Taarifa ya CUF kuhusu hali ya Zanzibar

HAKI SAWA KWA WOTE

…………………………………….
Salim A Bimani

Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu, Habari na
Uenezi na Mahusiano na Umma

Huyu Mkurugenzi kabebeshwa majukumu mengi na kibaya zaidi majukumu yenyewe hayaingiliani. Haki za Binadamu na Uenezi?! Lipumba hapa mmechemsha.

TUMBIRI (PhD, Hull University - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Mkuu wangu hadi sasa hivi nashindwa kabisa kuelewa hili swala la kuujadili Muungano. kinachotakiwa kujadili ni nini hasa?.. kuwepo kwa Muungano au kero zilizozopo ndani ya Muungano.
Maana nijuavyo mimi hawa UAMSHO wasichokitaka ni MUUNGANO kwa sababu wanadai ni batil na kifupi haukuwa halali kwani wananchi hawakuhusishwa na kadhalika.

Nachpenda kuuliza miye ni kwamba ni muungano gani wa nchi mbili kuunda moja ambao umehusisha wananchi? hivi kweli wewe unaweza kuuliza hati ya ndoa ya wazazi wako ili kuhalalisha kuzaliwa kwako? na hata kama wakikupa itaondoa karaha za kero za mateso unayopewa n mzazi wako kwa fikra na imani kwamba mzazi wako hawezi kukutendea mabaya!

Ni muhimu sana kufikiria nje ya box la Uzanzibar kwa sababu kuna Wazanzibara wengi kuliko kundi dogo sana la walalahoi ambao wanafikiria zaidi mkono unaoingia kinywani. Msityaombee yaliyotokea Sudan na yanaendelea kuwakwaza hata pale walipofikiria wamemaliza matatizo yao kumbe ndio kwanza wamewasha moto mwingine. Muungano sii swala la ardhi hata kidogo bali unganisho wa WATU wake na umaskini wa Zanzibar unatengenezwa na viongozi wetu wenyewe kama ilivyo bara na maskini wengine nchi nyinginezo. Uhuru, haki na usawa haupiganiwi kwa kutazama matabaka ya uzawa ama dini bali kile unachoamini ni haki ya kuishi kwa kila binadamu iwe mkristu au muislaam.

Mkuu Mkandara.

Niseme kuwa nimependa hoja ya kuwa umaskini wa Tanzania unatengenezwa na unalelewa na watawala wa serikali za Tanzania. Hoja hii naiunga mkono.

Halafu mkuu kwa nini unapenda kufananisha Muungano wa nchi na wazazi, baba/mama?

Kwa maoni yangu, Muungano ujadiliwe katika upana wake, uwepo au usiwepo? Kama uwepo wa aina ipi kuendana na mazingira ya leo? serikali ngapi ziwepo? Mgawanyo/mipaka inayoeleweka kimadaraka.

Mkuu hoja ya kuwa Tanganyika na Zanzibar ziliungana kuwa nchi moja naichukulia kuwa ni hoja dhifu kidogo.
Kuna mchangiaji hapo juu amesema kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni Muungano wa baadhi ya mambo na pia si muungano wa baadhi ya mambo.

Ukitaka kuona udhaifu wa hoja ya kuwa Tanzania ni nchi moja zinangatia utata huu ambao unajitokeza katika EAC.
Je kama mambo 18 ya EAC ni manne tu,4 ndio mambo ya Muungano. Bado tunaendelea kusema au kujidanganya kuwa Tanzania ni nchi moja? Muungano madudu! (link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...nzibar-improve-agriculture-2.html#post3896314 )

Wanasiasa wetu wa Tz wanazidi kutuchanganya na kutubabaisha badala ya kushughulikia kero za Muungano. Kero za Muungano na changamoto zake zingeshughulikiwa kwa uwazi na bila ya ubabaishaji (utapeli au ujanja ujanja) ni wazi wananchi wa pande mbili za Muungano wa TZ wangeufurahia kutokana na faida zake. Leo kinachojengeka ni chuki, kejeli na lugha za hamasa za kuchochea mtafaruku, machafuko.

Inapofikia hali ya kuwa muungano unaleta shari (usuluhishi hauwezekani) ni vyema kwa kutumia mfano wa ndoa ya wazazi, ndoa hiyo ikome.

EAC ilivunjika na tumeona umuhimu wake tumeifufua tena. Muungano wa Tz pia unaweza kuvunjwa kama upande mmoja unataka hivyo. Kama miaka 48 tumeshindwa kuondoa kero za muungano ni wazi tunatengeneza shari/mripuko kwa siku za baaadae. Dalili zinaanza kujionesha.

Baada ya kufuatilia kwa kina mijadala ya tukio/matukio ya Zanzibar na jumuia ya UAMSHO, mimi si mmoja wa wale wanaoamini kuwa UAMSHO wana mkono katika uchomaji wa makanisa. Nina kila sababu ya kuamini kuwa wale wanaozuia mjadala wa Muungano ndio wana mkono katika hilo, wamepata sababu na mtu(kikundi) wa kumtupia lawama. Pia inawekana ikawa ni mbinu ya kufanya kuwa itakapofika 2014 hiyo katiba mpya iwe haijapatikana. Ni moja ya mbinu ya kuchelewesha katiba mpya. They know what they are doing!

Wametuingiza katika malumbano ya udini na kuacha issue muhimu. Tunalaumu mtendwa na tunamwacha mtenda anachekelea nyuma ya pazia. Tusiwe wepesi kuyumbishwa na ving'ang'anizi wa madaraka.

Tanzania deserves something better than this kind of politicking!
 
nashukuru kwani CUF imejibu ombi langu la jana...kutoa tamko juu ya machafuko ya zanzibar.

Vuai alisema, hivi sasa Chama Cha Mapinduzi kimetambua na kufahamu kwamba Jumuiya ya "Uamsho" ipo katika kivuli cha chama kimoja cha siasa na ndiyo maana kimekuwa kikifanya kiburi na jeuri kiasi ya kutamka kwamba hakuna mtu wa kukifuta.
 
Umma unashuhudia hali tete ya machafuko ambayo hayakutarajiwa yakiibukia tena Zanzibar, wakati ambapo Nchi ilishaanza kunawiri matunda ya utulivu na maridhiano, chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Pamoja na sababu au visingizio mbali mbali vilivyotajwa kuwa chanzo cha hali hiyo, zikiwamo za hamasa za wananchi, chuki binafsi, ukosefu wa hikma, matumizi ya nguvu za dola, na hata uchochezi wa makusudi wa wale wanaoonekana kutopendelea Maridhiano ya Kisiasa ya Zanzibar.

Kwa thamani yoyote hakuna asiyeweza kubaini umuhimu wa hali ya amani na utulivu, na madhara ya kukosekana kwake, hasa katika Visiwa hivi vya Unguja na Pemba ambavyo vimewahi kuelemezewa athari kubwa ya machafuko kwa muda mrefu.

Chama cha Wananchi,CUF, kama sehemu muhimu ya Umma wa Watanzania, hakiwezi kukaa kimya kutokana na mwelekeo mzima wa hali tete ya amani katika nchi, ingawa ni dhahiri wapo baadhi ya watu wasioitakia mema Zanzibar wakibainika kufurahia mazingira hayo, kwa maslahi binafsi, na pia kutoa kauli za kutatanisha za kisiasa.

Chama cha CUF, kinatoa wito kwa wananchi wote kuwa watulivu, wavumilivu, na kuitumia fursa ya kutoa mawazo yao bila ya jazba, pamoja na kutowanyima wengine nafasi ya kuwasilisha mitazamo yao.

Vitendo vya watu wachache kuchoma makanisa na kuharibu mali za watu ni vya uvunjifu wa sheria na kinyume na Utamaduni wa Kizanzibari; uchunguzi wa kina ufanyike na waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria, bila uonevu wala upendeleo.

Tahadhari iwepo ya kuepuka matumizi ya mabavu yanayoweza kuleta hamasa kwa wananchi, hatimaye ikachochea vitendo vya hujuma dhidi ya watu na mali zao, na pia kuepuka tabia isiyokuwa ya haki, ya kuwabambikizia kesi wananchi.

Ni lazima kwa wakati huu, na haraka iwezekanavyo, Serikali ikazungumza na Masheikh, bila ya kuona muhali, na kwa uwazi kabisa, ili kutafuta suluhu ya kudumu, kwa faida ya Nchi na Taifa kwa Ujumla.

HAKI SAWA KWA WOTE

…………………………………….
Salim A Bimani

Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu, Habari na
Uenezi na Mahusiano na Umma
Ondokezenu hapa Cuf,Sisi wazanzibari tumeunda serikali ya umoja wa kitaifa kwa mategeo yatu ni kuwa kuja kumaliza matatizo ya wazanzibari,moja ya matatizo hayo kwa kiu kubwa ni suala la muungano.

Lakini leo viongozi hawa wameshapewa fupa wamejisahahu katika madaraka hayo, serikali ya muungano imekuwa ikivunja katiba ya zanzibar ,tume ya katiba kablaya haijaingia zanzibar kikatiba lazima ipite katika baraza la wakishi na ipitishwe ,sheria yoyote itakayo undwa ndani ya bunge la muungano haiwezi kufanya kazi zanzibar mpaka ipitishwe na baraz ala wakilishi,kwa katiba ya serikali ya mapinduzi ya zanzibar SUK,lakini viongozi wetu wameridhishwa na ukiukwaji wa sheria hio.

Wananchi hapa ndipo walipotokwa na imani na Tume ya katiba,wameshindwa kuvumilia kwa hilo,na hawako tayari kukaa na kujadili hilo suala.

Wananchi wanachi hitaji sasa ni kura ya maoni kuukana muungano,hakuna jengine,muungano tulio nao ni wa TANU na ASP = ccm
 
Back
Top Bottom