Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI): Wagonjwa, ndugu wa wagonjwa na wadau watakaofika MOI watatakiwa kuvaa Barakoa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
FB_IMG_1587035333820.jpg
 
Ni maelekezo mazuri. Na inatakiwa uwe ndio mwongozo wa maeneo yote yanayotoa huduma kwa umma.
 
Kwenda maeneo ya mahospitali saa hizi ni kujitoa muhanga, muhanga wa corona huko Mwanza nasikia sababu anavijihelahela ni mbishi sana, alitoka Dubai baada ya muda akaanza kujisikia hovyo.

Akaenda hospital moja binafsi, wakamuambia mbona ana dalili rafiki na corona akagoma, wakamuachia, kesho yake akarudi ikabidi akamatwe sasa. vipimo kutoka dar vinaonyesha ana corona, nadhani ndio nambari moja kwa Mwanza.

sasa kaishaambukiza wangapi hospitali, na mitaani, at least iko confirmed kaambukiza mke wake ambaye ni nambari mbili kwa mwanza maana ake.

Ni kama anayeitwa nambari moja wa italy, 38 years old lombardian, nae alikuwa mbishi kwelikweli, alienda hospitali mara mbili wanamuambia tupime corona hataki. sasa wote tunajua nini kilitokea pale.
 
Na huo ndio ulitakiwa uwe mwongozo hususan maeneo yaliyoathirika zaidi kama Dar es Salaam. Mtu yeyote in public ni lazima avae barakoa; popote pale. Sio lazima ziwe special, hata vitambaa watu wafunike midomo na pua itasaidia. Badala yake tunajiendea tu!
 
Na huo ndio ulitakiwa uwe mwongozo hususan maeneo yaliyoathirika zaidi kama Dar es Salaam. Mtu yeyote in public ni lazima avae barakoa; popote pale. Sio lazima ziwe special, hata vitambaa watu wafunike midomo na pua itasaidia. Badala yake tunajiendea tu!
Nilivaa kitambaa siku moja nilikuwa in 30minutes.
 
hizo barakoa wmewagawia RAIA ama
... tusitake kila kitu kugawiwa! Kwani nguo ulizovaa umegawiwa na nani kwa mfano? Barakoa ni kifunika mdomo na pua; tafuta kitambaa safi jifunike na hakikisha unabadilisha kila baada ya muda. Kilichotumika kinafuliwa that's all! Chonde chonde Serikali enforce hii kitu; huko kwenye mavituo ya daladala and other congested public areas watu wanapayukapayuka ovyo kitu inayoweza ku-accelerate maambukizi!
 
Kuanzia kesho tarehe 17/04/2020 wagonjwa , ndugu wa wagonjwa na wadau watakaofika Taasisi ya tiba ya mifupa- MOI kupata huduma watatakiwa kuvaa Barakoa (Mask), lengi ikiwa ni kuwakinga na maambukizi ya #CoronaVirus.

#CoronaTanzania #VifoVyaCorona #MaambukiziCorona #CoronaInfection

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuanzia kesho tarehe 17/04/2020 wagonjwa , ndugu wa wagonjwa na wadau watakaofika Taasisi ya tiba ya mifupa- MOI kupata huduma watatakiwa kuvaa Barakoa (Mask), lengi ikiwa ni kuwakinga na maambukizi ya #CoronaVirus.

#CoronaTanzania #VifoVyaCorona #MaambukiziCorona #CoronaInfection

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona serikali mda wote inabadilisha gia angani naa tutaona hatua ngumu mjiandae.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini tuwaeleze uma kwamba barakoa ni njia moja tu ya kijikinga.wanaweza wakadhani ukivaa barokoa basi ndiyo umedhibiti kuambukizwa korona.bahati mbaya ukivaa barakoa unaongeza confidence kiasi unaweza sahau kunawa kuzingatia njia nyingine ambazo nazo ni mhimu zaidi.kwa mfano nilimuona trafiki amevaa barakoa na gloves halafu ameshika mashine ya kuandikia fine.halafu anaongea na simu.halafu simu akaiweka mfukoni mwake.mwingine nilimuoma amevaa gloves halafu ameshika kitabu cha fine.point hapa sijui ni vipi unaweza vitakasa vitu hivyo hapo adaye utakapokuwa umemaliza kazi

Elimu inahitajika kuendelea hasa kwa matumizi sahihi ya barakoa na gloves.sababu unaweza sababisha maambukizi yakazidi
 
Kuna wanasayansi na wataalam wa afya walipinga kabisa uvaaji wa barakoa kwa watu wasioambukizwa!

Walitaka watu waishie kutakasa mikono tu na watembee pua na mdomo wazi na huku wakijua njia kuu ya maambukizi ya gonjwa hili ni hewa inayobeba matone kutoka kwa mwathirika anayepiga chafya au kukohoa! Binafsi sikuwaelewa hata kidogo!
 
Back
Top Bottom