Taarifa maalum ya maandalizi ya maandamano ya kupinga muungano wa Tanganyika na Zanzibar

jaman mlishaambiwa na mzee...
"Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kama koti, cku likiwa dogo likawabana mnaweza livua." nnadhan hii miaka karibia 50 koti tayari limeshawabana na xaxa huu ndio wakati muafaka wa kuvua gamba la muungano.
Nnaombeni niwatakie
MVUNJIKO WA MUUNGANO MWEMA!....
 
Muungano ukivunjika tutaingia kwenye matatizo makubwa, lazima Muungano uwepo kwa sasa. Tatizo walioko hawana nia ya dhati kushughulikia matatizo ya muungano, sasa mambo yanavyozidi kuparaganyika wenzetu wanapata nafasi ya kufanya wanachotaka. Hatujui mwisho wake lakini sioni uwezo wa JK kuishikilia nchi isiparaganyike kwa sasa.
 
Nyinyi Wazanzibari why to go all the hard way? Njia rahisi na fupi ya kuachana na Muungano huwa mnapewa
kila baada ya miaka 5 lakini hamtaki kuitumia. Njia hiyo ni KUACHANA NA CCM KATIKA SANDUKU LA KURA.
Kipigieni kura chama kingine mbadala muone, haitachukua hata miaka 2 mnapata Zanzibar yenu.

Maadamu mnaendelea kuikumbatia CCM sahauni kamwe kupata hiyo Zanzibar yenu. The last nail to the coffin
of Zanzibar out to the UNION ni huo muswaada mpya uliopelekwa bungeni na Celina Kombani, kama wawakilishi
wenu CCM + CUF = SUK watauipisha kama ulivyo basi hilo suala litabakia utopia, kwani hakuna RAIS yeyote kutoka
CCM atakayeiachia Zanzibar Count my words. Huo muswaada wa Katiba mpya, RAIS ni alpha na omega na kwa
mambo yalivyo sasa msitarajie hata siku moja RAIS wa JMT atatoka tena Zanzibar, Mlionjeshwa Mwinyi na huo ndio
mwisho wenu. Mgombea wa Urais wa JMT kutoka Zanzibar in this era is NOT ELECTABLE, ni garasha kwa maneno mengine
kwa mgombea yeyote kutoka Tanganyika hata akiwa Mtikila na DP yake.
 
hatuhitaji muungano wa nini kwanza ? sababu kubwa ya muungano ni karume kuogopa kupinduliwa sasa hayupo tena tunataka wa nini, what a shame guys
 
Eti ukoloni wa Tanganyika!!!! Nyie ndio bure kabisa!!! Kabla hamjaondoka mkumbuke kulipa lile deni lenu la TANESCO la zaidi ya shilingi bilioni 200.

Na wale wenye majumba bara nao wajiandae kuyaacha, maana hata kuyauza si halali, walikuja bara kwa mitumbwi na rambo zao na hawapaswi kuondoka na MV. Mali zote zilizochumwa bara na wapemba au waunguja ni za bara.

Wanzanzibar wanatishia nyau tu hawana ubavu wa ku-survive nje ya muungano. Wanafanya hivi ili kuwa na upper hand kwenye mchakato wa katiba, hata wao wanajua hilo. Wazanzibar kuvunja muungano ni ahueni kubwa sana kwa Tanganyika na pia itaongeza umoja wetu watanganyika. Mtoto akililia wembe mpe. Najua malengo yao ni kujiunga na OIC wakitarajia kupata misaada ya waarabu.
 
Na bet kuwa Kikwete hamalizi muda wake.

....hakustahili hata kupewa awamu ya pili maana katika awamu ya kwanza hakuna cha maana chochote alichokifanya zaidi ya usanii na uVDG. Asipomaliza awamu hii Watanzania wengi watajawa na furaha ya hali ya juu ya kuondokana na msanii ambaye hakustahili hata kuwa mjumbe wa nyumba 10 10
 
Kikwete ana afya njema sana.. kwa yote haya cjasikia hata kaugua.... Mganga wake kiboko
 
Nyinyi Wazanzibari why to go all the hard way? Njia rahisi na fupi ya kuachana na Muungano huwa mnapewa
kila baada ya miaka 5 lakini hamtaki kuitumia. Njia hiyo ni KUACHANA NA CCM KATIKA SANDUKU LA KURA.
Kipigieni kura chama kingine mbadala muone, haitachukua hata miaka 2 mnapata Zanzibar yenu.

Maadamu mnaendelea kuikumbatia CCM sahauni kamwe kupata hiyo Zanzibar yenu. The last nail to the coffin
of Zanzibar out to the UNION ni huo muswaada mpya uliopelekwa bungeni na Celina Kombani, kama wawakilishi
wenu CCM + CUF = SUK watauipisha kama ulivyo basi hilo suala litabakia utopia, kwani hakuna RAIS yeyote kutoka
CCM atakayeiachia Zanzibar Count my words. Huo muswaada wa Katiba mpya, RAIS ni alpha na omega na kwa
mambo yalivyo sasa msitarajie hata siku moja RAIS wa JMT atatoka tena Zanzibar, Mlionjeshwa Mwinyi na huo ndio
mwisho wenu. Mgombea wa Urais wa JMT kutoka Zanzibar in this era is NOT ELECTABLE, ni garasha kwa maneno mengine
kwa mgombea yeyote kutoka Tanganyika hata akiwa Mtikila na DP yake.

you said it all....
 
Binafsi cjui kama tunafaidika na muungano wa zanzibar. Kwanza wazanzibar wengi sana wanapewa vyeo huku bara bila sababu za msingi, mm cna uhakika kama kuna watanganyika wanaofanya kazi zanzibar especially kwenye serikali yao. Wabunge wa zanzibar wanakuja dodoma, ila sisi hatuna wawakilishi zanzibar, pia hata mawaziri wengi tu bara wanatoka zanzibar ila sisi hatuna waziri zanzibar. Huu muungano hauna usawa kabisa, natamani hata kesho ufike ukomo.
 
ok sasa mkifanikiwa ule udongo uliyochanganywa na waasisi wa taifa hili mtautenganisha vipi?

Udongo kitu gani? Kwani wewe unaamini matambiko? Kama unaamini katambike kwenu sisi wengine hatuamini na hatutaki Muungano uliopo
 
nafananisha madai yenu na kifaranga kikishakuwa kina mkana ***** na kujitegemea.

Do Mkuu king'amuz you make my day .Halafu,umeacha kwa makusudi, au kuogopa bann, au what ever ,Nadhani ulitaka kuongeza kifaranga kikishakuwa kama ni kijogoo kinajifanya tayari jogoo kinajirusha hata kwa mamaeke.
 
Muungano ukivunjika tutaingia kwenye matatizo makubwa, lazima Muungano uwepo kwa sasa. Tatizo walioko hawana nia ya dhati kushughulikia matatizo ya muungano, sasa mambo yanavyozidi kuparaganyika wenzetu wanapata nafasi ya kufanya wanachotaka. Hatujui mwisho wake lakini sioni uwezo wa JK kuishikilia nchi isiparaganyike kwa sasa.

Taja hayo matatizo yatakayokuwepo angalau matano (5) tu pia taja faida angalu tano (5) tu za Muungano
 
Back
Top Bottom