Taarifa kwa Vyombo vya Habari: Hoja ya Kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU BUNGENI KWA MUJIBU WA KATIBA IBARA YA 53A NA KANUNI YA BUNGE, KIFUNGU CHA 133 KUWASILISHWA KWA SPIKA KESHO TAREHE 23/04/2012


· Masharti yametimizwa; wabunge 73 wazalendo wamesaini

· Ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji’

Mnamo tarehe 19/04/2012 wakati nahitimisha hoja ya Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma nilieleza kusudio langu la kuwaomba waheshimiwa wabunge waniunge mkono katika kutia saini zisizopungua asilimia 20 ya wabunge wote ili kuweza kutimiza matakwa ya Katiba ibara ya 53A kwa ajili ya kuwasilisha Bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Mnamo tarehe 20/04/2012 niliandaa orodha ya waheshimiwa wabunge wote na kuisambaza ndani na nje ya ukumbi wa Bunge ili waheshimiwa wabunge wote waweze kutia saini hizo, na mpaka leo tarehe 22/04/2012 orodha hiyo imetimiza idadi ya wabunge wazalendo wanaopigania uwajibikaji 73 kutoka vyama vyote vyenye uwakilishi Bungeni, isipokuwa chama cha UDP ambacho kina Mbunge 1 na hajatia saini waraka huo mpaka sasa.

Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu cha 133 (1) kinasomeka “Mbunge yeyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa Spika ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 53A ya Katiba” na kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (3) kinasomeka “hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitajadiliwa na Bunge isipokuwa tu kama;

(a) “taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku zisizopungua kumi na nne kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa Bungeni;”

Hali kadhalika kanuni za Bunge Kifungu cha 133 (4) kinasomeka kuwa “hoja inayotolewa chini ya Kanuni hii na iliyotimiza masharti ya Katiba,itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo na itaamuliwa kwa kura za siri”.

Hivyo basi baada ya kutimiza matakwa ya kikatiba na kanuni za Bunge kesho tarehe 23/04/2012 tutawasilisha rasmi kwa Spika Taarifa ya Maandishi kwa mujibu wa kanuni 133 (1) na (3) ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa kushindwa kusimamia uwajibikaji wa Serikali Bungeni kwa mujibu wa ibara ya 52 na hivyo kulinda Mawaziri wenye kusababisha matumizi mabaya ya fedha za umma na kulisababishia hasara taifa.

Tunatarajia kwamba siku kumi na nne baada ya kuwasilisha hoja hiyo Bunge litakutana kwa haraka kujadili hoja hiyo ili kuwezesha uwajibikaji na hatua kuchukuliwa za kuhakikisha mapendekezo ya ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na maazimio ya Bunge yanatekelezwa. Hoja hii ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji’ hivyo tunaomba wabunge wazalendo na watanzania wote waiunge mkono ili kuimarisha Uwajibikaji wa Viongozi, kupambana na ubadhirifu na kunusuru uchumi wa nchi na kuchangia katika ustawi wa wananchi.

Kwa niaba ya wabunge wazalendo waliotia saini kuunga mkono taarifa ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni;
…………………………….
Kabwe Zuber Zitto.
Mbunge Jimbo la Kigoma Kaskazini.
22/04/2012.
 
Kumbe kuna mwelekeo. Ila kwa sasa shida ni pinda ama jk au ni kuwapa taarifa kwamba hata km jk kagoma ila wananchi hawataki. Tupeni mwelekeo bora wabunge wazalendo mungu awaongoze tutashinda.
 
Yeah mbele kwa mbele kama Baba Mwanaasha anajitia mjuaji, bora kumwaga ugali!!
 
Nchi yangu Tanzania inanajisiwa mchana kweupe huku rais akichekelea bila kuchukua hatua,
tuko nyuma yenu viongozi wetu wazalendo
 
pamoja wabunge wetu wazalendo! Yy si anajifanya ni kichwa cha NAZI kweli? Sasa 'M4C' inamkumba.. Go Zito.. Go wambunge wazalendo, tupo pamoja.....
 
Kumbe kuna mwelekeo. Ila kwa sasa shida ni pinda ama jk au ni kuwapa taarifa kwamba hata km jk kagoma ila wananchi hawataki. Tupeni mwelekeo bora wabunge wazalendo mungu awaongoze tutashinda.

Shida ni JK mkuu.Pinda ni mshauri tu hivo kazi yake ni kumwambia tu Mh. Wabunge wamewakataa hawa wezi kina Mkulo & Co.Sasa Majibu ya Baba Mwanaasha eti TULIA HUU NI UPEPO TU UNAPITA!Is he Serious?Rejea Suala la Jairo.Pinda alisema bayana kwamba angekuwa na Mamlaka angekwisha mfukuza saa ileile,****** aliporejea kutoka kuswali ughaibuni alisemaje?Tatizo ni JK anapenda publicity na ujiko kwamba yeye ndiye msikivu hali ni kiziwi na ni careless taker sana.Mi nilidhani Sheria inaruhusu Wabunge kuipiga chini Ikulu kabisa ndio ingekuwa bomba.:A S angry:
 
daima mbele nyuma ni mwiko waheshimiwa wabunge wazalendo wote mlioweka sahihi azimio hilo. wananchi tuko pamoja nanyi na mwenyezi mungu awatangulie.
 
Maana yake ni kwamba, huyu mama Anne(speaker) alikuwa anataka kuimbizia hii hoja kwa bunge lijalo la June, kumbe anatakiwa aitishe bunge tena ndani ya siku 14 baada ya kuipokea hii hoja kesho, kwa ajili ya mstakabali huu tu. hapo sasa patamu hapo!!
 
Nadhani hapa kuna makosa kidogo. Kitakacholetwa kesho siyo hoja yenyewe bali "taarifa ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu". Hoja yenyewe itatolewa kwenye kikao cha bunge kitakachoijadili hoja hiyo. Lengo la kuleta "taarifa hiyo" ni kumwambia spika kuwa matakwa ya asilimia 20 yametimizwa. Naamini spika atawapa muda huo ili kujadili. Hili pia linaweza kuzuia mawaziri wanaotajwa wasijiuzulu sasa na kusubiri hoja hiyo kwa madai ya kwamba kama wabunge watapiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu basi rais atavunja bunge!
 
Dah hiyo imetulia nadhani JK akiwakingia kifua atajuta mara atakapopitia hotuba za wabunge akiwa magogoni na chadema wakati wanasubiri kupiga kura ya kumuondoa PM waandae maandamano nchi nzima wagawane maana pia mratibu wa maandamano ni KAMANDA JASIRI G. Lema, kitaeleweka tu ba mwanaasha atajuta kukumbatia marafiki zake
 
aluta continua....lazma wango´ke pm,jk and if pocbo reshuffling the cabinet to interviewed cabinet!!!
 
Mpango huu ni mzuri maana watu watawajua wabunge wao kama wapo kwa maslahi ya Rais, Mawaziri, Wabunge wenyewe au wapo kwa ajili ya maslahi ya wananchi. Itajulikana tu na bahati nzuri vuguvugu la mabsdiliko liko juu sana nchini.
Kitakachofuata sasa ni zomea zomea kwa wabunge ambao hawakusaini kuunga. mkono mpango huo. Itajulikana tu.
 
Hii hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ingebadilishwa, badala yake iwe hoja kutokuwa na imani na rais.

I have observed that Pinda seemed to be very small tortories in Kikwete's team, so the Vote of no Confidence be for the head of the state.
 
salute mh.zitto,msisitizo ni kuitishwa bunge la dharura ili mambo yasisubiri mwezi juni.
 
Back
Top Bottom