Tabia au vitendo gani vinakuchukiza?

torvic

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
3,806
9,300
Vitendo au tabia gani unachukia kwa mwanaume/mwanamke kiasi ambacho hata kama upo kwenye mahusiano unaweza kukatisha mahusiano yenyewe kwasababu ya tabia hizo
kwa ME wengi hawapendi wanawake wachafu, msichana katoka kupika plus mjoto wa jikoni alafu hapo hapo anajipachika ma makeup yake, asee! Utasubiri sana ndoa
KE sijui tabia gani wanachukia kutoka kwetu, hope watazitaja za kutosha.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
uchafu...mtu katoka kuvaa viatu vimelowa vinanuka akiingia ndani anaviweka mvunguni chumba kinanuka kama panya kaoza..kesho anavaa hivohivo..akipanda daladala abiria hawapumui.
my bae is soo clean..
 
Aggressive behavior mi kwa upande wangu sipend mwanamke mkali,afu pia mweny mashindan kweny uhusiano,i love peace,..and non dramatic relations,afu na awe msafi,..
 
Kupost kila picha fb.

Unakuta picha nyingine hazijamstiri vya kutosha ila inawekwa fb.

Sipendiii
 
Aya mambo magumu!uvumilivu ndio utuongoze bila kujali madhaifu ya mwenzako!
 
Daaah dharau sipendi asee, maana imebeba vitu vingi sana. Akiwa na heshima hayo mengine yatakua rahisi kuyabadilisha
 
Mwanaume mjuaji!!! Kila unaloongea au unalofanya anakuona huna akili na anakukosoa.
mwenye dharau na nyodo... Yaani anakuja kwangu anakuta nimepika ugali na maharage anaanza kujishaua kusema mimi sipendi ugali maharage... Nakula ugali na nyama choma tu au samaki wa kukaanga!!! Nyooo!!! Nitoe hela yangu na mda wangu kukupikia alafu unakuja kuniambia huli chakula hucho... Sio kwamba una aleji, eti hutaki tu!!! Aisee mwanaume anifanyie hizo nyodo kama yeye ndo anatoa hela ya chakula. Ila kadri tunavyokua pamoja nikiona kuna chakula unakifurahia sana kuliko kingine basi ntaongeza jitihada kumpikia anachopenda... Sio kuleta minyodo yake ya kipuuzi
 
baasi baasi mama eeeh..!!!
 
1. Sipendi mwanamke anayetaka kunitawala kwenye maamuzi yote maishani
2. Usista duu wa kupitiliza na kudeka kwa kupitiliza
3. Mwanamke much know na dharau nyingi
 
Mtu anae nuna nuna kila muda, kukasirika kwa kitu kidogo na kuto niheshimu yani kuongea maneno ya dharau mbele yangu hapo siku mbili unapigwa chini.......
 
sipendi mwanaume anaepiga kelele au anaongea wakati wa tendo la ndoa, mwanaume mmbea, mwanaume asiejiamini
 
sipendi mwanaume mchafu

sipendi mwanaume wa kuropoka ovyo/mjuaji wa kila kitu

Mwanaume Gubu uuwiii nakuacha kama ifuatavyo

Mvuta sigara ndio hata habari usinipe

Mwenye mavaz ya kihuni, kufuga manywele kama msitu wa amazon hapana
 
sipendi mwanaume anaepiga kelele au anaongea wakati wa tendo la ndoa, mwanaume mmbea, mwanaume asiejiamini
hapo kwenye tendo la ndoa pagumu kidogo, sasa kama utamu ukinoga wew muache apayuke tu!
 
Back
Top Bottom