Taasisi ya kuzuiya Rushwa ya Tanzania

Scorpion_004

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
204
125
Taasisi ya kuzuiya Rushwa ya Tanzania
ilianzishwa mnamo tar. 15 Januari ya mwaka wa
1975 , kwa ajili ya kuzuiya rushwa. Taasisi ya
Kuzuia Rushwa (TAKURU) ni taasisi ya serikali
iliyopewa jukumu la kupambana na rushwa. Ni
idara inayojitegemea ambayo ipo chini ya Ofisi
ya Rais. Makao Makuu ya Taasisi ya Kuzuia
Rushwa. Ipo eneo la upanga magharibi kwenye
makutano ya barabara ya kalenga na Urambo Dar
es Salaam. Kwa sasa Taasisi hii inajulikana kama
TAKUKURU (Taasisi ya kuzuiya na Kupamban na
Rushwa)[ [1] ]
Historia
Kabla ya mwaka wa 1975 shughuli za kuzuia
rushwa zilifanywa na Wizara ya Mambo ya Ndani,
ambapo jeshi la polisi lilipewa jukumu zima la
kupambana na rushwa. Taasisi ya Kuzuia
Rushwa iliundwa na Sheria namba 2 ya mwaka
1974 ambayo ilipitisha kuundwa kwa Kikosi cha
Kuzuia Rushwa, baada ya kuifanyia marekebisho
Sheria ya Kuzuia Rushwa Namba 16 ya mwaka
1971 . Kikosi cha Kuzuia Rushwa kilianzishwa
rasmi tarehe 15 Januari 1975 kwa tamko la
Serikali Namba 17 la 1975,
Swali ambalo naomba mnisaidie kwa wale wanaofamu kuhusu mafunzo ,wanafanyia wapi?
Pia naomba kujua utaratibu wa kuajiri ulikuwaje hapo nyuma,kwa wale wajuzi wa mambo naomba kujua mengi kuhusu pccb.
 
Back
Top Bottom