Taasisi ya Boys Initiave yatoa elimu maalum ikiwemo afya ya akili kwa wanafunzi wa kiume

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Taasisi isiyo ya Kiserikali ya 'Boys Initiave' imetoa elimu maalum ikiwemo afya ya akili kwa wanafunzi wa kiume katika shule ya Sekondari ya ALFA iliyoko Mikocheni, Kinondoni Jijini Dar es Salaam,

Akizungumzia elimu hiyo Mkurugezi Mtendaji wa taasisi hiyo, Dayana Rose Alfred Rweyemamu amesema kuwa elimu hiyo inalenga kuwaleta karibu wanaume kutambua kuwa na ni sehemu ya wao kutambua haki zao kama inavyofanywa zaidi na kwa wanawake ambao wemekuwa wakipewa kipaombele.

Ameleza kuwa elimu hiyo imejikita katika kuwapatia ujuzi watoto wa kiume katika kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo elimu ya afya ya akili na namna ya kukua katika maadili bora.

"Tunatoa elimu hii kwakuwa kundi ili tunaweza kujikuta tunaliacha nyuma tukiamini lipo salama, leo tumetoa elimu ya afya ya akili pamoja na elimu ya kuwawezesha watoto wa kiume kukabiliana na changamoto mbalimbali, tusipokuwa makini kuelimisha mtoto wa kiume tutajikuta siku moja tunapoteza Baba bora" amesema Mkurugezi huyo

Aidha Mwl. Fulgence Kabiligi, ambaye ni Mratibu wa mtaala wa ziada kwenye shule ya Sekondari ALFA amesema kuwa elimu hiyo inaongeza chachu ya kufanya watoto wa kiume wasiachwe nyuma.

"Wapo watoto wa kiume tunaona ujasiri wao unazidi kushuka hii inaweza kutokana na kukosa hamasa lakini tunaona watoto wa kike wanakuja kasi, hivyo hii elimu itasaidia kuleta hamasa maana hatutakiwi kuwaacha nyuma madhara yake ni makubwa." amesema mwalimu huyo.

Kwa upande wa wawasilisha mada, Magolange Shagembe ambaye Muhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais wa Chama cha Wanasaikolojia Tanzania, amesema kuwa elimu ya afya ya akili ni sehemu ya kuwawezesha watoto wa kiume na wakike kukabiliana na changamoto, ameshauri kuwa watoto wa kiume wasiachwe nyuma katika kunufainka na programu mbalimbali ambazo uwezesha upatikanaji wa elimu na ujuzi.

Hata hivyo imeelezwa kuwa elimu hiyo itakuwa endelevu katika shule nyingine Jijini Dar es Salaam, hususani Wilaya ya Kinondoni ambayo hipo katika mkakati wa awali.
 
Back
Top Bottom