Mtunza siri zako
JF-Expert Member
- Apr 11, 2025
- 586
- 975
Watu wengi tunafurahia kujadiliwa kwa kesi ya Tundu Lissu Bunge la Ulaya, binafsi nafikiri ni hatua nzuri kwa ajili ya check and balance za uwajibikaji wa Serikali.
Ila taarifa hii kwa namna ilivyowasilishwa si kweli na imepotoshwa (nikimaanisha sehemu ya yale yaliyoripotiwa ni kweli na mengine ni uongo).
Bunge la Ulaya kufanya kikao cha dharura Mei 7, 2025 - SI KWELI, hakuna kikao cha dharura.
Bunge la Ulaya linafanya kikao cha kawaida kulingana na ratiba zake za plenary. Zaidi ya Hoja 20 na mapendekezo yanajadiliwa leo ikijumuisha Kesi ya Tundu Lissu ambayo itawasilishwa na wabunge watano wa bunge la ulaya kwa dakika takribani 20 (na si masaa nane kama ilivyoelezwa na media nyingi).
Hii si hoja ya dharura (urgent debate) bali ni resolution yenye mapendekezo kama yalivyoonyeshwa kwa kirefu hapa MOTION FOR A RESOLUTION Arrest and risk of execution of Tundu Lissu, Chair of Chadema, the main opposition party in Tanzania | B10-0260/2025 | European Parliament
Na itasomwa na wabunge wachangiaji kama walivyoorodheshwa kwenye ratiba ➡️ Home | Plenary | European Parliament
Hii habari imegusa hisia za wengi na kuwafikia maelfu ya watanzania kupitia watu mashuhuri na vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Millard Ayo, Mwananchi media, na majukwaa kama Jamii Forum na sehemu nyingine nyingi. Nadhani habari ilianzia mitandaoni na vyombo vya habari vikaichukua na kuiripoti bila kuhakiki ukweli wake.
Humu JF naona mijadala mingi na imechukua sana hisia za watu wakiamini kwamba bunge la Ulaya limeitisha kikao maalum cha dharura kwa ajili ya Tanzania, kitu ambacho si kweli. Ni muhimu tujifunze kufact check mambo yanayoletwa mitandaoni ikijumuisha yale yanayoandikwa na online media.
Nimetumia huu mfano kwa sababu ni habari recent ambayo ni ya moto kwa sasa, ila kuna mifano mingine mingi ambayo habari ya uongo au iliyopotoshwa inaenea na kuaminika. Karibu uongeze ya kwako ambayo unaifahamu.