Taarifa rasmi ya ikulu; hand writing analysis and criminal profiling graphology

WILLY GAMBA

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
211
87
Ubongo wetu ndio unaongoza mkono wa kuandikia(uwe wa kuume au wa kike)
Kila utakacho liandika ni zao la ubongo wako kutuma ujumbe kwa msuli wa mkono wako kuandika .
Kwako wewe wa Magogoni unaona umemaliza kazi yako lakini wengine ndio umetufungulia ka dirisha
ka jikoni tuingie ndani tujionee.....

Ugumu wa kusoma ujumbe -maneno yamepigwa mshkaki- space bar imekufa? au???
Judge not- Ooooh Mrema ni MPUUZI,UKOSEFU MKUBWA WA ADABU(Kwa nani,nyie ndio mmepewa green light ya kukashifu????)

Kigezo cha kwanza hapo juu wataalam tunakwambia upo under pressure au unatumia vitu ambavyo havitakiwi vitumike ukiwa kazini.
 
viongoziikulu.JPG




https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/170168-wasiotaka-ikulu-iwe-na-website-hawa-hapa.html
 
Mkuu Will Gamba, nimeisoma ile taarifa ya Ikulu na yake mapungufu ya uandishi nimeona na ukiisoma in between the lines, utagundua mwandishi alikuwa na tatizo la intelect!.

Zamani nilidhani graphology ni kwa handwriting tuu, kumbe hata kwa keyboard!.
 
Taarifa kama inatoka kwa diwani, kauli za mtaani nyingi. maneno ya mipasho kama "hakuna mtu mwingine wakumbebea msalaba huu. Badala ya kutafuta mchawi asiyekuwepo" yananifanya nifikiri aliyeandika alikuwa Mama Salma.
 
Kesi imeamuliwa asubuhi ,mchana ikulu inajibu,Hapa ni kuwa Ikulu ilikuwa inacontrol shughuli nzima pale mahakamani.Kwa ufupi Ikulu ina mkono wake.? Kwanini imewahi kujibu na vingine awajibu????/
 
Kwa wale walio soma somo la Mantiki [Logic] hawawezi kupata tabu kuhusu kilicho jibiwa na Ikulu.

Ikulu imekanusha hadharani kile ilicho kuwa ina kifanya kwa kificho nyuma ya pazia.

1. Wamekanusha kuwa hakuna mawasiliano ya simu ya kushawishi mahakama/jaji kutoa hukumu. Kwa nini wataje mawasiliano ya simu kuwa hayaja tumika wakati hakuna mahali popote walipo shutumiwa kuwa wametumia simu? Ina maana wanajua kuwa walisha yatumia mawasiliano kwa kificho kutoa hukumu kwa remote control halafu wakaona haraka sana waje wakanushe kuwa hawaja tumia mawasiliano ya simu.

2. Wamekanusha kuwa hakuna hata njia ya maandishi iliyo tumika kumshawishi jaji/mahakama kuhusu kesi hiyo ili atoe uamuzi wa hukumu. Hapa pia pana uwanikaji wa siri iliyotumika na Ikulu kupenyeza hukumu, nani kaituhumu ikulu kuwa imetumia maandishi? Kwa nini wasinge jibu tu kuwa hakuna mawasiliano yoyote yaliyotumika bila kutaja aina ya mawasiliano wanayo hisi kuwa wameyatumia?

3. Kwenye kanusho la Ikulu kuna lugha za mtaani zilizo zoeleka kujibu mipasho ya mitaani. Kwa nini ikulu iseme Lema asitafute mchawi? Je ikulu yetu inaamini kwenye uchawi? Anae muaminisha uchawi mwenzie na yeye ni mchawi, je kama Ikulu ina mshurutisha lema asitafute mchawi inataka tuione taarifa ya ikulu kuwa niya malaika wakati anae muaminisha mwenzake uchawi nae ni mchawi au muamini vitendo vya kichawi? Jiulize, Kama Lema atakuwa haamini uchawi/vitendo vinavyo ambatana na uchawi, mchawi ni nani kati ya Lema na Ikulu kwenye hukumu ya ubunge?

4. Kwenye taarifa yake Ikulu imesema lema ni mtovu wa nidhamu! Ikulu imeanza lini kuwa na baraza la nidhamu lenye vipimo vya kujua kuwa Lema ni mtomvu wa nidhamu au si mtovu wa nidhamu? Na ili kuamua kuwa fulani ni mtovu wa nidhamu
lazima ulikuwepo mjadala wa awali wa kutuhumu na kufikia maamuzi kuwa huu ni utovu wa nidhamu. Mjadala huo umefanyika lini? Yaani hapa ni sawa na mwanao akuambie "baba! makamasi ni matamuuu!" huhitaji kuwa na shahada ya uzamivu kujua, mwanao atakuwa ameyaonja tu na kujua radha yake.

Mwisho.
Taarifa nyingi za Ikulu huwa zina maneno ya lugha za vijembe vya mitaani ambavyo huku mitaani hutumika kujibu tuhuma zinazo mchoma mtu. "Usitafute MCHAWI bibi mpe mapenzi mumeo", "We shan'kupe acha UZABINA ZABINA", Hayo niliyo bold ni maneno ya mitaani kwetu ambayo nimesha yaona yakitumika kutoa taarifa za mahali patakatifu.
 
Ubongo wetu ndio unaongoza mkono wa kuandikia(uwe wa kuume au wa kike)
Kila utakacho liandika ni zao la ubongo wako kutuma ujumbe kwa msuli wa mkono wako kuandika .
Kwako wewe wa Magogoni unaona umemaliza kazi yako lakini wengine ndio umetufungulia ka dirisha
ka jikoni tuingie ndani tujionee.....

Ugumu wa kusoma ujumbe -maneno yamepigwa mshkaki- space bar imekufa? au???
Judge not- Ooooh Mrema ni MPUUZI,UKOSEFU MKUBWA WA ADABU(Kwa nani,nyie ndio mmepewa green light ya kukashifu????)

Kigezo cha kwanza hapo juu wataalam tunakwambia upo under pressure au unatumia vitu ambavyo havitakiwi vitumike ukiwa kazini.
Mkuu umenena vema hata mimi nimeliona hilo eti imeandikwa na kurugenzi ya mawasiliano.Yaani ukiona hiyo taarifa haina viwango kwani maneno mengi yameunganishwa na inavyoonekana ni kweli alikuwa underpressure,pia ameandika maneno mengine ambayo hayana busara.Sijui kama aliyeandika kama ana fikra iliyotimilika.
 
Wawe wanajifunza kwenye press release za wenzetu. Mfano hii toka Bolton Wanderers. Inakuwa short and clear.
"Bolton Wanderers can confirm that Fabrice Muamba has been admitted to the heart attack centre at London Chest hospital where he is currently in a critically ill condition in intensive care. No further information will be issued at this stage. The club has requested the media to respect his family's privacy at this time."
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Jana tarehe 5 febr, 2012 baada ya mahakama kuu kanda yaArusha kutamka kutengua matokeo ya Mhe. Godbless Lema, jioni hiyo hiyo tunapatataarifa kwamba ikulu inasikitika kwamba Mhe. Godbless Lema amesema ikulu/Mhe.Rais hajahusika ktk maamuzi hayo kama ilivyodaiwa na Mhe. Gobless Lema. Miminajiuliza kwa nini Ikulu imekuja haraka katika hili wakati, si kurugenzi husikawala Mhe. Rais amejitokeza hadharani kutolea kauili mambo mbalimbali ama kwamuda muafaka au haijitokezi kabisa. Je kurugenzi ya mawasiliano Ikulu/Mhe Raisje walitoa matamko mara moja ktk mambo ya fuatazo;
1. Rais kuwekwa ktk orodha ya watuhumiwa wa EPA
2. Mmiliki wa Richmondi
3. Mgomo wa mafuta
4. Kukatika ktk kwa umeme kila wakati
5. Posho za wabunge/kusainiwa au kutosainiwa
6. Sakata la ugonjwa wa Mwakyembe,
Kurugenzi ya Mawasiliano ikulu bado haijasimama na hivyokuaminiwa kuwa inawajibika vilivyo. Bado inaleta maswali mengi, kama hiviambavyo imekuja na kauli ya haraka baada ya kuhusishwa na kutengua matokeo yaUbunge wa Mhe. Godbless Lema.
 
Kesi imeamuliwa asubuhi ,mchana ikulu inajibu,Hapa ni kuwa Ikulu ilikuwa inacontrol shughuli nzima pale mahakamani.Kwa ufupi Ikulu ina mkono wake.? Kwanini imewahi kujibu na vingine awajibu????/

Kweli mzee wameishiwa mbinu sana,yani haiwezekani ikulu iwahi kujibu namna ile kama haikua inacontrol na kufuatilia kwa makini utekelezaji wa maagizo yake,hebu fikiri kesi ya mbunge inawezaje kuteka attention ya ikulu kiasi kile wakati ikulu ina mambo mengi ya kufuatilia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom