Ndumbayeye
JF-Expert Member
- Jan 31, 2009
- 7,420
- 4,033
kule mtwara walivipata wapi wakati wa sakata la gesiVifaru!!!!!! siku hiz polis wana wanavifaru!!
kule mtwara walivipata wapi wakati wa sakata la gesiVifaru!!!!!! siku hiz polis wana wanavifaru!!
Na longo
N A L O N G Oshoga
Wameona aibu wamehariri kidogo, sasa wamekuja na idadi ya askari wasio na idadi, sijui wamekuwa sisimizi?Hahahaa taarifa imejaa uongo mwanzo mwisho...sijui tangu lini Polisi wakafundishwa kutumia vifaru....hao ndio bavicha aisee
Jina lako tu linaakisi uwezo wako wa kufikiri, kuandika na kujenga hojaTulia moto wewe
1. Walimu wakwee mchuma bure....0
2. Sugwede bwerere mtonyo 1800....0
3. Wajukuu wa Matonya watarejea kijijini...0
4. Watu kama wewe marufuku Dar....0
5. Kuanzia leo marufuku kubanduana bila pingu za maisha...0
Haya ndio maneno mengi. Ulioandika wewe ni machache
Akili yako haitoshi kufanya utafiti...mbaya zaidi, kutafiti IQ za watu. Mimi nitakwambia kwa nini.
Hivi karibuni limetoka katazo la harakati zote za kisiasa kwa upande wa upinzani. Kwa katazo hilo, ulitaka BAVICHA uwaonee uwani kwako wakija kukusaidia kuanika nguo kwenye kamba? Hiyo ndio IQ yako...unataka kuchunguza wenzio!
Unawezaje kuchoshwa na habari isiyokuhusu? Kweli dunia ina magonjwa mengi kuliko uwezo wa matabibuLao ni siku ya mapumziko Bavicha mnapaswa kupumzika kesho mwende shambani na kuchunga mifugo yenu ,mnatuchosha na habari zenu za bavicha.
Juu ya yote, mimi siyo level yako linapokuja suala la kufikiri...nyu..u!Jina lako tu linaakisi uwezo wako wa kufikiri, kuandika na kujenga hoja
Juu ya yote, mimi siyo level yako linapokuja suala la kufikiri...nyu..u!
huu ni upumbaf na ul ofa. siasa za namma hii kiongozi mkuu wa chama bwana Lowasa ameshazipiga marufuku. chama kimesha graduate wajameni hivi hamjitambui? ? mkizidi kukaidi basi chama kitafikiria kuwafukuza mwende mkatafute uelekeo wa chama kingine. ni lazima tujifunze namna ya kutii amri ya viongozi. hata Mbowe mwenyewe ameshakemea na kusimamisha utumbo wote huo ulioanzishwa na BAVICHA. tafuteni shughuli nyingine ya kufanya kama hamuwezi siasaVijana Wa Bavicha wamesema mpango Wa kwenda Dodoma upo palele na kinachoendelea sasa ni kutazama mpango B wa kufika huko.
Wamesema hawawezi kuacha Uhuru wa kufanya siasa ukitekwa na wachache huku vijana wenye uzarendo kwa taifa Lao kama wao wakikaa kimya.
Kiongozi Wa Bavicha taifa akihojiwa na ITV habari SAA mbili usiku amesema wametii agizo la Mwenyekiti taifa mh.Mbowe ila wanaandaa kikao kitakacho mwalika Mh.Mbowe kuweka mikakati ya kurudisha Uhuru wa Tanganyika mikononi mwa RAIA.
Kwa mikutano ya CCM ulinzi unaimarishwa, ila upande wa Upinzani inapigwa marufuku. Siasa za kiafrika ni Mateso hasa kwa vyama vya UpinzaniKwa kweli haipendezi kuona taifa hili likijengwa kwa kodi za wote lakini wanaofaidi ni kakundi kadogo ka viongozi ndani ya CCM na marafiki zao tu.
Sio sawa kuwakataza wapinzani wasihiloji wala kuwaambia watanzania juu ya matumizi na mwenendo wa kodi za watu mil. 6 waliowapigia kura. CCM ina haki ya kuwapa taarifa wapiga kura wao mil. 8 juu ya maendeleo yanayotokana na kodi zao halikadhalika wapinzani nao wanahaki ya kukosoa juu ya matumizi ya kodi zao
Pamoja na kwamba sera zinazotekelezwa ni za CCM lakini kodi hawatoi wao wenyewe na kwa uzoefu maCCM wengi ndio wakwepa kodi na wala kodi inayotoka kwa asilimia kubwa kutikana na kushika ajira zote nono serikalini.
Haki ni vizuri ikawa sawa kwa vyama vyote sio kwa CCM wenyewe.
Nadhani ingekuwa vyema jeshi la polisi likaachana na mambo ya wanasiasa wanaokosoana kwa hoja.Kwa sababu hapakua na haja ya kutafuta taarifa za kiintelijensia kwa ajili kujua kuwa kuna vyama vitakwenda Dodoma kuzuia mkutano wa CCM kwani CDM walitangaza hadharani bila kificho na mimi nikategemea kuwa mkutano huo utaahirishwa kutokana na taarifa hizo zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani. Nadala yake Polisi wameimarisha ulizi ,jambo ambalo ni sahihi na ndilo lilokuwa linatakiwa kufanyika hata kwenye mikutano ya uponzani.
Kinachotakiwa ni kuimarisha ulinzi na sio kupiga marufuku mikutano ya kisiasa.
CCM imeinunua CHADEMA tena kwa hela za walipa kodi mpango wa lowasa na mbowe si mipango ya wapinzani hivi sasa chama kina say moja akisema ni mapanya ndio mkuu hata kama twaona ni mapakahuu ni upumbaf na ul ofa. siasa za namma hii kiongozi mkuu wa chama bwana Lowasa ameshazipiga marufuku. chama kimesha graduate wajameni hivi hamjitambui? ? mkizidi kukaidi basi chama kitafikiria kuwafukuza mwende mkatafute uelekeo wa chama kingine. ni lazima tujifunze namna ya kutii amri ya viongozi. hata Mbowe mwenyewe ameshakemea na kusimamisha utumbo wote huo ulioanzishwa na BAVICHA. tafuteni shughuli nyingine ya kufanya kama hamuwezi siasa
Mtakomaa lini? lowassa kawapa ushauri muwache uwanaharakati hamsikii..na mzee mtei juzi kamsifu sana jpm..eti anafuata sera za chadema. la ajabu chadema yenyewe sasa hawafuati sera zao bali wameamua kufuata magamba na nyumbu wafuata malisho waliobanduka ccm.Ndugu waandishi wa habari kwanza tunawashukuru kwa kazi kubwa mliyoifanya kwa kuwaeleza Watanzania adhima yetu ya kwenda Dodoma, katika kuhakikisha BAVICHA tunaisimamia kauli Jeshi la Polisi na ya Mhe. Raisi, na kulisaidia jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya kisiasa kwa vyama vyote hadi mwaka 2020 tukianza na mkutano haramu wa CCM hapo tarehe 23 July 2016.
Tunaendelea na msimamo wetu kuamini mkutano huo sio halali,kwakuwa ni Mkusanyiko wa Kisiasa ambao Mhe. Raisi na Jeshi la Polisi waliikataa vinginevyo watoke hadharani kukanusha Agizo na msimamo wao ulioathiri tayari vyama vya upinzani vikiwemo CHADEMA na ACT kwa kuzuiwa kukutana.
Sisi BAVICHA tunaheshimi kauli ya Kiongozi wetu mkuu wa chama,aliyotuomba tusiende Dodoma, kauli hii imeipa nafuu kubwa CCM kwakuwa hawakuwa na ubavu wa kutuzuia tusizuie mkutano wao.
Tulijipanga kila kona ya nchi hii,na hata jeshi la Polisi lisingeweza kutuzuia katika kutekeleza azima yetu,ya kutaka haki na usawa wa Kidemokrasia katika nchi hii ya Kidemokrasia.
Sasa basi,baada ya M/kiti kutuomba vijana wake tusiende Dodoma, sasa tunaamua kuja na plan B,ambapo hatutaenda Dodoma lakini hatutaruhusu mkutano wa CCM ufanyike mpaka pale Serikali itakapotoa kauli ya haki sawa za Kidemokrasia kwa kila chama,kufanya siasa maana hivi tunavyoongea CCM wao wanafanya mikutano ya hadahara na wengine wanazuiwa.
Tunayo taarifa ya Baadhi ya mawaziri na wabunge wa CCM wao wanafanya mikutano ya hadhara katika majimbo mbali mbali,na picha za matukio hayo tunazo kwa ushahidi hivyo tukashitaki wapi?
Tunazo taarifa za Wakuu wa wilaya wakifanya mikutano ya hadhara na wanachi,hivi kati ya mkuu wa wilaya na vyama vya siasa nani mwenye mamlaka ya kufanya siasa!??
Tunaomba Watanzania waone na wapaze sauiti jinsi nchi yao inavyoongozwa Kidikteta,na kukosa usawa.Leo Dodoma kumepelekwa Polisi kutoka katika mikoa ya Morogoro, Singida,Dar es salaam na Iringa wakiwa na kila aina ya Vifaa vya kivita.
Kwa Mara ya kwanza katika historia ya nchi hii Polisi wengi wasio na Idadi wakiwa na silaha nzito za kivita wanaenda kulinda mkutano wa Kisiasa,hii haijawahi kutokea.
Mtakumbuka Polisi wamewahi kuzuia mikutano mingi sana ya CHADEMA kwa kigezo kutokea machafuko na hali ya usalama ni ndogo,lakini hii imekuwa tofauti sana kwa upande wa Ccm wao usalama ni mdogo sana kupita maelezo katika mkutano wao wa tarehe 23 July,lakini vimepelekwa mpaka vifaru vya jeshi kuimarisha usalama.
Hii ni double standard ya hali ya juu,inayooneshwa na jeshi la Polisi kwa vyama vya siasa na huwa mara nyingine tunasema Polisi wanatumika na Ccm na huu ni ushahidi wa kwanza mkubwa kabisa.
Polisi wa nchi hii wako radhi wao wafe lakini Ccm isiguswe na wapo radhi hata kuua wapinzani ili Ccm iendelee kuwa madarakani,uko wapi usawa wa Kidemokrasia??? Uko wapi weledi wa kiutendaji wa jeshi letu la Polisi?.
UNYANYASAJI WA HAKI ZA BINADAMU.
Tokea BAVICHA tumatangaza kwenda Dodoma, majeshi yaliyopelekwa Dodoma kuisaidia Ccm yamekuwa yakifanya unyanyasaji mkubwa kwa raia,wamekuwa wakikamata wananchi hivyo na kuwaweka ndani bila kuwafungulia kesi,na jina la mtu aliyekamatwa tokea siku ya jumatano mpaka Leo hajafunguliwa kesi,wala kufikishwa Mahakamani na hata mawakili wanapoenda kujua hatima yake wanafukuzwa na Polisi.
Polisi wanaingia katika Nyumba vya kulala wageni usiku,kufanya ukaguzi,kinadada wanadhalilika kwakuwa wengine wanakutwa uchi wa mnyama na Polisi wa kiume,huu ni unyanyasaji mkubwa unaofanywa na jeshi la polisi Dodoma.
Sasa tunawaomba vijana wetu wote nchi nzima watulie na wasubirie maamuzi ya kikao kikubwa cha kamati ya Utendaji,kitakachokaa siku ya jumatano ya tarehe 20.07.2016 Kukutana na M/kiti wetu tukiwa tayari na Plan B ya kuipigania Demokrasia ya Taifa letu.
Imetolewa July 16
M/kiti BAVICHA Taifa