Taasisi ya "Usheikh'' na fani ya uigizaji Tanzania

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,193
30,533
TAASISI YA "USHEIKH'' NA FANI YA UIGIZAJI TANZANIA
Written By Mohamed Said on Saturday, March 21, 2015 | 12:14 PM

10942489_893855877341652_2687773226950844526_n.jpg
Masheikh na Maimamu 83 kutoka wilaya nzima ya Bagamoyo wamfuata mhe.lowassa nyumbani kwake dodoma kumshawishi agombee..
LOWASA NI CHAGUO LA MUNGU
SIMAMA NA UHESABIWE

Hii picha nimeipata katika mtandao. Nilipokuwa naitazama kinywa kimenikauka mate. Najiuliza hivi hii taasisi ya usheikh mbona ghafla imekuwa taasisi ya vichekesho? Hawa masheikh wa Bagamoyo wanatoka Bagamoyo ipi? Hawa masheikh wanatoka misikiti au madrasa ipi? Huu usheikh siku hizi imekuwa ya mpata mpatae yaani mtu akivaa kanzu, koti na kofia tayari keshakuwa sheikh?

Sasa wazo jingine likawa linanijia....Tanzania ni mwiko kuchanganya dini na siasa. Sasa vipi tena hawa masheikh wanatoka Bagamoyo hadi Monduli kwenda kufanya siasa? Haya mambo mbona mimi yananikoroga kidogo?

Kweli TANU ya 1950s wakati Tanganyika inadai uhuru kilikuwa chama cha masheikh - Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Mohamed Ramia, Sheikh Yusuf Badi, Sheikh Issa Nasir, Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Haidar Mwinyimvua na wengine wengi lakini mbona hawa staili yao ya siasa ilikuwa tofauti na hawa masheikh wa miaka hii?

Hakuna popote kwenye historia inapoonyesha Sheikh Hassan bin Amir alitoka mguu mosi mguu pili kwenda kwa Nyerere kumshawishi...nahema...

Bunge la Katiba kasimama Sheikh anasema yeye usiku kucha hakupata usingizi...kisa nini? Anasema Baba wa Taifa katukanwa ghafla akaanza kuangua kilio...huyu sheikh hivi sasa ni "kadhi," wa BAKWATA kapanda cheo. Alikuwa sheikh wa BAKWATA sasa kaongezwa cheo kingine kawa kadhi wa BAKWATA...

Turudi kwa masheikh wa Bagamoyo...mtu yoyote aliyekaribu na masheikh hasa wa vijijini kama Msoga, Msata, Lugoba, utaona hali zao...taaban hali zao ngumu cha kutia mdomoni wanakitafuta.

Masheikh hawa wa Bagamoyo nikiwaangalia kwenye picha...Mashaallah kanzu zinameremeta na wakapata nauli ya kutoka Bagamoyo hadi Monduli na kurudi na masurufu ya njiani na ya kuacha nyuma nyumbani...

2015%2B-%2B1


Kweli masheikh wa BAKWATA wajanja lakini hawa wa Bagamoyo wamewapiku masheikh wa BAKWATA, hawawawezi hawa... hii ni lligi nyingine kabisa...

Kuna msemo mpya vijana wamekujanao kuna masheikh wanaitwa, "Masheikh Ubwabwa."

Watengenezaji filamu wa Hollywood ni hodari kweli kweli wanaweza kukuwekea kitu kinaitwa "set," wakajenga mji wa Bagamoyo kama ulivyokuwa wakati wa Wajerumani na ukahisi khasa hiki ninachoona sasa hivi kwenye senema ndiyo wakati wenyewe miaka 100 iliyopita...hii ya hawa masheikh wa Bagamoyo nadhani mafundi wa Hollywood wakiiona watalia ngoa.

Hii ni zaidi ya uigizaji wa mtu kuchukua "Oscar." Afrika Kusini unaweza kukodi, "waliaji,'' wakaja "kukulia," kwenye msiba wa mama yako.

Bagamoyo Khalifa wa Tariqa Kadiriyya ni mtoto wa Sheikh Mohamed Ramiya, Sheikh Abdulkadir Ramiyya...sidhani kama Sheikh Abdulkadir ana taarifa ya safari hii ya "murid," wake kwenda Monduli... na hii nasema tu maana huenda hawa, "masheikh,'' si Tarika Kadiriyya...

Piga ua lakini Bagamoyo sheikh gani atakuwa si wa Zawiyya ya Sheikh Mohamed Ramiyya?
Kwa ndugu zetu Wakristo "Zawiya," ni sawasawa na "KIgango."

Sasa kweli Mkristo safi anaweza kutoka nje ya Kigango na akasalimika?
Au siku hizi juu ya kuwa na masheikh kutoka Chuo Cha Sanaa Cha Bagamoyo kuna "masheikh mamluki" kuongeza katika "masheikh ubwabwa?

2015%2B-%2B1


Moh%27dSaid_Ramiya_120912_IMG_1367.jpg



Sheikh Abdikadir bin Sheikh Mohamed Ramiyya
Khalifa wa Tariqa Qadiriyya Bagamoyo


2015%2B-%2B1
 
Alhaj Mohamed Said, hao "masheikh" wamepelekwa(naamini si kwa hiari ya mioyo yao) Dodoma.

Ila kwakweli hilo la masheikh ubwabwa linawatambulisha vema kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Hata wewe una haki ya kupeleka mkuu, wametumia haki yao kwa vile wanavyomkubali mshikaji.
 
Mwal JKN (rip) alitutahadharisha kuhusu watu wanaokimbilia Ikulu hususan kwa kutumia kila ghiliba na mbinu pamoja na fedha. Ndugu yetu Lowassa kama ni mbinu basi amezimaliza zote! Hii ya Masheikh wa Bagamoyo imeniacha hoi, shaaban bin taaban!! Mawili yanaweza kutokea: akitokea akaingia Ikulu kila mwananchi ajiandae kuchangia kikubwa ili arejeshe vijisenti anavyotupatupa hovyo. Au akitokea akakosa kuingia basi kuna uwezekano mkubwa bp itapanda sana na kuleta maafa ya kitaifa!!
Tukiacha Masheikh wa Bagamoyo kando, huyu ni mtu wa kuogopa kama ukoma!!!
 
Mimi nimeipenda picha ya tatu kutoka juu kuja chini. Kuna dada kasimama(na hisi ni mwandishi wa habari) yaani ameshika tama na peni yake mkononi' anawatizama hao masheikh waliokaa na muheshimiwa Lowassa na anawasikitikia sana tena sana!! Naomba na nyinyi wanajamvi muingalie hiyo picha tena na muipe maneno.
 
Jamani...Masheikh ubwabwa...hii kali...ebu punguzeni ukali wa maneno...!!!

EL hadi maaskofu watamfuata...subirini...msiwaponde masheikh bure mapema...muwe na akiba ya maneno...!!!
 
Historia imejirudia masheikh wa ile miaka ya hamsini na sitini walimuomba Julius awaongoze kutafuta uhuru wa Tanganyika. Masheikh wa karne ya ishirini na moja wamemuomba Edwardo awaongoze - Hivi hawa hupewa bahasha za kaki au nyeupe. Mara nyingi kanzu maarufu na kuvaliwa kwa wingi ni nyeupe.
 
mohamed said acha wivu wa kike,we kama hujipendekezi kwa wakuu wa nchi hii, kama kimya au endelea kucheza bao huko mtaa wa gerezani,mashehe wenzio yao yana enda.inaitwa "akili kumkichwa".chezeya njaa weyeee:lol::lol:
 
mama weeee wametuwai safar yetu ssi ni jmos,wajasilia Mali 100 kutoka Moshi .nassi tunaenda kumuomba EL agombee,jamaa ni jembe eti( mscm wa mavuno)
 
Mimi nimeipenda picha ya tatu kutoka juu kuja chini. Kuna dada kasimama(na hisi ni mwandishi wa habari) yaani ameshika tama na peni yake mkononi' anawatizama hao masheikh waliokaa na muheshimiwa Lowassa na anawasikitikia sana tena sana!! Naomba na nyinyi wanajamvi muingalie hiyo picha tena na muipe maneno.
ungejua mahesabu ya huyo mwandishi ni EL umuone,hata usingedhani hivyo.waandishi wengi wa tz ni njaa kali,hawana tofauti na hao mashehe ubwabwa.LOL
 
Back
Top Bottom