Hivi kweli watu 5,600 Lema anataka waende mahakamani wakafanyaje? kweli hizi akili za kunguru sijawai kuona toka nianze kufuatilia kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi wa mbunge sijawai kusikia mbunge akiwataka waliompigia kura waende mahakamani..
yaani watu waache kazi zao wakashinde mahakamani, anajuaje kama wote waliompigia kura ni Chadema?
Lema hajaita mtu, na wanaoenda ni walompigia kura bila kujali tofauti zao. Na mashahidi ni wapiga kura wenyewe walokuwepo kwenye hiyo mikutano ya kampeni anayoshutumiwa lema kuwatukana hao greens. Sasa watamteteaje kama hawajui muendelezo wa kesi kaka?
Kuhusu hayo maandamano ni hivi..
1. Watu walokuwa mahakamani walikuwa wengi sasa saa ya kutoka lazima waonekana mafungu (ikaonekana ni maandamano.)
2. Walokuwa mahakamani wasingeweza kusubiriana atoke mmoja mmoja. Ingewachukua siku nzima au mbili mpaka waishe mahakamani.
3. Kutoka mahakamani mpaka ofisi ya Lema sio mbali hivyo, so Lema aliamua kutembea kwa mguu (yuko huru ni jimbo lake). Kumbuka kuna kina mama wanatembea kilometres wakitafuta maji na dispensary, so hakuna ubaya mbunge kutembea kidgo.
4. Barabara alopita Lema kuelekea ofisi ndio exit road toka mahakamani, hata wewe ungekuwepo ungepita hapo hapo kaka.
5. Ukipita au kukutana barabara moja na mtu unaempenda au ulemchagua haunyimwi kumsabahi au kumshangilia.
Kwa hayo machahce nilowaza kwa upeo wangu mdogo na mnaouita wa "mvuta bangi" bado polisi hawana grounds yeyote wa ku-rule out kuwa kulikuwako maandamano.
Pia Ofisini Kwa Lema ni ofisi ya wanajimbo walomchagua Lema so
1. Wana ruhusa wa kufika pale muda wowote wa kazi kukutana na mbunge wao
2. Lema kama mwenye ofisi ana uwezo wa kualika mgeni yeyote haswa waajiri wake (wapiga kura wake)
Kwa hayo machache pia Polisi hawana uwezo wa ku-rule out kuwa kaalika watu kwa njama.
Kama wafuasi na wote walofika mahakamani hawakuwa hata na fimbo wala viwembe mifukoni, basi walikuja kwa AMANi kushiriki haki yao ya kikatiba. Sioni ground yeyote ambayo polisi ina ruhusa ya kuwanyima haki yao, zaidi wangetakiwa kuwalinda mpaka shauri liishe lakini cha ajabu polisi ndio walikuwa na silaha ready to kill or surpress wananchi. Nani mkorofi hapo?
Kuhusu kuwaita wafuasi kuwa nii wakaa vijiweni.
1. Ni kweli wengi wetu nikiwamo mimi ni wa vijiweni (hustahili kutukumbusha)
2. Tungekuwa wapi pengine? Tungelala home?
3. Tungekuwa shamba lakini mbolea za ruzuku na pembejeo ndio mnalipwa nazo ninyi mnaotutusi leo. Mashambammewapa maswahiba wenu wazungu na viongozi. Unafahamu ya morogoro.
4. Vijiweni atleast tunajadili ya msingi na kupeana deal japo ndogo. Inatusaidia kununa sukari(2300tshs) na chumvi tunarudisha home kwa wazee wetu walotesekea ilokuwa EAC lakini now mnawatukana.
5. Kijiweni ninapopiga viatu rangi na elimu yangu ndio panaponiwezesha kumsomesha mdogo wangu na kumtibu bibi. Wakati ninyi na ndugu zenu mnasoma nje au ndani kwa mkopo 100% na kutibiwa nje au ndani kwa priviledges.
Vijiwe ni vingi kuliko ofisi na ndio vinatulisha. Je hali ikibadilika ukarudi kijiweni utafurahi nikikutenga na kukudharau eti kisa wewe uko kijiweni? Mtu ni Utu.
Kwa niaba ya wapenda maendeleo wote nawasilisha