya wa watu wa nje kuingilia mambo yenu hakuna anaeweza kuvuruga ndoa. Ila mkiachia mwanya, sio ndugu wa mume tu, hata mahausigelo wao na walinzi wa nyumba zao watawavuruga haswaa! Na kutokuwa na amani ni dalili ya mwanaume kushindwa kuwa kichwa cha nyumba.
a
hapo kwenye red umenena. ni bora watu waseme mumeo ammejitenga kuliko awe ni mtu wa kuwachukulia poa ndugu na mabinti wa kazi. napenda sana mwanaume ambaye yuko siriaz na hana masihara na watu ya hovyo
 
Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,969
2,000
[/COLOR][/B]a
hapo kwenye red umenena. ni bora watu waseme mumeo ammejitenga kuliko awe ni mtu wa kuwachukulia poa ndugu na mabinti wa kazi. napenda sana mwanaume ambaye yuko siriaz na hana masihara na watu ya hovyo
Laiti ningekuwa na namba yako ningekutumia airtime. umeongea bonge la point.
 
Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
36,025
1,500
usikae na wakwe karibu saana

sie kule kwetu zamani, ukiolewa unaenda kaa kwa wakwe na mmeo.

Baada ya muda, mnapewa fungu lenu mkaanze maisha
sababu tu msije anza kugombana hapo nyumbanilol, ukweni kuna visa mno.. huwa yatokea tu ...
 
BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
31,316
2,000
udhaifu wa mwanaume ndo unapelekea ndugu wa mume kuongoza ndoa kwa remote control.........

Juzi kati kuna dada alikuwa analalamika huko fb mumewe mipanho ya maendeleo anapanga na ndugu zake....kaongeaaaaa haijasaidia katumia marafiki za mume wamshauri mwenzao weeeee hola, wasimamizi wamejaribu hola, mwisho wa siku akagundua hati ya kiwanja kwenye droo kuuliza mume kawa mbogo dada wa watu kanyanyua mikono juu ameamua nae ajishughulishe na maendeleo binafsi, sasa ndoa si ndo ishaparaganyika hapa?

Naamini humu ndani kila mmoja ni ndugu wa mwanaume tafadhali tafadhali waacheni wanandoa kwa amani......

Mwanamke wa watu kaolewa na mtu mmoja na si milioni moja mheshimuni na msimpangie nyumba yake, waacheni wanandoa wajipangie maisha yao.....
 
Tized

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
4,023
2,000
Binafsi naona inachangiwa na baadhi ya haya yafuatayo.
Mosi, mume kutokusimama katika nafasi yake kwa ukamilifu na kwa msimamo ulio thabiti, Mwanamume ameumbwa kuwa kiongozi akianzia na familia yake.

Mbili, Kusikiliza upande mmoja na kufanya maamuzi, ni vizuri kusikiliza pande zote kama kuna malalamiko na ukemee hizo hali mbele ya wote. Wataheshimu

Tatu, kumsikiliza sana mama yako (upande wa mwanaume) Wakaka wengi wana ukaribu mkubwa sana na mama zao, hali hii imewazidi wengine kufikia hatua ya kuchukua maamuzi ya mama na kuyapelekeka kwa familia yake bila kuyatazama kwa makini, hatimaye inavuruga nyumba.

Pia kuwa wasemaji semaji saana kupitiliza, kunatukosesha mara kwa mara maana ulimi haufugiki.

Na Nyumba yoyote inayoongozwa na mwanamke kwa maana ya kwamba Mume yupo lakini maamuzi anafanyiwa na mkewe au mamaye, ni matatizo, na huyo mwanaume ni tatizo pia, hata wadada wengi walio smart wakikuona wewe kama mwanamume huna maamuzi unayumba yumba tu, wanakereka sana. ''Mwanaume ni Kichwa cha nyumba/familia'' lazima tusimame kuziongoza familia zetu na kuzipatanisha pale kunapotokea kutoelewana na kuweka misingi imara na misimamo ya kifamilia ambayo itaheshimika na kila mmoja kwa nafasi yake, vinginevyo ndoa na mahusiano ya familia zetu itakuwa si salama sana.
 
peter daudi

Senior Member
Sep 16, 2012
112
225
Hahika katika ndoa mke na mme inatakiwa kuwa na msimamo maana kufungwa kwa ndoa tayari ufalme mpya unakuwa umeanzishwa hivyo ninyi(wanandoa) ndio watawala. Maneno na chokochoko kutoka kwa ndugu vinatakiwa kuishia mlangoni.:A S 103::target::target::A S 103:
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom