Taazia ya Dkt. Dau kwa Benjamin Mkapa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,787
30,083
TAAZIA YA DR. DAU KWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA NA YALE MAKUBWA NA MAZITO AMBAYO HAKUYASEMA

Hakuna kitu kinagusa fikra na linabaki akilini na kuhifadhika kwengineko kama neno lililoandikwa.

Aliyesoma taazia ya Dr. Dau kwa rafiki yake Benjamin William Mkapa atakuwa ameona kanitaja kuwa mimi ndiye niliyemsukuma kuandika taazia ile.

Dr. Dau hakuwa amefikiria kuandika taazia lakini nikamweleza kuwa ana wajibu kama rafiki ya Mkapa kuandika kitu kuhusu sahib yake na sababu kubwa niliyompa ni kuwa kama mwandani wake anawajibika kumpa mkono wa buriani kwa taazia ipatikane nafasi ya kumweleza katika yale ambayo wengi hawayajui kwani si wengi wanaojua urafiki na mapenzi yalikukuwapo baina yao.

Kuna mengi Balozi hakuyasema labda kwa kuchelea na hayo ni mazito mno.

Kuna jambo Dr. Dau aliniambia kuhusu Mkapa ambalo wengi naamini litawastaajabisha.

Mkapa alikuwa anaguswa na Uislam wa Dr. Dau na akimstahi sana kwa sifa hii.

Anasema Mkapa alimkataza mashauri wake wa uchumi asimwingize Dr. Dau katika maamuzi yoyote yale ambayo shirika analoliongoza Dr. Dau NSSF litakuwa na uhusino wowote na chombo chochote cha biashara ya pombe hata kama NSSF itanufaika.

Binafsi nilishtuka sana tena sana kupita kiasi.

Balozi ni mzungumzaji katili sana kwangu.

Kwa miaka tuliyoishi pamoja anajua kitu gani anambie avuruge ubongo wangu na kuniharibia siku yangu nzima tena kwa makusudi.

Hata sijapata muda wa kushusha roho akaniongoza kishindo kingine.

Akanambia iko siku Rais Mkapa kamwita Ikulu na ilikuwa siku ya Ijumaa.

Rais akawa kashikika hadi kufika kuonana na Dr. Dau muda unakimbilia saa tano.

Rais akamtaka radhi sana kwa kumwita waonane siku ile na kwa kumweka ilhali yeye Dr. Dau anatakiwa kwenda kusali Ijumaa.

Rais Mkapa akamtaka radhi sana Dr. Dau na hakumweka sana akamruhusu kuondoka huku akirejea kumtaka radhi.

Ule ukimya wangu kwa huu mshtuko wa pili kinywa kilinijaa mate.

Rais Mkapa anamtaka radhi Dr. Dau mteule wake aliyemwita Ikulu kwa jaili ya mambo ya kazi...

Lakini uzuri wa kuandika ni kuwa unachokoza fikra za wasomaji na watakayoandika yako yatakayo kufurahisha na yapo pia yatakayo kuchoma nafsi.

Sasa unatakiwa uwe tayari kuumizwa nafsi yako.

Mengi yameandikwa kuhusu taazia hii ambayo jana ilizunguka sana duniani na nimejikuta katikati ya kalamu ya Balozi labda kwa kuwa Dr. Dau ni ndugu yangu na labda pengine kwa yeye kusema kuwa mimi ndiye niliyemshinikiza kuandika taazia ile.

Iwe iwavyo wengi wawalioniandikia wamefurahishwa na taazia ile na wale ambao kidogo walitaka mengi zaidi ya Mkapa Balozi angeyaandika lakini hakuyaandika wengi wao wamekuwa wakimaliza na maneno ya kusema kuwa hakuna mkamilifu ila Allah.

Nimeona nami nieleze jinsi taazia hii ilivyoniathiri mimi mchezea pembeni hasa baada ya kuelezwa yale ambayo ingawa ni muhimu sana Balozi kwa kuchelea akaamua kuyanyamazia kimya.

MOHAMED SAID, HASSAN MNJEJA NA DAU.jpg
 
Dr dau msomi mdini moja ya watu wa ajabu na ovyo sana, unaliongozaje shirika la serikali isiyokua na dini kidini
Ongeza maneno kidogo ili walau nijaribu kujiuliza kuwa ilikuwaje Mzee Mkapa(Mkatoliki aliyelelewa na kanisa) alishindwa kuliona hilo kiasi akamteua?
 
Kwa mtu aliyekua Nssf kipindi Cha dau atakuambia, mtu aliweka mpaka sehemu za kusalia ndani ya taasis ya serekali serious
Na kipind Cha mwisho wa mwaka taasis inanunua miti ya krismass na kad kibao pamoja na Yale maandish wanayawekaga mapokez
 

Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom