Kuna jambo linakera sana mtandaoni kuona MTU kwa makusudi anaamua kumtusi Mh Rais Dr john pombe Joseph Magufuli tena anamdhalilisha kwa kumuita majina ya ajabu ajabu mi nadhani ifike wakati waheshimu taasisi ya urais km hawataki kuheshimu taasisi hiyo vyombo vilivyoundwa maalum kwa kazi hiyo kama TISS, Polisi na JWTZ iwashurutishe kwa nguvu kutii taasisi ya urais.
Nasema hivi kwasababu nimesoma maandiko aliyoandika mtu anayeitwa Ben Sanane na nimewaambia ni mfanyakazi wa cdm makao makuu km mkuu wa kitengo cha utafiti na mtu wa karibu sn na Mh Mbowe kiukweli machapisho yake ya Jana naleo mtandaoni inapasa kabisa kumfikisha ktk vyombo vya usalama hasa kile chombo kilichopewa mamlaka kulinda taasisi ya Urais. Tukiacha watu kuchezea taasisi ya urais kuna hatari kubwa taasisi hiyo kutoheshimika milele. Watanzania pamoja na demokrasia ya vyama Vinci kuanzishwa nchini lkn hiyo haitoi nafasi kwa kutusi Mh Rais.
Nimeamua kuandika kwa uchungu kwasababu haya yote yanafanyika wakuu wa wilaya wapo mdogo wangu Ally Salum Hapi dc kinondoni yupo kimya mh rais anadhalilishwa wilayani kwake hajachukua hatua, mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda yuko kimya wakati majeshi yote ya kulida taasisi ya Urais wanayo, cjui wanasubiri mpk Mwigulu Nchemba Waziri wa mambo ya ndani au naibu wake Hamad Masauni ndiyo wachukue hatua?
Jamani ninyi viongozi mliyopewa mamlaka mkishindwa tuachieni sisi vijana wa ccm tufanye kazi hiyo hatuta kubali kuona Rais wetu anadhalilishwa na wahuni. Muda sasa umefika wa kusema no no no.
Tunataka kuona hatua zikichukuliwa haraka iwezekanavyo