Taasisi ya Urais iheshimiwe

Taasisi ya Urais iheshimiwe

Frey Cosseny

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2015
Posts
1,984
Reaction score
1,409
Kuna jambo linakera sana mtandaoni kuona MTU kwa makusudi anaamua kumtusi Mh Rais Dr john pombe Joseph Magufuli tena anamdhalilisha kwa kumuita majina ya ajabu ajabu mi nadhani ifike wakati waheshimu taasisi ya urais km hawataki kuheshimu taasisi hiyo vyombo vilivyoundwa maalum kwa kazi hiyo kama TISS, Polisi na JWTZ iwashurutishe kwa nguvu kutii taasisi ya urais.

Nasema hivi kwasababu nimesoma maandiko aliyoandika mtu anayeitwa Ben Sanane na nimewaambia ni mfanyakazi wa cdm makao makuu km mkuu wa kitengo cha utafiti na mtu wa karibu sn na Mh Mbowe kiukweli machapisho yake ya Jana naleo mtandaoni inapasa kabisa kumfikisha ktk vyombo vya usalama hasa kile chombo kilichopewa mamlaka kulinda taasisi ya Urais. Tukiacha watu kuchezea taasisi ya urais kuna hatari kubwa taasisi hiyo kutoheshimika milele. Watanzania pamoja na demokrasia ya vyama Vingi kuanzishwa nchini lkn hiyo haitoi nafasi kwa kutusi Mh Rais.

Nimeamua kuandika kwa uchungu kwasababu haya yote yanafanyika wakuu wa wilaya wapo mdogo wangu Ally Salum Hapi DC kinondoni yupo kimya mh rais anadhalilishwa wilayani kwake hajachukua hatua, mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda yuko kimya wakati majeshi yote ya kulida taasisi ya Urais wanayo, cjui wanasubiri mpk Mwigulu Nchemba Waziri wa mambo ya ndani au naibu wake Hamad Masauni ndiyo wachukue hatua?

Jamani ninyi viongozi mliyopewa mamlaka mkishindwa tuachieni sisi vijana wa CCM tufanye kazi hiyo hatuta kubali kuona Rais wetu anadhalilishwa . Muda sasa umefika wa kusema no no no.

Tunataka kuona hatua zikichukuliwa haraka iwezekanavyo
 
Jee yeye Rais kauli zake nzuri kwa watu au viongozi wengine? Tuwe wakweli ikiwa muheshimiwa hataki kutukanwa na yeye asitumie lugha za matusi. Ati mleta uzi anasema tuachie sisi ccm tushuhulukie mgeshuhulika wakati wa kampeni pale kariakoo mkizomewa pumbavu kabisa.
 
Kipaumbele cha kwanza ni Kupambana na watu wasio mpenda Mtukufu!! Kwel tufumbe macho tu hii miaka mitano iishe alafu tutajua plan B apo badae maana hii taasisi imeingiliwa!!
 
Jifunze kuandika kwa usanifu kwanza, kisha njoo ulilie vyeo . Kiswahili tu huwezi kuandika unataka ukuu wa wilaya??
 
Ungeleta Post unayosema "Nimemtusi" Rais halafu Ulete na Contents za Hotuba ya Rais kule Pemba na Zanzibar tuone ni nani aliyeidhalilisha hadhi ya Urais kati ya mimi na yeye

Nilidhani ninyi mnaojiita vijana wa CCM mngemtetea kwa hoja badala ya kulilia msaada wa vyombo vya dola.Sidhani pampja na mapungufu yao kama wanaweza kufuata ushauri wa ovyo kama huu

Unatia huruma sana! Pole
 
Kuna Rais ambae nchi hii katukanwa kama Kikwete mpaka watu miaka hiyo walithubutu ku edit picha yake akiwa anajigijigi.

Ni vile tu alikuwa na kitu kinaitwa busara maana aliamini maneno mabaya au matusi hayawezi mdhuru ila yeye alijikita kupiga kazi na si kujishughulisha na mtu/watu tena akaamua aweke uhuru wa vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii ili watu watapike uchafu wote na madini waliomeza mwisho wa siku uchafu aliuacha akachukua madini, hivyo ukitaka kuwafatilia wananchi kila wanachoandika kama kiongozi utaishia kupata vidonda vya tumbo bure maana binadamu tumetofautiana usitegemee wewe ukiwa mstahimilivu wa kutokufunguka yanayokukela na mwenzio atakuwa hivyo.

Kiongozi yoyote inabidi ajikite katika kuleta maendeleo tokana na yale aliyoyaahidi kwa watu wake badala ya kugombana nao,kama uliwaahidi utawasaidia watanzania maskini fanya hivyo siyo unawabana mpaka wananyauka afu wabaki kimya na ukiona mtu anapiga ukelele ujue hali tete
 
Wewe unatakiwa ukamatwe kwa uchochezi maana unamchinganisha Mh. Rais na wapiga kura wake.
Pia nani kakudanganya kazi ya msingi ya jeshi la wananchi ni kutafuta wanaoshambuliana mitandaoni.
 
Kuna jambo linakera sana mtandaoni kuona MTU kwa makusudi anaamua kumtusi Mh Rais Dr john pombe Joseph Magufuli tena anamdhalilisha kwa kumuita majina ya ajabu ajabu mi nadhani ifike wakati waheshimu taasisi ya urais km hawataki kuheshimu taasisi hiyo vyombo vilivyoundwa maalum kwa kazi hiyo kama TISS, Polisi na JWTZ iwashurutishe kwa nguvu kutii taasisi ya urais.

Nasema hivi kwasababu nimesoma maandiko aliyoandika mtu anayeitwa Ben Sanane na nimewaambia ni mfanyakazi wa cdm makao makuu km mkuu wa kitengo cha utafiti na mtu wa karibu sn na Mh Mbowe kiukweli machapisho yake ya Jana naleo mtandaoni inapasa kabisa kumfikisha ktk vyombo vya usalama hasa kile chombo kilichopewa mamlaka kulinda taasisi ya Urais. Tukiacha watu kuchezea taasisi ya urais kuna hatari kubwa taasisi hiyo kutoheshimika milele. Watanzania pamoja na demokrasia ya vyama Vinci kuanzishwa nchini lkn hiyo haitoi nafasi kwa kutusi Mh Rais.

Nimeamua kuandika kwa uchungu kwasababu haya yote yanafanyika wakuu wa wilaya wapo mdogo wangu Ally Salum Hapi dc kinondoni yupo kimya mh rais anadhalilishwa wilayani kwake hajachukua hatua, mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda yuko kimya wakati majeshi yote ya kulida taasisi ya Urais wanayo, cjui wanasubiri mpk Mwigulu Nchemba Waziri wa mambo ya ndani au naibu wake Hamad Masauni ndiyo wachukue hatua?

Jamani ninyi viongozi mliyopewa mamlaka mkishindwa tuachieni sisi vijana wa ccm tufanye kazi hiyo hatuta kubali kuona Rais wetu anadhalilishwa na wahuni. Muda sasa umefika wa kusema no no no.

Tunataka kuona hatua zikichukuliwa haraka iwezekanavyo
km=?
sn=?
Cjui=?
 
Ungeleta Post unayosema "Nimemtusi" Rais halafu Ulete na Contents za Hotuba ya Rais kule Pemba na Zanzibar tuone ni nani aliyeidhalilisha hadhi ya Urais kati ya mimi na yeye

Nilidhani ninyi mnaojiita vijana wa CCM mngemtetea kwa hoja badala ya kulilia msaada wa vyombo vya dola.Sidhani pampja na mapungufu yao kama wanaweza kufuata ushauri wa ovyo kama huu

Unatia huruma sana! Pole
Ben inawezekana una malezi ya kilevi na inawezekana unaandika umelewa lkn ujue taasisi ya Urais ina hadhi yake na inalindwa kisheria Mimi nimewaambia wasipotaka kuulinda hadhi ya taasisi Ya urais kama hawatafanya ivyo sisi wanaccm tutafanya ivyo. Bahati nzuri nishafanya utafiti nakuwafahamuvwalinzi wenu wote na CV yao.
 
Kwanza nikufahamishe hivi tunapoongea taasisi ya uraisi hatumaanishi Magafuli pekeyake, bali taasisi ya uraisi ina watu wengi akiwepo mama Samia na hakuna hata mtu mmoja anayelalamikia Taasisi ya raisi Tanzania bali watu wanamlalamikia Magufuli sio taasisis nzima

Sifa moja ya Raisi ni kuwaunganisha watu, lakini sio kwenye moto na wewe unaweka moto, ni kwa bahati mbaya sana, kwa sasa kuona vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vingeingia kwenye siasa, zamani vilikuwa hivyo kwa kificho lakini sasa vinajionyesha dhairi, watu wanamlalamikia raisi

Sifa nyingine ya Raisi ni kuinua uchumi kwa njia yoyote ile, na wala sio kuua uchumi, nchi moja inaweza kufanikiwa kuinua uchumi wake kwa njia fulani ambayo hiyo njia haitaweza kamwe kuinua uchumi kwenye nchi nyingine, watu wanamlalamikia raisi

Na mengine kadha wa kadha

Watu wana hoja kwa Rais na wala sio taasisi ya uraisi
 
Uhuru wa maoni uheshimiwe
1473049591372.jpg
1473049595321.jpg
 
Back
Top Bottom