CCM original
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 373
- 68
- Thread starter
- #21
mkuu mleta mada hiyo semena kama ina posho ninaomba kuudhuria!
haina posho wala maji ya kunywa.
mkuu mleta mada hiyo semena kama ina posho ninaomba kuudhuria!
miaka 20 iliyopita, tulikua sawa kiuchumi na nchi za malaysia,indonesia,singapore,korea leo hii tupo bado dunia ya 3 huko hizo nchi nilizotaja zipo dunia ya pili kimaendeleo.Unafikiri tatizo ni nini kwa nchi yetu?nchi kama malaysia walichukua mbegu ya michikichi kigoma,leo hii mafuta yote ya kula kama kiwanda cha Murzah tunategemea toka malaysia.Umewahi pita njia ya bagamoyo au kisarawe ukaona malori ni mangapi ya mkaa yanayopita kila siku kwenda dar kuuza mkaa?jee kila lori lingeambiwa linunue dawati 1 tuu kwa ajili ya wanafunzi wanaokaa chini tatizo hili lisingekua limeisha?nina maswali mengi sana ila haya tuu yanaweza kukufanya ukaichukia CCM daima ingawa ndiyo unapotegemea watoto wapate kwenda chooHabari?
Kumekuwa na wimbi kubwa sana la vijana ktk mitandao ya kijamii ambao wamekuwa wanaishutumu, kuishambulia, kukosoa, kuhitaji ufafanuzi na hata hufika mahali hujenga maneno ya mzaha na kejeli kwa viongozi waandamizi wa CCM na serikali.
Kuna viongozi wachache huwa wanatolea ufafanuzi na majibu mambo mbalimbali, Nape Nnauye, Mwigulu Nchemba, na Januari makamba, ni viongozi wachache ambao huwa wanakuja kutoea ufafanuzi na majibu.
Lakini hata hivyo huwa wanajikuta wanajibu hoja zinazowahusu maisha binafsi kwa vile wanapotezwa na mashambukizi ya hoja zenye kupoteza mijadala. Wakishtuka wanajikuta wanajibu matusi, kejeli na mambo binafsi.
Tumetokea wanaCCM wachache ambao tumeamua kujibu hoja mbalimbali ktk mitandao ya kijamii dhidi ya watu hao. Majibu yao na mashambulizi yao kwetu ni kuwa "tunatumwa" na "tunalipwa". Jambo ambalo si kweli kwani sisi hujibu na kutetea kama wao wafanyavyo. Tena wanafika mbali na kusema tunalipwa shilingi elfu saba.
Baada ya kutafakari na kuona hali hii nimeona nitoe wito wa wanaCCM ambao huwa tunajibu hoja, kuitetea kueneza itikadi na sera ya CCM ktk mitandao ya kijamii tujenge umoja wenye mlengo mmoja.
Nachukua orodha ya wote ambao tuko ktk social networks ili tufanye seminar/mkutano wetu . Lengo ni kufahamiana na kuona namna iliyo bora ya kujibu hoja zao ktk mitandao ya kijamii . Vilevile itafanya na itasaidia kueneza itikadi na sera ya chama cha mapinduzi.
Kama ni miongoni mwao(RITz, Zemacopolo, CCMone, Sumu, m23, etc) naomba wote tushirikiane ktk hili
Namna ya usajili wa majina halisi nitawajulisheni pindi unitumiapo PM yako. Utaratibu utakuwa kama ifuatavyo: ukishatuma PM yako nitalazimika kutazama posts zako zote hapa JF ili kujiridhisha kama kweli ni mwanaCCM, then nitakutumia ujumbe wa kukujulisha kukubaliwa kwako na kupewa utaratibu unaofuata.
Mahali pa mkutano na tarehe mtajulishwa pindi nikifanya mawasiliano na uongozi wa juu wa chama kwani tutaomba viongozi kadhaa kuhudhuria.
Nategemea kupata ushirikiano wa dhati na wa kutosha kwa hili. CCM original