Taarifa ya BAVICHA kuhusu Mikutano ya CCM Dodoma

Komaa kwanza mdio.urudi humu kwenye uzi kwa sababu credit zako zinaonyesha wewe ni kilaza na anaeshoboka na Ubavicha hujui kama wenzako wameshageuza mgongo?wameshapanda boat ya kuelekea kwenye likizo ya kujipanga upya dhidi ya maisha yao wewe unang'ang'ani JF na bavicha@mwana mtoka pabaya...
 
Excellent mmepigana kwa maneno ujumbe umefika! Hata Wapalestina sio wajinga wanapopigana kwa kurusha mchanga na mawe wakati Israelites wana vifaru!
 
Freedom of speech, that is my opinion and I am entitled to it like you are entitled to yours.

Siwezi kukubaliana na kila unachoamimi kwa vile tu wewe unaamini hivyo. Si vizuri kufuata rai ya mtu kibubusa na sifuati rai kwenye hiyo taarifa kibubusa.

I am keeping in mind that even freedom has limits.


Wacha weee! acha kujambajamba, jibu hoja za watu.
 
Ndugu waandishi wa habari kwanza tunawashukuru kwa kazi kubwa mliyoifanya kwa kuwaeleza Watanzania adhima yetu ya kwenda Dodoma, katika kuhakikisha BAVICHA tunaisimamia kauli Jeshi la Polisi na ya Mhe. Raisi, na kulisaidia jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya kisiasa kwa vyama vyote hadi mwaka 2020 tukianza na mkutano haramu wa CCM hapo tarehe 23 July 2016.

Tunaendelea na msimamo wetu kuamini mkutano huo sio halali,kwakuwa ni Mkusanyiko wa Kisiasa ambao Mhe. Raisi na Jeshi la Polisi waliikataa vinginevyo watoke hadharani kukanusha Agizo na msimamo wao ulioathiri tayari vyama vya upinzani vikiwemo CHADEMA na ACT kwa kuzuiwa kukutana.

Sisi BAVICHA tunaheshimi kauli ya Kiongozi wetu mkuu wa chama,aliyotuomba tusiende Dodoma, kauli hii imeipa nafuu kubwa CCM kwakuwa hawakuwa na ubavu wa kutuzuia tusizuie mkutano wao.

Tulijipanga kila kona ya nchi hii,na hata jeshi la Polisi lisingeweza kutuzuia katika kutekeleza azima yetu,ya kutaka haki na usawa wa Kidemokrasia katika nchi hii ya Kidemokrasia.

Sasa basi,baada ya M/kiti kutuomba vijana wake tusiende Dodoma, sasa tunaamua kuja na plan B,ambapo hatutaenda Dodoma lakini hatutaruhusu mkutano wa CCM ufanyike mpaka pale Serikali itakapotoa kauli ya haki sawa za Kidemokrasia kwa kila chama,kufanya siasa maana hivi tunavyoongea CCM wao wanafanya mikutano ya hadahara na wengine wanazuiwa.

Tunayo taarifa ya Baadhi ya mawaziri na wabunge wa CCM wao wanafanya mikutano ya hadhara katika majimbo mbali mbali,na picha za matukio hayo tunazo kwa ushahidi hivyo tukashitaki wapi?

Tunazo taarifa za Wakuu wa wilaya wakifanya mikutano ya hadhara na wanachi,hivi kati ya mkuu wa wilaya na vyama vya siasa nani mwenye mamlaka ya kufanya siasa!??

Tunaomba Watanzania waone na wapaze sauiti jinsi nchi yao inavyoongozwa Kidikteta,na kukosa usawa.Leo Dodoma kumepelekwa Polisi kutoka katika mikoa ya Morogoro, Singida,Dar es salaam na Iringa wakiwa na kila aina ya Vifaa vya kivita.

Kwa Mara ya kwanza katika historia ya nchi hii Polisi wengi wasio na Idadi wakiwa na silaha nzito za kivita wanaenda kulinda mkutano wa Kisiasa,hii haijawahi kutokea.

Mtakumbuka Polisi wamewahi kuzuia mikutano mingi sana ya CHADEMA kwa kigezo kutokea machafuko na hali ya usalama ni ndogo,lakini hii imekuwa tofauti sana kwa upande wa Ccm wao usalama ni mdogo sana kupita maelezo katika mkutano wao wa tarehe 23 July,lakini vimepelekwa mpaka vifaru vya jeshi kuimarisha usalama.

Hii ni double standard ya hali ya juu,inayooneshwa na jeshi la Polisi kwa vyama vya siasa na huwa mara nyingine tunasema Polisi wanatumika na Ccm na huu ni ushahidi wa kwanza mkubwa kabisa.

Polisi wa nchi hii wako radhi wao wafe lakini Ccm isiguswe na wapo radhi hata kuua wapinzani ili Ccm iendelee kuwa madarakani,uko wapi usawa wa Kidemokrasia??? Uko wapi weledi wa kiutendaji wa jeshi letu la Polisi?.

UNYANYASAJI WA HAKI ZA BINADAMU.

Tokea BAVICHA tumatangaza kwenda Dodoma, majeshi yaliyopelekwa Dodoma kuisaidia Ccm yamekuwa yakifanya unyanyasaji mkubwa kwa raia,wamekuwa wakikamata wananchi hivyo na kuwaweka ndani bila kuwafungulia kesi,na jina la mtu aliyekamatwa tokea siku ya jumatano mpaka Leo hajafunguliwa kesi,wala kufikishwa Mahakamani na hata mawakili wanapoenda kujua hatima yake wanafukuzwa na Polisi.

Polisi wanaingia katika Nyumba vya kulala wageni usiku,kufanya ukaguzi,kinadada wanadhalilika kwakuwa wengine wanakutwa uchi wa mnyama na Polisi wa kiume,huu ni unyanyasaji mkubwa unaofanywa na jeshi la polisi Dodoma.


Sasa tunawaomba vijana wetu wote nchi nzima watulie na wasubirie maamuzi ya kikao kikubwa cha kamati ya Utendaji,kitakachokaa siku ya jumatano ya tarehe 20.07.2016 Kukutana na M/kiti wetu tukiwa tayari na Plan B ya kuipigania Demokrasia ya Taifa letu.

Imetolewa July 16

M/kiti BAVICHA Taifa
Acheni vichekesho. Kuweni makini japo kidogo. Kuzuia Mkutano UPI? Thubutuuuuuuuu!!
 
Ningependa kuzungumzia swala la kusahidia Polisi kwa kuzuia mkutano wa chama tawala.

Kama utaenda Dodoma umeumia nenda ukaage kwenu mapema siasa mpaka muda ufike tufanyeni kazi mambo ya wanaharakati tuweke pembeni jaman muda huo bora tukatafute pesa maisha yaendelee tu . Kama wakubwa wamesema mtulie tulieni tu mbona maisha yapo na yataendelea tu ni ushauri tu kama kuandamana twendi na watoto wao tena wakae mbele kwani hata wao ni vijana.

Ila si mlikatazwa mpaka na viongozi wachama mpaka watoe tamko ? sema walimwengu ndo sisi wenyewe kama ukutaka kusikia utasikia tu.

Fikilia juu ya hilo ndugu uku mambo ni hatari ..? ila hutishiwi uwamuzi ni wako kuchambua jema na baya ila kama una familia utasumbua tu ndugu ,Jamaa na marafiki tu baada wafanye mengne wanabaki kukuangaikia wewe.
Ndugu zangu tambueni kuwa wanakula tizi tu mkija mtawakuta wako fiti sana Ila tambua hapa kazi tu. Mengine badae tulijenge taifa .Vijana ndo taifa LA Leo na kesho pia
 
Mke aliamka saa nane za usiku kakuta
mumewe hayuko kitandani,akamkuta
yuko sebuleni akiwa na mawazo tele;
MKE: Jamani vipi tena usiku huu? MUME: Unakumbuka siku baba yako
alipogundua una mimba yangu
... nakunilazimisha
nikuoe au la atanifunga miaka kumi?
MKE: He kumbe ndio unalokumbuka?
MUME: (huku machozi yakidondoka) Kama ningekukataa leo
ningekuwa huru natoka jela.
 
Kama ccm wanamkutano wa mw/kiti kukabidhi uongozi na
mw/kiti mbowe na yeye aitishe mkutano wa kukabidhi uenyekiti kwa MTU mwingine tuone Kama utazuiliwa na police?ndipo tuone huo uonevu.sio kila siku mkutano ya kuhamasisha vulugu na maandamano.mfano toka wenje ashidwe ubunge mwanza hakuna maandamano na mabomu.watu tunafanya kazi kwa raha mstarehe.
 
Back
Top Bottom