JIULIZE KWANZA
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 2,569
- 499
Bravo Kabwe na sisi tuko nyu
ma yenu ila angalieni mama mchungaji asikabe vivuli vyetu
ma yenu ila angalieni mama mchungaji asikabe vivuli vyetu
Mkuu MKJJ kosa likowapi, let us not complicate things whether ni hoja au taarifa, movement bado iko under process sasa watu tunataka kukosoa kila pre mature stage ili tuonekane tunajua kama alivyofanya Januari, tuwa-encourage wazalendo wenzetu rather than discouraging them.Nadhani hapa kuna makosa kidogo. Kitakacholetwa kesho siyo hoja yenyewe bali "taarifa ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu". Hoja yenyewe itatolewa kwenye kikao cha bunge kitakachoijadili hoja hiyo. Lengo la kuleta "taarifa hiyo" ni kumwambia spika kuwa matakwa ya asilimia 20 yametimizwa. Naamini spika atawapa muda huo ili kujadili. Hili pia linaweza kuzuia mawaziri wanaotajwa wasijiuzulu sasa na kusubiri hoja hiyo kwa madai ya kwamba kama wabunge watapiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu basi rais atavunja bunge!
Hiyo sign tu ya kuwa PM hatakiwi inatosha kupeleka signal kwa rais kuwa serikali yake akiwemo yeye hawafai.Hii hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ingebadilishwa, badala yake iwe hoja kutokuwa na imani na rais.
I have observed that Pinda seemed to be very small tortories in Kikwete's team, so the Vote of no Confidence be for the head of the state.
Yeah mbele kwa mbele kama Baba Mwanaasha anajitia mjuaji, bora kumwaga ugali!!
akivunja bunge ni right move maana naye kwa mujibu wa katiba atajiuzulu ili makamu wake aongoze kwa muda huku uchaguzi mkuu ukiandaliwa!!Nadhani hapa kuna makosa kidogo. Kitakacholetwa kesho siyo hoja yenyewe bali "taarifa ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu". Hoja yenyewe itatolewa kwenye kikao cha bunge kitakachoijadili hoja hiyo. Lengo la kuleta "taarifa hiyo" ni kumwambia spika kuwa matakwa ya asilimia 20 yametimizwa. Naamini spika atawapa muda huo ili kujadili. Hili pia linaweza kuzuia mawaziri wanaotajwa wasijiuzulu sasa na kusubiri hoja hiyo kwa madai ya kwamba kama wabunge watapiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu basi rais atavunja bunge!
Chanzo: H@ki Ngowi
HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU BUNGENI KWA MUJIBU WA KATIBA IBARA YA 53A NA KANUNI YA BUNGE, KIFUNGU CHA 133 KUWASILISHWA KWA SPIKA KESHO TAREHE 23/04/2012
• Masharti yametimizwa; wabunge 73 wazalendo wamesaini
• Ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji'
Mnamo tarehe 19/04/2012 wakati nahitimisha hoja ya Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma nilieleza kusudio langu la kuwaomba waheshimiwa wabunge waniunge mkono katika kutia saini zisizopungua asilimia 20 yawabunge wote ili kuweza kutimiza matakwa ya Katiba ibara ya 53A kwa ajili ya kuwasilisha Bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.
Mnamo tarehe 20/04/2012 niliandaa orodha ya waheshimiwa wabunge wote na kuisambaza ndani na nje ya ukumbi wa Bunge ili waheshimiwa wabunge wote waweze kutia saini hizo, na mpaka leo tarehe 22/04/2012 orodha hiyo imetimiza idadi ya wabunge wazalendo wanaopigania uwajibikaji 73 kutoka vyama vyote vyenye uwakilishi Bungeni, isipokuwa chama cha UDP ambacho kina Mbunge 1 na hajatia saini waraka huo mpaka sasa.
Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu cha 133 (1) kinasomeka "Mbunge yeyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa Spika ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 53A ya Katiba" na kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (3) kinasomeka "hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitajadiliwa na Bunge
isipokuwa tu kama;
(a) "taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku zisizopungua kumi na nne kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa Bungeni;"
Hali kadhalika kanuni za Bunge Kifungu cha 133 (4) kinasomeka kuwa "hoja inayotolewa chini ya Kanuni hii na iliyotimiza masharti ya Katib mapema iwezekanavyo na itaamuliwa kwa kura za siri".
Hivyo basi baada ya kutimiza matakwa ya kikatiba na kanuni za Bunge kesho tarehe 23/04/2012 tutawasilisha rasmi kwa Spika Taarifa ya Maandishi kwa mujibu wa kanuni 133 (1) na (3) ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa kushindwa kusimamia uwajibikaji wa Serikali Bungeni kwa mujibu wa ibara ya 52 na hivyo kulinda Mawaziri wenye kusababisha matumizi mabaya ya fedha za umma na kulisababishia hasara taifa.
Tunatarajia kwamba siku kumi na nne baada ya kuwasilisha hoja hiyo Bunge litakutana kwa haraka kujadili hoja hiyo ili kuwezesha uwajibikaji na hatua kuchukuliwa za kuhakikisha mapendekezo ya ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na maazimio ya Bunge
yanatekelezwa. Hoja hii ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji' hivyo tunaomba wabunge wazalendo na watanzania wote waiunge mkono ili kuimarisha Uwajibikaji wa Viongozi, kupambana na ubadhirifu na kunusuru uchumi wa nchi na kuchangia katika ustawi wa wananchi.
Kwa niaba ya wabunge wazalendo waliotia saini kuunga mkono taarifa ya
hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni;
…………………………….
Kabwe Zuber Zitto.
Mbunge Jimbo la Kigoma Kaskazini.
22/04/2012.
Nadhani hapa kuna makosa kidogo. Kitakacholetwa kesho siyo hoja yenyewe bali "taarifa ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu". Hoja yenyewe itatolewa kwenye kikao cha bunge kitakachoijadili hoja hiyo. Lengo la kuleta "taarifa hiyo" ni kumwambia spika kuwa matakwa ya asilimia 20 yametimizwa. Naamini spika atawapa muda huo ili kujadili. Hili pia linaweza kuzuia mawaziri wanaotajwa wasijiuzulu sasa na kusubiri hoja hiyo kwa madai ya kwamba kama wabunge watapiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu basi rais atavunja bunge!
hii inaonyesha kwamba sasa bunge la tanzania linakuwa bunge