Newfame
JF-Expert Member
- Feb 27, 2015
- 485
- 1,134
TAARIFA KWA UMMA JUU YA KASHFA YA RUSHWA INAYOZIKABILI BAADHI YA KAMATI ZA BUNGE.
TANZANIA YOUTH PATRIOTS (TYP) tumepokea kwa Masikitiko Makubwa Taarifa ya baadhi ya Kamati za Bunge kuhusika na kupokea Rushwa kutoka kwa Mashirika ya Umma.
Tukiwa kama Vijana Wazalendo wenye Uchungu na Taifa letu tumehuzunishwa sana na Wawakilishi hawa tuliowachagua na kuwatuma watuwakilishe sisi Wananchi na badala yake wao wamekwenda Kujiwakilisha wao wenyewe na Kuwawakilisha wale ambao wana faida nao za moja kwa moja.
Tuliwachagua tukijua kuwa watakwenda kupigania Maslahi ya Taifa kama suala la Ajira kwa Vijana,Katiba Mpya na Changamoto nyingine nyingi ambazo Taifa zinaikabili badala yake imekuwa kunyume na matarajio yetu.
Tukiwa kama Wazalendo kwa Sauti Moja tunamuomba Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Job Ndugai badala ya kuwabadilishia Wajumbe Kamati, atengue uteuzi wao Mara moja hadi Taratibu za Uchunguzi zitakapo kamilika.
Aidha tunavitaka Vyombo vingine husika kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) na Kamati ya Maadili kuchukua Hatua Stahiki dhidi ya wote waliohusika na Kashfa hii ili Kulinda na Kurudisha Heshima ya Bunge Tukufu La Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.
Vilevile Tunapenda kuwapongeza Wabunge, Hussein Bashe(Nzega) na Zitto Kabwe(Kigoma) kwa Kitendo Chao cha Kizalendo kujiuzuru Ujumbe wa Kamati Husika na Kashfa hizo ili kupisha Uchunguzi, tunatoa wito kwa Wabunge wengine ambao ni Wajumbe wa Kamati hizo kuiga Mfano huo.
Tunaamini Bunge pamoja na Taasisi nyingine husika zitalifanyia kazi suala hili kwa Umakini mkubwa kwa Maslahi ya Watanzania wote.
Imetolewa na:-
Ofisi Taarifa
Tanzania Youth Patriots(TYP) Taifa.