Aegon Targaryen
Member
- Sep 1, 2017
- 24
- 21
Wakazi wa Tabata Kimanga kwa muda mrefu imekuwa kama vile tumeshaulika. Tumepigia sana kelele suala la barabara yetu ambayo ikinyesha mvua ni tabu tupu, wenye magari madogo wanayapaki wakati wenye magari makubwa wanakumbana na adha ya kujaa maji. Kipindi cha jua litapita greda likwangue lakini tunakoma na vumbi.
Suala la ubovu wa stendi na kukosekana soko lilikuwa kwenye ajenda kuu ya kampeni 2015 lakini mpaka sasa hatuoni chochote. Kila siku tunamuona mbunge anafanya ziara kata nyingine za jimbo lakini Kimanga hathubutu kukanyaga.
Fedha za mfuko wa jimbo tunasikia zimegawanywa lakini tukiwauliza watendaji wanatuambia hazijafika kwenye kata zetu.
Nadhani imefikia wakati serikali ikubali kwamba jimbo la Segerea ni kubwa inatakiwa ligawanywe ili Kimanga na Buguruni vijitigemee maana tunachokiona kwa sasa ni mbunge wetu kufanya kazi kwa kata za Segerea tu.