Taasisi ya mikopo (PRIDE) mbioni kufilisika? Mamlaka zinazohusika ziingilie kati

Wakati zzk akiwa mwenyekiti wa PAC aliwahi kusema hivi, "Pride ilikua ni moja kati ya taasisi za umma na hata CAG alikua akikagua hesabu zake, from no where imepotea katika vitabu vya hesabu za mashirika ya UMMA, nini kimetokea!!"
So huwezi jua labda malaika mkuu anataka kuirudisha kwa wamiliki wake halali wa zamani; tusubiri kwanza.
 
Kwanza ziwezi kukopa Pride tena,,mambo ya kupeleka marejesho kila wiki,harafu eti unasimama mbele ya darasa unapoomba mkopo,ajabu kubwa ni pale ambapo mtu mmoja kama hajaleta rejesho basi meki nzima hamtoki mnachanga hadi pesa itimie,,mtu unataka million moja unaambiwa uwe na mali isiyohamishika,mali isiyohamishika ni kiwanja,nyumba na shamba basi.sasa kuna nyumba ya milion moja? Kifupi wale wamefirisika kwa sababu wateja wanakimbia,kwanza kuanza eti ni lazima upewe laki tatu na nusu na si zaidi ya hapo.mkuu achana na mikopo ya vikundi,njoo benki wala hakuna mashariti makubwa kama ya huko.nenda ACCESS BANK/
access bank hapo sasa ukichelewesha rejesho siku moja tu wanakufilisi
 
Kwa mujibu wa ripoti ya CAG pride ni mali ya serikali lakini hesabu zake hazijulikani, Idd simba kama kawaida Nasaco,sukita na sasa pride zinafilisikia mikonoi mwake
 
Kumbe nina jamaa yangu mwanachama namdai sasa ananiambia PRIDE Nasubiri Nasubiri nilimuona muongo tu ananipiga zuluzunga
 
Kwa mujibu wa ripoti ya CAG pride ni mali ya serikali lakini hesabu zake hazijulikani, Idd simba kama kawaida Nasaco,sukita na sasa pride zinafilisikia mikonoi mwake
Watu waliifanya mali yao, wapiga dili nashauri serikali iwafilisi wote
 
Tangu kipindi cha uchaguzi mkuu taasisi hii ilianza kusuasua katika utoaji wa mikopo. Kuna wanachama walioomba mikopo toka mwezi wa nane hadi leo hawajapatiwa mikopo hali iliyopelekea wateja wengi kukosa imani na taasisi hii na karibu 60% wamejifuta uanachama.

Cha ajabu na cha kushangaza hata wale wanaojifuta bado wanasumbuliwa kupewa akiba zao, wengi wao wana miezi 2-3 baada ya kujifuta uanachama ila hawajapewa akiba zao kila siku imekuwa kesho kesho.

Tunaomba mamlaka zinazohusika ziingilie kati ili akiba fedha zetu zisidhurumiwe
Hawajamaa walikuwa wanacheza sana na crdb, sasa ilipotoka 'amri' pesa za mwenyewe zoote ziende Banki Kuu, ikawa imewabana crdb na wao wakawabana Pride.
 
Inamaana ni msimu wa kufilisika kwa taasisi za kifedha au?
Lakini PRIDE inafilisika vipi? Serikali imeondoa fedha zake kweny mabenki, na kufukuzwa wafanyakazi vyeti feki imetikisa mabenki. PRIDE kulikoni? Kuna watu hawajalipa? PRIDE hukopesha wafanyabiashara. Hao wafanyabiashara hawajalipa?
 
Back
Top Bottom