Taarifa kwa Vyombo vya Habari: Hoja ya Kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu

Bado kunatatizo kwenye hizo siku 14,kwenye kipindi cha bunge au muda wowote tu asilimia 20 ya sahihi ikipatikana unapereka hoja kwa spika.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU BUNGENI KWA MUJIBU WA KATIBA IBARA YA 53A NA KANUNI YA BUNGE, KIFUNGU CHA 133 KUWASILISHWA KWA SPIKA KESHO TAREHE 23/04/2012


· Masharti yametimizwa; wabunge 73 wazalendo wamesaini

· Ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji’

Mnamo tarehe 19/04/2012 wakati nahitimisha hoja ya Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma nilieleza kusudio langu la kuwaomba waheshimiwa wabunge waniunge mkono katika kutia saini zisizopungua asilimia 20 ya wabunge wote ili kuweza kutimiza matakwa ya Katiba ibara ya 53A kwa ajili ya kuwasilisha Bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Mnamo tarehe 20/04/2012 niliandaa orodha ya waheshimiwa wabunge wote na kuisambaza ndani na nje ya ukumbi wa Bunge ili waheshimiwa wabunge wote waweze kutia saini hizo, na mpaka leo tarehe 22/04/2012 orodha hiyo imetimiza idadi ya wabunge wazalendo wanaopigania uwajibikaji 73 kutoka vyama vyote vyenye uwakilishi Bungeni, isipokuwa chama cha UDP ambacho kina Mbunge 1 na hajatia saini waraka huo mpaka sasa.

Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu cha 133 (1) kinasomeka “Mbunge yeyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa Spika ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 53A ya Katiba” na kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (3) kinasomeka “hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitajadiliwa na Bunge isipokuwa tu kama;

(a) “taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku zisizopungua kumi na nne kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa Bungeni;”

Hali kadhalika kanuni za Bunge Kifungu cha 133 (4) kinasomeka kuwa “hoja inayotolewa chini ya Kanuni hii na iliyotimiza masharti ya Katiba,itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo na itaamuliwa kwa kura za siri”.

Hivyo basi baada ya kutimiza matakwa ya kikatiba na kanuni za Bunge kesho tarehe 23/04/2012 tutawasilisha rasmi kwa Spika Taarifa ya Maandishi kwa mujibu wa kanuni 133 (1) na (3) ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa kushindwa kusimamia uwajibikaji wa Serikali Bungeni kwa mujibu wa ibara ya 52 na hivyo kulinda Mawaziri wenye kusababisha matumizi mabaya ya fedha za umma na kulisababishia hasara taifa.

Tunatarajia kwamba siku kumi na nne baada ya kuwasilisha hoja hiyo Bunge litakutana kwa haraka kujadili hoja hiyo ili kuwezesha uwajibikaji na hatua kuchukuliwa za kuhakikisha mapendekezo ya ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na maazimio ya Bunge yanatekelezwa. Hoja hii ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji’ hivyo tunaomba wabunge wazalendo na watanzania wote waiunge mkono ili kuimarisha Uwajibikaji wa Viongozi, kupambana na ubadhirifu na kunusuru uchumi wa nchi na kuchangia katika ustawi wa wananchi.

Kwa niaba ya wabunge wazalendo waliotia saini kuunga mkono taarifa ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni;
…………………………….
Kabwe Zuber Zitto.
Mbunge Jimbo la Kigoma Kaskazini.
22/04/2012.

Kaka Zito!!pambaneni maana ss walalahoi huku uswahilini tumewatuma ninyi mkatutafutie usawa huko mbele,tuko pamoja na nyie wapambanaji wote. Maana hii nchi sasa IMEOZA inaonekana ni ya watu wachache tu sisi wengine tumezaliwa kwa bahati mbaya humu!!HATUKUBALI IKISHINDIKANA MTUPE MAELEKEZO TUFANYEJE!!!AAAAAAAAH BWANA EEEEHH TUMECHOKA AAAAAAHH!!!
 
Maskini PINDA! such a hardworking, clean and nice guy!

Ndiyo hivo tena maana ya uwajibikaji
 
Hata hivyo, wakati wa uchaguzi ujao 2015 lazima tuwahukumu wana CCM waliosaliti. wote ambao tulikuwa hatujajiandikisha tujitahidi tujiandikishe kwa wingi sana ili tuwapige chini maana wakiwa mjengoni wanajifanya wajanja
 
Ndugu wa Tanzania, yamepita majuma,siku,miez na miaka na tumekuwa mashaid wa kile kinaendelea ktk taifa hili,tumeona reaction ya wabunge wote pasipokujal itikadi zao wakiinyooshea kidole serikali. Kuna msemo unasema mwenye macho haambiw tazama. Niwakati wawatanzania kesho kumjuwa Mchawi wetu baada yakuanguka baraza la mawazir lakwanza kunasiri zilifichwa ila tuone je ikiwa Rais huyu ataweza kuwa adhibu mawazir wabovu ktk serikal yake take from me ikiwa atashindwa basi watanzania tujuwe J. K ametuingiza choo chakike/kiume wote watanzania. Maana ukimya wake utakuwa na maovu na kwa hakika "Mene Mene tekel naperezi"!
 
Tunaomba tupate mtandaoni list ya waliosaini(majina) ili tuwajue wanafiki walioacha kusaini wakijua mawaziri hawatekelezi majukumu yao kama inavyo stahili ili tuwawajibishe 2015
 
Katika kutaka kumvisha paka kengele Bwana Zitto hakikisha mnajipanga hata kumshughulikia bosi wake waziri mkuu kwani amekuwa kikwazo cha maendeleo ya taifa letu kutokana na kuteua washirika zake kwa njia ya kulipa fadhila au kukusanya mtaji wa baadaye. Hivyo tatizo kubwa kwa Tanzania ni rais ambaye yuko kitanda kimoja na mafisadi. Tutoe mfano, anamlipa Edward Lowassa aliyeachia madaraka kutokana kashfa tena malipo ya ustaafu wakati hakustaafu bali kuondoka kwa kashfa. Ameruhusu mkewe kuwa na NGO ambayo kimsingi ni njia ya kuchumia utajiri kwa kutumia mgongo wa ikulu. Amekuwa akifuja pesa ya umma kwa ziara zisizo na maana wala ulazima. Amepanua ukubwa wa serikali bila kuzingatia uwezo wa kiuchumi. Makosa ni mengi na wote mnayajua fika. Wakati wa kulikomboa taifa letu ni huu. SAA YA UKOMBOZI NI SASA.
 
kila mtu abebe mzigo wake,haya ndio yaliyomwondoa lowasa.ni vyema mawaziri wajiuzulu kuliko pinda kubebeshwa madhambi ya walio chini yake
 
hehehehehe

tunaelezwa ni upepo tu unapita,kwanza watanzania wenyewe ni mbumbu hawana mbele wala nyuma,upepo utapita na tutawaachia vumbi,kuleni vijana wangu mwisho wasiku tutawaachia nyumba yao na vigoda vyao.
 
Chanzo: H@ki Ngowi

HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU BUNGENI KWA MUJIBU WA KATIBA IBARA YA 53A NA KANUNI YA BUNGE, KIFUNGU CHA 133 KUWASILISHWA KWA SPIKA KESHO TAREHE 23/04/2012

• Masharti yametimizwa; wabunge 73 wazalendo wamesaini
• Ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji'

Mnamo tarehe 19/04/2012 wakati nahitimisha hoja ya Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma nilieleza kusudio langu la kuwaomba waheshimiwa wabunge waniunge mkono katika kutia saini zisizopungua asilimia 20 yawabunge wote ili kuweza kutimiza matakwa ya Katiba ibara ya 53A kwa ajili ya kuwasilisha Bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Mnamo tarehe 20/04/2012 niliandaa orodha ya waheshimiwa wabunge wote na kuisambaza ndani na nje ya ukumbi wa Bunge ili waheshimiwa wabunge wote waweze kutia saini hizo, na mpaka leo tarehe 22/04/2012 orodha hiyo imetimiza idadi ya wabunge wazalendo wanaopigania uwajibikaji 73 kutoka vyama vyote vyenye uwakilishi Bungeni, isipokuwa chama cha UDP ambacho kina Mbunge 1 na hajatia saini waraka huo mpaka sasa.

Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu cha 133 (1) kinasomeka "Mbunge yeyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa Spika ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 53A ya Katiba" na kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (3) kinasomeka "hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitajadiliwa na Bunge
isipokuwa tu kama;

(a) "taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku zisizopungua kumi na nne kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa Bungeni;"

Hali kadhalika kanuni za Bunge Kifungu cha 133 (4) kinasomeka kuwa "hoja inayotolewa chini ya Kanuni hii na iliyotimiza masharti ya Katib mapema iwezekanavyo na itaamuliwa kwa kura za siri".

Hivyo basi baada ya kutimiza matakwa ya kikatiba na kanuni za Bunge kesho tarehe 23/04/2012 tutawasilisha rasmi kwa Spika Taarifa ya Maandishi kwa mujibu wa kanuni 133 (1) na (3) ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa kushindwa kusimamia uwajibikaji wa Serikali Bungeni kwa mujibu wa ibara ya 52 na hivyo kulinda Mawaziri wenye kusababisha matumizi mabaya ya fedha za umma na kulisababishia hasara taifa.

Tunatarajia kwamba siku kumi na nne baada ya kuwasilisha hoja hiyo Bunge litakutana kwa haraka kujadili hoja hiyo ili kuwezesha uwajibikaji na hatua kuchukuliwa za kuhakikisha mapendekezo ya ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na maazimio ya Bunge
yanatekelezwa. Hoja hii ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji' hivyo tunaomba wabunge wazalendo na watanzania wote waiunge mkono ili kuimarisha Uwajibikaji wa Viongozi, kupambana na ubadhirifu na kunusuru uchumi wa nchi na kuchangia katika ustawi wa wananchi.

Kwa niaba ya wabunge wazalendo waliotia saini kuunga mkono taarifa ya
hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni;


…………………………….
Kabwe Zuber Zitto.
Mbunge Jimbo la Kigoma Kaskazini.
22/04/2012.

Samahani sijakuelewa vizuri naomba uniweke sawa Bwana Zito, ina maana baada ya siku 14 wabunge wote mtarudi Dodoma maalum kwa ajili ya kujadili hoja hiyo au itakuwaje hapo? Nimeuliza hivyo kwa maana bunge litaahirishwa kesho na kwa ratiba ya kawaida mlitakiwa kuwa Dodoma tena mwezi Juni kwenye bunge la bajeti.
 
Nina amini kua katika upigaji kura za siri, za kutokua na imani na Mheshimiwa Mizengo Pinda,zitakua nyingi mno.
kwa sababu zifuatazo;



  • Wabunge wa ccm kama kweli walikaa na kuazimia kua walengwa waandike barua kujitoa,basi watataka kuona hilo linatokea.

  • kura ya siri ni ngum kujua ni nani hasa waliotia saini ndan ya ccm wenyewe
  • Hawatapenda kuona maazmio kutoka ktk kikao yamedharauriwa
  • Sababu ingne ya kisiasa, kutoa 8wazri ,ina mana unatoa nafasi 8 wazri ndani ya ccm

Hivo watanzania wenzangu, tunaopenda maendeleo, tutarajie makubwa!!!

 
Najisikia ilifika hatua ya kupiga kura yenyewe, kunauwezekano mkubwa hata wabunge wa CCM kupiga kura ya ndiyo hasa Kama itakuwa siri. Wabunge wengi wanaogopa kuwa wakweli katika kuwajibishana sababu ya mfumo kandamizi ulioshamiri ndani ya chama.
 
:A S-cry: :lalala: Zitto is another bwana. Kazi nzuri mkuu. Huwanajisikia faraja sana CCM wanapoteseka.:bathbaby:
 
Maskini PINDA! such a hardworking, clean and nice guy!

Ndiyo hivo tena maana ya uwajibikaji

Sasa Moony umechemka Pinda anafanya kazi gani zaidi ya kuwa naye mlalamikaji? Watu wanafanya ujinga naye analalamika kama vile siyo semu ya serikali, usijeshangaa siku moja unakwenda kumwambia DC fulani kachukua nyumba na shamba langu naye akasema pole sana ndugu yangu Mungu atalipa!!!!!!!!!!!!!

Kama angekuwa haridhiki na utendaji wa Boss wake angekuwa na chuki kamili dhidi ya mabaya tunayofanyiwa watz na baadhi ya mawaziri wabadhilifu, angeshajiuzulu toka zamani lakini kwa kuwa yuko pale kwa maslahi binafsi ndiyo maana anakuwa mnafiki kwa kujifanya mlalamikaji.
 
14 days regardless of MPs sittings or on urgent bases????

Mama Makinda alinivunja moyo akisema hoja hiyo ni incomplete.

Please tupeni elimu Zitto
 
Last edited by a moderator:
Mbona tayari mchawi ameshajulikana. Ni baba Ridh one. Katoa maagizo kuwa "huo ni upepo tu unapita. Malizeni kikao cha bunge endeleeni na kazi, hakuna kung'atuka mtu". kamuagiza bimkubwa apokee tu hayo majina 73, atayashughurikia akirudi. Anatarajia kesho kukwea pipa kwenda Malawi kwenye mazishi. Chezea ****** wewe!
 
Back
Top Bottom