Huyo mwendesha mashtaka ana mapepo? Daudi Mwangosi amekufa mikononi mwa askari-zaidi ya mmoja. Kabla ya kulipuliwa na bomu alipigwa vibaya na hao askari. Sasa kwa nini ni askari mmoja tu amechukuliwa hatua? Vipi wale walioshiriki kumpiga (bodily harm)? Na RPC yuko wapi maana ndiye aliyeruhusu haya yote yatendeke, tena mbele ya macho yake? Where is he? Pia ningetaka kujua huyo askari ni wa kituo gani? anatoka mkoa wa Iringa? kama jibu siyo alikuja hapo kwa amri ya nani na kwa nini?
Mambo mengine:
1. Barua ya waziri inakiri kuwa Daudi aliuliwa na bomu la machozi, sasa, ni lini msemaji wa jeshi la polisi atatoa apology kwa kusema kuwa marehemu aliuliwa na kitu kizito? when?
2. Vifaa vya kazi vya marehemu (camera na laptop) viko wapi? Kwanini haviongelewi hivi vitu?
3. Ni lini serikali itaenda kumuona mjane na kumpa formal apology maana sasa waziri anakiri kuwa Daudi aliuliwa na bomu la machozi la polisi?