Taarifa maalum ya maandalizi ya maandamano ya kupinga muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Vizuri sana, kwani hawa Wazanzibar hawatusaidii lolote watu wa bara, wamekalia udini tu.
 
wazanzibar kwa kuongea bwana,wanaongea ongea tu,wenyewe ndio wanafaidika na upendeleo kibao lakini kelele nyingi.tokeni zenu,mkafie mbali,hatuuhitaji muungano bora muondoke.kila la kheri
 
Hivi jamani, kweli Tanganyika wanafaidika nini na uwepo wa Zanzibar? Niliwahi kuambiwa kuwa ni kwasababu ya usalama wa Tanganyika tu maana hawa jamaa wanaweza kuleta kashkashi za Ualshababu. Ntashuikuru kama mtafanikiwa kujitenga ili na sisis tujulikane kuwa tupo maana hata sherehe za miaka hamsini zilitambulisha na JK kama uhuru wa Tanzania, sisi hatuna hata bendera wala wimbo wa Taifa wakati nyie mna jeshi, wimbo wa Taifa, bendera na mambo mengine.....mmmh haya hongereni sana
Mi nadhani waachiwe kisiwa chao ila Tanganyika tu keep a close eye on the island.

Kama hayo ya Alshabab yakitokea basi tuna kioccupy kisiwa until further notice.
 
Kama upande mmoja wa muungano unataka kujitenga hamna haja ya kung'ang'ania. Hata ndoa, wanandoa mmojawapo akichoka inabidi mwingine akubali yaishe japo ahadi alikuwa mpaka kifo kiwatenganisha. Kwa mantiki hiyo basi hapatakuwepo na kizuizi, Wazenj kuwa na serikali yao kwa amani alikadhalika watanganyika.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Ila jamani naombeni tu tuwe wakweli hivi ninani Zanzibar ni fisadi? Ebu waipate nchi yao wajiendeleze sisi tubaki na ufisadi wetu labda tukiona nidhamu ya serikali na viongozi jinsi inavyo account kwenye maendeleo ya nchi tutapata akili na kujua kuwa ufisadi ni misumari inayotoboa matairi ya gari la maendeleo.....I wish u all da best...
 
Watanganyika tufanye maamuzi magumu, tuvunje muungano na zanzibar na tujitoe Jumuia ya Africa mashariki. Kisha tukae chini tutafakari tunakokwenda tuitoe nchi hii kwenye kwenye haya matatizo lukuki ya kujitakia. Adui mkubwa kwa Tanganyika kwa sasa ni Muungano na Jumuia ya Africa Mashariki, hivi vitu ni mzigo unaotulemea. Wazanzibar wanajua fika kuwa ziko lao tulipakaziwa na CIA tulibebe na si siri tena, wala muungano huo hatujawahi furahishwa nao. Hata mwalimu JKN alishawahi sema kuwa angekuwa na uwezo hivyo visiwa angevisukumia mbaali kabisa na Tanganyika. Hakika mwalimu alijua, aliliona zigo la gunia la misumari la visiwa vya Zanzibar.

Mnyukano wa kisiasa uliopo sasa kati ya CCM na CDM, Wapambanaji na ufisadi na wazee wa ukwasi hii yote inasababishwa na kukosekana kwa "SOCIAL COHESION" baina ya Watanganyika na imesabisha tukose muelekeo kwa sasa. Tukipata kiongozi imara haya yote yataisha, ila sio la Muungano hili litatusesa milele.

Tanganyika inayopakana na nchi nane, itakuwa muhimi zaidi kama tutaongeza nchi ya tisa kwa kupakana nayo ambayo itakuwa ni Zanzibar na in future tutapakana na nchi kumi yaani Unguja na Pemba hapo ndipo inatufanya tuweze amua nani wa kushirikia na naye kwa maslahi zaidi.

Hivi sisi mungu atupe nini... nchi kubwa zaidi ya kuziungaisha nchi zote za Jumuia ya Africa mashariki pamoja na Zanzibar, ardhi, mito, madini hatuna kitisho cha jangwa kama hao walioko kaskazini kwetu.
Ni wakati sasa wa kujua nchi gani za kushirikiana nazo. Kulingana na Geographia ya ukanda huu, kuna nchi kama Zambia, Malawi, Rwanda, Burundi, East DRC zinatuhitaji kwa vyovyote vile ili kupitisha bidhaa zao, Kwa nini iwe tunawakumbalia Zanzibar na Kenya mbao hawana opportinity hiyo na wanaimezea mate kwa hali na mali ili waifikie...Whyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyy Kenya!!!!!.

Lets put our hands together and surpport the effort initiated by Zanzibaris...Zanzibar must quit the bogus Union ili nasi tulitue hili zigo la misumari. Hakika tunaweza

Tanganyika is coming soon!!
 
Harakisheni hayo maandamano yafanyike na msisitize huo muungano uvunjike haraka. Watanganyika wa kawaida (na hao ndio wengi) hawaelewi na hawajaona faida ya muungano kwao zaidi ya malalamiko kila kukicha.Kuna member hapa JF ameandika akiuliza "ni ndoa gani hiyo ambayo kila kukicha mke anatishia kurudi kwao?" swali la msingi!
 
Hongereni wazanzibar ingawa kwa style za diplomacy walizonazo UN, jambo hilo laweza kucheleweshwa. Mbona hapo kazi ni ndogo tu! Saidieni kukiweka madarakani chama cha upinzani huko bara na mwanga mtauona asubuhi na mapema maana sote tunajua huo ni muungano wa ccm! Bila kuiondoa ccm Zanzibar kujitenga ni ndoto. Bila kujali itikadi za vyama wala dini, ungeni mkono upinzani huko bara! Hiyo ndiyo dawa!
 
Nyie kupe mwende salama hakuna anaewahitaji mmetunyonya na tumewabeba vyakutosha.
 
Harakisheni hayo maandamano yafanyike na msisitize huo muungano uvunjike haraka. Watanganyika wa kawaida (na hao ndio wengi) hawaelewi na hawajaona faida ya muungano kwao zaidi ya malalamiko kila kukicha.Kuna member hapa JF ameandika akiuliza "ni ndoa gani hiyo ambayo kila kukicha mke anatishia kurudi kwao?" swali la msingi!
Mke ni nani hapo?
Mi nazani ni ndoa ya jinsia moja! bora tuivunje!
 
Back
Top Bottom