Taarifa ya CUF kuhusu hali ya Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa ya CUF kuhusu hali ya Zanzibar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by EMT, May 29, 2012.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,442
  Likes Received: 687
  Trophy Points: 280
  Umma unashuhudia hali tete ya machafuko ambayo hayakutarajiwa yakiibukia tena Zanzibar, wakati ambapo Nchi ilishaanza kunawiri matunda ya utulivu na maridhiano, chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

  Pamoja na sababu au visingizio mbali mbali vilivyotajwa kuwa chanzo cha hali hiyo, zikiwamo za hamasa za wananchi, chuki binafsi, ukosefu wa hikma, matumizi ya nguvu za dola, na hata uchochezi wa makusudi wa wale wanaoonekana kutopendelea Maridhiano ya Kisiasa ya Zanzibar.

  Kwa thamani yoyote hakuna asiyeweza kubaini umuhimu wa hali ya amani na utulivu, na madhara ya kukosekana kwake, hasa katika Visiwa hivi vya Unguja na Pemba ambavyo vimewahi kuelemezewa athari kubwa ya machafuko kwa muda mrefu.

  Chama cha Wananchi,CUF, kama sehemu muhimu ya Umma wa Watanzania, hakiwezi kukaa kimya kutokana na mwelekeo mzima wa hali tete ya amani katika nchi, ingawa ni dhahiri wapo baadhi ya watu wasioitakia mema Zanzibar wakibainika kufurahia mazingira hayo, kwa maslahi binafsi, na pia kutoa kauli za kutatanisha za kisiasa.

  Chama cha CUF, kinatoa wito kwa wananchi wote kuwa watulivu, wavumilivu, na kuitumia fursa ya kutoa mawazo yao bila ya jazba, pamoja na kutowanyima wengine nafasi ya kuwasilisha mitazamo yao.

  Vitendo vya watu wachache kuchoma makanisa na kuharibu mali za watu ni vya uvunjifu wa sheria na kinyume na Utamaduni wa Kizanzibari; uchunguzi wa kina ufanyike na waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria, bila uonevu wala upendeleo.

  Tahadhari iwepo ya kuepuka matumizi ya mabavu yanayoweza kuleta hamasa kwa wananchi, hatimaye ikachochea vitendo vya hujuma dhidi ya watu na mali zao, na pia kuepuka tabia isiyokuwa ya haki, ya kuwabambikizia kesi wananchi.

  Ni lazima kwa wakati huu, na haraka iwezekanavyo, Serikali ikazungumza na Masheikh, bila ya kuona muhali, na kwa uwazi kabisa, ili kutafuta suluhu ya kudumu, kwa faida ya Nchi na Taifa kwa Ujumla.

  HAKI SAWA KWA WOTE

  …………………………………….
  Salim A Bimani

  Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu, Habari na
  Uenezi na Mahusiano na Umma
   
 2. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,767
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Asanteni wana CUF kwa taarifa.
   
 3. T

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,747
  Likes Received: 516
  Trophy Points: 280
  Asante Bimani kwa kutambua watu wenye ushawishi ZNZ
   
 4. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 5,923
  Likes Received: 1,703
  Trophy Points: 280
  Wazanzibar ni watu wakarimu sana, Tatizo nadhani ni hao uamsho wanao Taka damu imwagike Zanzibar kwa maslahi yao
   
 5. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kauli za baadhi ya viongozi wenu ndio moja kati ya sababu Kubwa ya haya yanayotokea Leo hii Zanzibar.....Mfano hai ni Jusa na Kauli yake ile baada ya kushindwa Jimbo la Uzini (Ubara na Ukafir). Hakika lazima nafsi ziwasute katika hili.
   
 6. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,052
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  I think sheria kali zichukuliwe na ili iwe fundisho kwa baadae tubadili hizi sheria nyingine ili swala la fujo zozote za kidini liwe na adhabu kali sana!
   
 7. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wazanzibari na makatili na roho mbaya kuliko wote duniani
   
 8. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #8
  May 29, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,937
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  mkuu kwani uamsho sio wazanzibari?
   
 9. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #9
  May 29, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Asante CUF kwa kutoa tamko. ingawa wakati mwingine kutoa tamko kunaweza kuonyesha welevu ama ujinga wa mtu. Kiini cha tatizo la wazanzibari, ni Mkuu wa kaya, bunge pamoja na wabunge wote ambao kwa pamoja walipitisha sheria gandamizi ya kuzuia watu kutoa maoni yao wakati wa mchakato wa katiba. KIPEKEE, NAPENDA KUWAPONGEZA WABUNGE WOTE WALIOTOKA NJE YA BUNGE WAKATI SHERIA HII GANDAMIZI INAPITISHWA. Hakuna namna ya jinsi watakavyo kwepa kubeba dhamana wale wote waliokubali kwa pamoja kupitisha sheria ya kuzuia watu wasijadili muungano wakati muungano ni sehemu kubwa ya Katiba.
  Matokeo ya kuziba watu midomo wasiseme kwa maneno ni kusema kwa vitendo. Hii ndiyo sababu kubwa ya yote yanayotokea zanzibari.
  siwalaumu wazanzibari, siwalaumu waisilamu, wala sitalaumu UAMUSHO, bali lawama zangu ziende kwa mkuu wa kaya pamoja na wabunge wote walioshiriki kupitisha sheria gandamizi. Nawashukuru wabunge wote walio toka nje ya bunge kupinga sheria hii.
  Kwa kuwa hakuna anayependa kuona machafuko, Lawama sasa hivi hazina msaada wala nafasi, napenda kumwomba Mkuu wa kaya, kwa busara zake, atoe nafasi kwa bunge lake tukufu, kikao cha kwanza, cha mwezi ujao, kiondoe sheria hii gandamizi, kiruhusu Muungano ujadiliwe, na mawazo ya wananchi yapewe nafasi.
  "MUNGU IBARIKI TANGANYIKA, MUNGU IBARIKI ZANZIBARI, RIP TANZANIA"
   
 10. m

  mtume pauli Member

  #10
  May 29, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  zanzibar ikijitenga haitatawalika. nawaonea huruma watanganyika waliowekeza zanzibar.
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  May 29, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,441
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu hadi sasa hivi nashindwa kabisa kuelewa hili swala la kuujadili Muungano. kinachotakiwa kujadili ni nini hasa?.. kuwepo kwa Muungano au kero zilizozopo ndani ya Muungano.
  Maana nijuavyo mimi hawa UAMSHO wasichokitaka ni MUUNGANO kwa sababu wanadai ni batil na kifupi haukuwa halali kwani wananchi hawakuhusishwa na kadhalika.

  Nachpenda kuuliza miye ni kwamba ni muungano gani wa nchi mbili kuunda moja ambao umehusisha wananchi? hivi kweli wewe unaweza kuuliza hati ya ndoa ya wazazi wako ili kuhalalisha kuzaliwa kwako? na hata kama wakikupa itaondoa karaha za kero za mateso unayopewa n mzazi wako kwa fikra na imani kwamba mzazi wako hawezi kukutendea mabaya!

  Ni muhimu sana kufikiria nje ya box la Uzanzibar kwa sababu kuna Wazanzibara wengi kuliko kundi dogo sana la walalahoi ambao wanafikiria zaidi mkono unaoingia kinywani. Msityaombee yaliyotokea Sudan na yanaendelea kuwakwaza hata pale walipofikiria wamemaliza matatizo yao kumbe ndio kwanza wamewasha moto mwingine. Muungano sii swala la ardhi hata kidogo bali unganisho wa WATU wake na umaskini wa Zanzibar unatengenezwa na viongozi wetu wenyewe kama ilivyo bara na maskini wengine nchi nyinginezo. Uhuru, haki na usawa haupiganiwi kwa kutazama matabaka ya uzawa ama dini bali kile unachoamini ni haki ya kuishi kwa kila binadamu iwe mkristu au muislaam.
   
 12. A

  Albimany JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45

  Mkuu umejitahidi kujenga hoja ila inaonekana hujui kua huu muungano sio wa nchi mbili kuunda moja bali ni muungano wa baadhi ya mambo machache ndani ya mambo mengi yahusuyo nchi.
   
 13. kamonga

  kamonga Senior Member

  #13
  May 29, 2012
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 170
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Natamani nimuone huyu ndugu Bimani nataka nimwambie kua hakuanza leo WALIANZA NA KUCHOMA BAA MKAWABARIKI KWA KUKAA KIMYA!!! NA SASA MAKANISA!!! wanasema ni kikundi cha watu which is obvious hawaweza tosha wazanzibari wote kufanya ni kundi la watu mliowabariki kwa kukaa kimya tangu mwanzo....I am very angry veryyyy angry!!!
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  May 29, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 33,789
  Likes Received: 8,361
  Trophy Points: 280
  Boko Haram tayari imeshatuwa Zanzibar na hakuna namna yoyote ile ya Masheikh kutohusika na hujuma hizi.
   
 15. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #15
  May 29, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,580
  Likes Received: 1,329
  Trophy Points: 280
  kwani uamsho sio wazanzibar?
   
 16. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #16
  May 29, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kwani hao uamsho sio wazanzibar????
   
 17. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #17
  May 29, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 7,496
  Likes Received: 353
  Trophy Points: 180
  nashukuru kwani CUF imejibu ombi langu la jana...kutoa tamko juu ya machafuko ya zanzibar.
   
 18. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #18
  May 29, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Hii ni kweli mkuu.
   
 19. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #19
  May 29, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Hii ni kweli mkuu.
   
 20. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #20
  May 29, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,395
  Likes Received: 1,550
  Trophy Points: 280
  Post yangu ya kwanza ngoja niendelee kuwasona
   
Loading...