Taasisi karibia zote zi ajiri kupitia Utumishi

Mwana Ukoo

JF-Expert Member
Nov 21, 2016
253
500
Wakuu Moja ya mifumo imara ni huu wa Secretariat ya Ajira utumishi, Huu mfumo Utaleta Uimara mkubwa katika Taasisi za umma ambalo mwazo ilikuwa shamba la bibi yani ofisi unakuta imejaa ndugu tupu, Au watu wa ukanda fuĺani tu matokeo yake ufanisi hupungua sana na kufanya ofisi za umma kuwa kijiwe cha kupigia tu mana hakuna wa kumkemea mwezie watu wanapiga deal Sana kwa vile tu Chain inayozunguka yote mtu anaijua na pengine huyo mpiga dili ndo amefanya wao wakapata kazi hata kama wapo juu yake hawana cha kumfanya.

Nashauri taasisi ambazo ziko under performance zote zipelekewe watumishi kutoka utumishi waondolewa ile power ya kuajiri wao kama wao kuna taasisi kama Tanzania Revenue Authority TRA hii tayari ipo Utumishi japo ilichelewa Tanesco ivo hata Majeshi nayo kama Police yapelekewe watumishi kutokea portal yani polisi yeye atoe tu requirements kama urefu sijui mtu asiwe na Criminals records then utumishi ndo wamalize mchezo, Hakika matunda ya huu mfumo yataanza kuonekana Siku za usoni mana undugu maofisi unapungua na hata heshima inarudi mana watu hawajuani nani ni nani mana mtu katoka tu from nowhere na kuja kureport

Nimefanya kazi Kampuni za nje kwa kweli nimejifunza kuwa ni u smart wako tu ndio utakupa ajira hakuna cha mtoto wa mjomba wala mtoto wa baba mdogo
 
C.T.U

JF-Expert Member
Jun 1, 2011
4,972
2,000
Kwenye majeshi sikubaliani na wewe kwa sababu mfumo wa utumishi hauna vetting ya kutosha

Ukifanya hivyo utashangaa Mr Slim akapenyeza watu wake mwisho wa siku ukajikuta una IGP, CDF kutoka kwa Mr Slim
 
Mwana Ukoo

JF-Expert Member
Nov 21, 2016
253
500
Kwenye majeshi sikubaliani na wewe kwa sababu mfumo wa utumishi hauna vetting ya kutosha

Ukifanya hivyo utashangaa Mr Slim akapenyeza watu wake mwisho wa siku ukajikuta una IGP, CDF kutoka kwa Mr Slim
Mkuu kwani kwa sasa recruitment ya vyombo vya dola ikoje? Mimi ni mtoto wa Askari na utaratibu wa kuingia uaskari kipaumbele huwa ni watoto wa maskari nimeliona ilo kwa muda, kuna post ambazo zinaweza kuwa excluded utumishi ila hawa wanaoenda depo wapite utumishi tu
 
MCHEZA KAMARI

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
1,607

Mbona naskia ni lazma upite jkt Kwanza kabla ya kujiunga na jesh lolote zama hizi au unaongelea zama za kale?
 
road master

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
560
1,000
Aisee una akili sana ,hili mm nililiona kitambo sana!!! Mashirika yooooote ya uma mfano tpa ,tanesco,tanapa,posta nk ni vyema yafanye hivyo ili kiondoa
1) upendeleo
2) kugushi vyeti
3) kuongeza ufanisi
 
Mwana Ukoo

JF-Expert Member
Nov 21, 2016
253
500
Mbona naskia ni lazma upite jkt Kwanza kabla ya kujiunga na jesh lolote zama hizi au unaongelea zama za kale?
Utafutwe utaratibu tu mkuu hata hao wanopita JKT ni wanabebana sana sana kiasi kwamba taasisi inakuwa underperformance kwa vile tu waajiliwa wamebebwa na mbeleko na hawako competent hata kama wanazo qualifications
 
MCHEZA KAMARI

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
1,607
2,000
Utafutwe utaratibu tu mkuu hata hao wanopita JKT ni wanabebana sana sana kiasi kwamba taasisi inakuwa underperformance kwa vile tu waajiliwa wamebebwa na mbeleko na hawako competent hata kama wanazo qualifications
Kweny majesh utasaidiwa kuingia tu ila kma huna moyo utatoroka kabla mafunzo hayajaisha wote mnapitia mafunzo sawa hata mtt wa CDF lazma aumie , ukiona mtu kamaliza na kavaa unform zake ujue kastahil kuwa hapo
 
GKado

JF-Expert Member
Oct 7, 2017
556
1,000
Baada ya kuona mfumo wa utumishi unataka kuchukua fursa za waliojazana kwenye mashirika ya umma.​
Wakubwa wameona isiwe tabu wamebadili mfumo wanaajiri kwa mikataba ambayo ni renewable.​
Utumishi wao wamebase kwenye kazi ambazo ni permanent and pensionable.​
Mashirika yakapiga chenga kwa kuajiri kwa contact tu wanatangaza kazi wanajaza ndugu watakuwa wanarenew tu mkataba akipewa miaka miwili ukikaribia kuisha anaongezewa mitatu maisha yanaendelea na wanavuna miposho ya kutosha.​
Haya maisha acha tu bila connection utasugua benchi kusubiri zitangazwe utumishi na hutasikia mfano mashirika Kama NSSSF, EWURA,LATRA,TANROADS,TPDC, TARURA etc....​
 
Underdog

JF-Expert Member
Apr 14, 2014
301
500
Ni kweli Utumishi ingekuwa ni daraja zuri sana la kuingiza watu kwenye taasisi za umma kama michakato yake ya uajiri ingekuwa wazi na yakueleweka na pia mamlaka yake ingeheshimiwa na kutiiwa na taasisi za umma.

Yafuatayo ni mojawapo ya mambo yanayochanganya kuhusu mfumo wao wa uajiri.

1. Pass mark ya kwenda kwenye usaili wa mahojiano ni ngapi.

2. Uwiano upoje kati ya idadi za nafasi zinazohitajika kujazwa na idadi ya watu wanaotakiwa kuitwa kwenye usaili wa mahojiano. Unakuta wakati mwingine nafasi ni moja ila wanaitwa watu 27 kwenda kwenye usahili wa mahojiano, lakini wakati huo huo unakuta nafasi ni tano lakini wanaitwa watu 10 kwenda kwenye usahili wa mahojiano.

3. Je ni vitu gani vinazingatiwa kwenye usahili wa mahojiano ambavyo vitamfanya mtu apate nafasi ya ajira. Je, ni idadi ya maswali aliyoyajibu vizuri, uwezo wa kujieleza, GPA, uzoefu wake wa kazi au ni kitu gani.

4. Tunaambiwa huwa wanachukua watu wanawaweka kwenye database, vigezo vya kuwekwa kwenye database ni zipi, na je, ni nafasi zipi au taasisi ipi ambazo zinachukua walio kwenye database na ni zipi hazichukui na kwanini. Nauuliza maswali haya sababu unaweza kuta tuseme wiki hii Utumishi imewaita tuseme Wahandisi wa Ujenzi 20 kwenye usahili wa mahojiano ili apatikane mtu mmoja wa kujaza nafasi husika, mtu anapatikana. Lakini baada ya wiki tatu tena unaona utumishi labda wanatangaza tena nafasi moja ya Muhandisi wa Ujenzi kwenye taasisi nyingine, sasa unajiuliza kwenye wale 19 waliobaki kwenye ile usaili uliopita inamaana hakuna aliye kwenye database, kwanini wasimpe hiyo nafasi mtu mmoja kati ya hao.

5. Kuna wakati watu fulani walimfuata Katibu wa Utumishi (kwa mambo tofauti kidogo) , katika maongezi yao Katibu akawaambia huwa wanapata shida kutoka kwa Mashirika fulani, alitaja TPA, TRC na Tanesco kuwa unakuta wametangaza nafasi za kazi kupitia Utumishi,mchakato wote unafuatwa na waliofuzu kujaza wanapatikana ila hayo Mashirika unakuta yanataka kuwachomeka watu wao wengine tofauti na hao waliopatikana kupitia Utumishi. Hapa ndo suala la nguvu na mamlaka yao linaleta sintofahamu.

6. Kingine suala la ufuatiliaji wa mashirika yanayohitaji watu, kama Utumishi mshafanyia watu mahojiano na kuwapata kwa idadi iliyotakiwa na shirika fulani na mnawapelekea majina. Sina uhakika kama wanafuatilia kama watu hao wanachukuliwa kulingana na idadi iliyoombwa na shirika lenyewe. Mfano TRC ilikuwa inahitaji Mechanical Engineers II kumi na mbili, utumishi ikafanya michakato yake ikapata watu, pamoja na ukinzani wa TRC kutaka kupachika watu wao tofauti lakini walishindwa nadhani maagizo yalitoka juu. Katika hao 12 waliripoti 11 mmoja hakuja ikabidi TRC tena wamchukue mtu mwingine kutoka kwenye ile list ya utumishi (list ilikuwa na watu 43 waliofanya usaihili wa oral, imeorodhesha majina kulingana na ufaulu), huyo aliyechaguliwa na TRC kutoka kwenye list naye hakwenda. Baadaye tena katika wale 11 walioripoti mmoja akaacha kwa hiyo wakabaki 10, tafsiri yake kuna nafasi mbili ambazo hazijajazwa katika zile walizotangaza TRC, na list ya majina 43 waliofanya usaili wa mahojiano wanayo. Sasa unajiuliza walishindwa nini kuchukua tena hao watu wawili kutoka kwenye list. Tutajuaje kama hao si ndiyo watumishi hewa wenyewe? Leo ni karibia miaka miwili sasa hawajawachukua hao watu ili kujaza zile nafasi mbili. Sasa unajiuliza nafasi ya Utumishi hapa ikoje, ndiyo tunajua kuna Wakaguzi wa ndani na pia CAG yupo angeweza ku raise quiry kuhusu hilo, lakini vipi Utumishi wao nafasi yao ikoje kwenye kudhibiti mambo kama hayo ambayo yanaweza pelekea kuwa na watumishi hewa?

Kiukweli maswali ni mengi sana.
 
Underdog

JF-Expert Member
Apr 14, 2014
301
500
Ni kweli Utumishi ingekuwa ni daraja zuri sana la kuingiza watu kwenye taasisi za umma kama michakato yake ya uajiri ingekuwa wazi na yakueleweka na pia mamlaka yake ingeheshimiwa na kutiiwa na taasisi za umma.

Yafuatayo ni mojawapo ya mambo yanayochanganya kuhusu mfumo wao wa uajiri.

1. Pass mark ya kwenda kwenye usaili wa mahojiano ni ngapi.

2. Uwiano upoje kati ya idadi za nafasi zinazohitajika kujazwa na idadi ya watu wanaotakiwa kuitwa kwenye usaili wa mahojiano. Unakuta wakati mwingine nafasi ni moja ila wanaitwa watu 27 kwenda kwenye usahili wa mahojiano, lakini wakati huo huo unakuta nafasi ni tano lakini wanaitwa watu 10 kwenda kwenye usahili wa mahojiano.

3. Je ni vitu gani vinazingatiwa kwenye usahili wa mahojiano ambavyo vitamfanya mtu apate nafasi ya ajira. Je, ni idadi ya maswali aliyoyajibu vizuri, uwezo wa kujieleza, GPA, uzoefu wake wa kazi au ni kitu gani.

4. Tunaambiwa huwa wanachukua watu wanawaweka kwenye database, vigezo vya kuwekwa kwenye database ni zipi, na je, ni nafasi zipi au taasisi ipi ambazo zinachukua walio kwenye database na ni zipi hazichukui na kwanini. Nauuliza maswali haya sababu unaweza kuta tuseme wiki hii Utumishi imewaita tuseme Wahandisi wa Ujenzi 20 kwenye usahili wa mahojiano ili apatikane mtu mmoja wa kujaza nafasi husika, mtu anapatikana. Lakini baada ya wiki tatu tena unaona utumishi labda wanatangaza tena nafasi moja ya Muhandisi wa Ujenzi kwenye taasisi nyingine, sasa unajiuliza kwenye wale 19 waliobaki kwenye ile usaili uliopita inamaana hakuna aliye kwenye database, kwanini wasimpe hiyo nafasi mtu mmoja kati ya hao.

5. Kuna wakati watu fulani walimfuata Katibu wa Utumishi (kwa mambo tofauti kidogo) , katika maongezi yao Katibu akawaambia huwa wanapata shida kutoka kwa Mashirika fulani, alitaja TPA, TRC na Tanesco kuwa unakuta wametangaza nafasi za kazi kupitia Utumishi,mchakato wote unafuatwa na waliofuzu kujaza wanapatikana ila hayo Mashirika unakuta yanataka kuwachomeka watu wao wengine tofauti na hao waliopatikana kupitia Utumishi. Hapa ndo suala la nguvu na mamlaka yao linaleta sintofahamu.

6. Kingine suala la ufuatiliaji wa mashirika yanayohitaji watu, kama Utumishi mshafanyia watu mahojiano na kuwapata kwa idadi iliyotakiwa na shirika fulani na mnawapelekea majina. Sina uhakika kama wanafuatilia kama watu hao wanachukuliwa kulingana na idadi iliyoombwa na shirika lenyewe. Mfano TRC ilikuwa inahitaji Mechanical Engineers II kumi, utumishi ikafanya michakato yake ikapata watu, pamoja na ukinzani wa TRC kutaka kupachika watu wao tofauti lakini walishindwa nadhani maagizo yalitoka juu. Katika hao 10 waliripoti 9 mmoja hakuja ikabidi TRC tena wamchukue mtu mwingine kutoka kwenye ile list ya utumishi (list ilikuwa na watu 43 waliofanya usaihili wa oral, imeorodhesha majina kulingana na ufaulu), huyo aliyechaguliwa na TRC kutoka kwenye list naye hakwenda. Baadaye tena katika wale 9 walioripoti mmoja akaacha kwa hiyo wakabaki 8, tafsiri yake kuna nafasi mbili ambazo hazijajazwa katika zile walizotangaza TRC, na list ya majina 43 waliofanya usaili wa mahojiano wanayo. Sasa unajiuliza walishindwa nini kuchukua tena hao watu wawili kutoka kwenye list. Tutajuaje kama hao si ndiyo watumishi hewa wenyewe? Leo ni karibia miaka miwili sasa hawajawachukua hao watu ili kujaza zile nafasi mbili. Sasa unajiuliza nafasi ya Utumishi hapa ikoje, ndiyo tunajua kuna Wakaguzi wa ndani na pia CAG yupo angeweza ku raise quiry kuhusu hilo, lakini vipi Utumishi wao nafasi yao ikoje kwenye kudhibiti mambo kama hayo ambayo yanaweza pelekea kuwa na watumishi hewa?

Kiukweli maswali ni mengi sana.
Jambo lingine ni ile mitihani ya mchujo,ni nani anayetunga ile mitihani? Je, ni taasisi husika inayohitaji watu au ni Utumishi wenyewe?Wamejiridhisha kiasi gani kwamba aina ile ya mitihani inachuja vizuri (inatoa nafasi kwa yule mtu bora na kumchuja yule ambaye si bora kivile), isije ikawa ni elimradi tu inapunguza watu bila kujali ubora wao.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom